TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Hivi tanesco wapo humu?

Sent using OnePlus 6T Maclaren Edition
 
Wape takukuru then wewe endelea na mambo yako. Hawa wanajifanya wajanja. Dogo mmoja maisha yameinuka kama uyoga. I swear sio mshahara tu, rushwa ipo ya kufa mtu.

dottoz,
 
Mkipost nyie mnaandika vitu vya msingi kweli utazani watu. majuzi hapa mtaani kulitokea shida ya low voltage nawapigia najibiwa eti bora huko kuna low voltage kuna pengine umeme umezima kabisa, nikajiuliza kumbe hata low voltage ni huduma ya TANESCO. afu mda ule nawaeleza tatizo wananiambia wana taarifa tangu juzi, ha haaaa.
 
Mkipost nyie mnaandika vitu vya msingi kweli utazani watu. majuzi hapa mtaani kulitokea shida ya low voltage nawapigia najibiwa eti bora huko kuna low voltage kuna pengine umeme umezima kabisa, nikajiuliza kumbe hata low voltage ni huduma ya TANESCO. afu mda ule nawaeleza tatizo wananiambia wana taarifa tangu juzi, ha haaaa.
Huwa najiuliza mheshimiwa Rais anapohujumiwa hivi mkurugenz hajui?? Haiingii akilini kutufanya wajima. Wkt Rais anapapambana tuhame ulimwengu huu wangese wanatupigia porojo. Kuna watoto wengi wamehitimu vyuo, atuondolee hawa warugaruga wapiga porojo

Maana sisi tunawajibika kwa Rais
 
Nina mambo mawili

1. Kimara mwisho njia hii ya kwenda bonyokwa kila siku umeme unakatika na sio unakatika kwa muda mfupi no. Unakatika muda mrefu bila matangazo bila samahani bila chochote tunaomba kujua hili tatizo litakwisha linii????Maana imekuwa ni kawaida sio siku moja mbili wala tatu ni almost kila siku umeme lazima ukatike hapa muda huu saa moja na robo usiku umeme umekatika kwa mara ya tatu rupo gizani naomba kujua tatizo hapa ni nini na kama linajulikana nini kinashindikana kulitatua mara moja lisijirudie?nina mashaka sana kama mna wataalamu wanaojua kazi yao maana kama wapo basi ingekuwa tatizo likitatuliwa halijirudii.tuliaminishwa bomba la gesi likikamilika hakuna kukatika kwa umeme sasa nimejiridhisha issue sio umeme kidogo issue ni wataalamu wetu kutatua matatizo yaliyopo

2.naomba kujulishwa uhusiano wa mvua kunyesha na umeme kukatika hapa kimara hakuna siku ya mvua umeme lazima ukatike embu tanesco tuambieni kitaalamu uhusiano uliopo wa mvua na kukatika kwa umeme maana ni aibu kwa nchi hii ya viwanda na janga la umeme,shame on you
 
naomba kujua ni jinsi gani naweza kufanya ili kampuni yangu iingizwe kwenye list ya contractors wanaotambuliwa na Tanesco wa kutandaza nyaya kwenye majengo na kuchora ramani ,ili niweze kuhudumia wananchi,
natanguliza shukrani zangu
 
Sehemu zngne mkuu ,hata sio za kuziishi kabisa, kama unapesa ni bora kununua solar ya watt 200 na betr za kutosha kama 2 kubwa utaepukana na tatzo la umeme kopa tu hata benki uwe na umeme wa ziada wa solar hiyo maana huko dar joto lake si mchezo hata kwa feni tu sawa hilo ndo wazo langu kwako mkuu,chukua hata watt 100 tu utumie hata kwa feni tu na taa basii..

Maana hawa Tanesco sio wa kutegemea 100% zote,kuna baadhi ya sehemu wako vzuri umeme bwelele kama ununio,n.k huko umeme full muda wote ukikatka kdogo unarudi,kuna kinyanambo a mafinga pale.
manyusi,
 
Nenda Tanesco ilyokarb nawe ,mshike mtumish mmoja wa pale ongea naye atakuelekeza,fuata hayo af ulete mrejesho.
Asante,
naomba kujua ni jinsi gani naweza kufanya ili kampuni yangu iingizwe kwenye list ya contractors wanaotambuliwa na Tanesco wa kutandaza nyaya kwenye majengo na kuchora ramani ,ili niweze kuhudumia wananchi,
natanguliza shukrani zangu
 
Nahisi kuna hujuma inatengenezwa Tanesco dhidi ya serikali haiwezekani kila siku ifika saa 8 au 9 usiku umeme Bunju unakatwa alafu unarudishwa alfajiri.

Yaani katika mazingira yetu ya uswahili hiyo ndio mida ya wezi na Wanga
Alafu Tanesco ndio mida yao ya kukata umeme kila siku iendayo kwa Mungu
Mm sielewi hawa Tanesco uwa wanatumwa na vibaka au ndio hujuma kuelekea uchaguzi mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitawekewaje umeme in an overnight. I am extremely in need. Tanesco please help

Kila kitu tayari. But no surveyor surveyed
 
Kwa niaba ya wananchi wa mji mdogo wa MALAMPAKA ulioko wilaya ya MASWA mkoa wa SIMIYU ktk jimbo la MASWA MAGHARIBI chini ya mbunge wangu ndugu Mashimba (CCM) naandika kulalamikia upatikanaji wa umeme kwa sababu umekuwa kero kubwa na kusababisha athari nyingi na kubwa za kiuchumi na kijamii kwetu sisi wananchi na hata tumeshindwa kuvumilia

Kwa takribani wiki mbili mfululizo sasa umeme umekuwa ukikatika katika hovyo hata mara 20 kwa siku. Na kuna wakati TANESCO mnakata hata masaa zaidi ya 48 bila umeme

Mji wa Malampaka ni wa pili kwa ukubwa katika wilaya ya Maswa baada ya makao makuu ya wilaya.

Mji huu ndiyo kituo kikuu cha reli kwa mkoa wote wa Simiyu.

Aidha huu ni mji wa viwanda vidogo dogo vingi hasa vya kusaga nafaka (unga), kukoboa mpunga na mji huu ni kituo kikuu kimkoa kwa biashara ya Michele

Mji huu mdogo unakadiriwa kuwa na wakaazi (population) ya watu karibu 25,000

Umeme ni nishati muhimu sana kwetu kwa ajili ya shughuli za uzalishaji kwenye viwanda vidogo dogo vya kusaga nafaka (unga), kukoboa mpunga ili kupata mchele, kupoza juice kwenye friji ili tuuze tujipatie kipato, umeme na saluni za kunyoa na za wanawake, stationeries kuendeshea computers nk

Si hivyo tu, bali tunategemea umeme wa TANESCO ili uendeshee machine ya kusukuma maji kwenye matenki ili wakaazi wapate maji kwenye magati

Sasa hebu fikiria, masaa 48 unapokuwa huna umeme unawaathiri watu kwa kiwango gani? Ni wazi kabisa, kuwa, ni kwa kiwango kikubwa!

Kibaya zaidi ni kuwa TANESCO hawatoi taarifa yoyote kueleza tatizo ni nini na litachukua muda gani kutatuliwa. Hivyo hutudharau na kutuacha wananchi ktk sintofahamu kubwa isiyo na maelezo

Nakumbuka waziri wa nishati ndugu Medard Kalemani mapema mwezi Februari, 2018 alikuja hapa Malampaka na kufanya mkutano na wananchi ktk viwanja vya TTCL na kuawaahidi kuwa tatizo la kukatika katika umeme Malampaka na Maswa kwa ujumla litakuwa historia ifikapo mwezi Mei, 2018 kwa sababu serikali inajenga line kubwa mpya mbili za umeme;

¶ Moja toka Ibadakuli, Shinyanga hadi Maswa kisha Bariadi

¶ Na ya pili toka Mwabuki - Misungwi - Mwanza ipite hapa Malampaka hadi Maswa kisha iungane na ile inayotoka Ibadakuli - Shinyanga kuelekea Bariadi

Aidha Waziri aliahidi na kuagiza yafuatayo kufanyika pia;

¶ Mosi, TANESCO kufungua ofisi ndogo hapa Malampaka kuhudumia wananchi.

Hili limefanyika japo kiuhalisia hakuna ofisi bali kuna Tent (turubai) tu na kuna vijana wawili ambao kazi yao ni kupokea malalamiko tu ya wateja

¶ Mbili, TANESCO wajenge kituo kidogo cha kupozea umeme pale MASWA ili kusaidia kuleta stability ya upatikanaji umeme ktk eneo hili

Sina hakika kama maagizo haya yalitekelezwa na wahusika kwa sababu laiti kama ingekuwa hivyo, watu tusingekuwa tunalalamika hivi hata kuona kuwa umeme ni tatizo kuliko hata virusi vya CORONA!

HIVI, ninavyoposti taarifa sasa ikiwa ni SAA 4:30 usiku huu, hatuna umeme tangu jana!

Ulikatika around saa 9alasiri jana tarehe 10/3/2020. Ukawaka tena leo saa 6 mchana. Umekuwa hivyo hivyo ukiwaka na kukatika katika hivyo na umekatika moja kwa moja ilipofika saa 12jioni na haieleweki utarudi lini!!

Sasa hebu TANESCO mtuambie, mna matatizo gani? Mnakwama wapi? Kwanini inakuwa ni ngumu kuwasiliana na sisi wateja wenu ili tujue na watu tujiandae kutafuta nishati mbadala?

Msituambie kuwa tatizo ni mvua zinazonyeesha na kuathiri miundo mbinu ya usafirishaji umeme

Hili linaweza lisiwe kweli kwa sababu hata umeme unapokuwa umewaka, unakuwa haupo stable. Ndani ya saa moja unaweza kuwaka na kuzima hata mara 10 mpaka hufikia watu tunajisemea "labda fundi mitambo anajifunza kuwasha na kuzima!!"

Rais JOHN POMBE MAGUFULI mwaka 2015 alipoingia madarakani, alitamba sana kuwa umeme wa mgawo na ile hali ya kukatika katika hovyo nchi hii itakuwa historian

Sasa hii ahadi yake mbona inakuwa kama zilikuwa nguvu ya soda ya coca cola tu? Kwanini mnanyanyasa wananchi hivi nyie serikali ya CCM ya wanyonge??
 
Week hii kuanzia jtatu mpaka jtano umeme unakatika asubuh unarud jion,week iliyopita fuse ilizingua baada ya masaa24 ndio wakaja rekebisha,leo tena fuse ile ile imeharibika tangia saa saba mchanaa mpka usiku huu bado hamjaja na taarifa tumeshatoa hamna umeme mpka saiz na ni arusha jijini et tanesco mnatutia hasara asee kinyamaa yaan hizi juhud za mh raisi mnazihujumu walah,watu tumefungua viwanda vidogo tunashindwa fanya kazi sijui asee maendeleo yanakuja vp hapa kwa mindset hii ya tanwsco asee
 
Week hii kuanzia jtatu mpaka jtano umeme unakatika asubuh unarud jion,week iliyopita fuse ilizingua baada ya masaa24 ndio wakaja rekebisha,leo tena fuse ile ile imeharibika tangia saa saba mchanaa mpka usiku huu bado hamjaja na taarifa tumeshatoa hamna umeme mpka saiz na ni arusha jijini et tanesco mnatutia hasara asee kinyamaa yaan hizi juhud za mh raisi mnazihujumu walah,watu tumefungua viwanda vidogo tunashindwa fanya kazi sijui asee maendeleo yanakuja vp hapa kwa mindset hii ya tanwsco asee
Ni eneo gani wilaya na namba yako ya simu tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
naomba kujua ni jinsi gani naweza kufanya ili kampuni yangu iingizwe kwenye list ya contractors wanaotambuliwa na Tanesco wa kutandaza nyaya kwenye majengo na kuchora ramani ,ili niweze kuhudumia wananchi,
natanguliza shukrani zangu
Tafadhali pata udhibitisho wa EWURA ndio uje TANESCO na vithibitisho vyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom