TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Mbagala kuu tamesco wawajibishwe
Kiukweli nasikitikq sana kuleta malalamiko yangu hapa kwani kwa siku huku mbagala kuu umeme unazimwa mara 10 kwa siku tumepiga simu tanesco wamesema watarekebisha ilq kiukwwli wanatukwaza sana mana ni miezi sita sasa watafanyia huu upuuzi hasa usiku
Tafadhali onyedha taarifa kamili za

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Wengi au mwenyewe

Toka.saa ngapi

Tuma hata inbox kwa ufatiliaji na hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafadhali onyedha taarifa kamili za

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Wengi au mwenyewe

Toka.saa ngapi

Tuma hata inbox kwa ufatiliaji na hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app

Eneo la mbagala kuu
Wilaya ya temeke
0762987034
Tatizo la kukatika umeme mara kwa mara kwa mara,kwa siku mara 10
Wengi sanna nyumba zaid ya 200
Hii ni miezi sita tatizo hili limeanza zaidi mida ya usiku
 
Huko huo umeme ulishawashinda, mara propaganda utasikia tumeweka transfoma nyingi zaidi na kubwa, mara tumejenga kituo kidogo, sub station, na tatizo haliishi lipo palepale.

EWURA wapo tu na mishahara minono! Wanachodhibiti wanadhibitiwa nao na vikao vyenye posho!

Everyday is Saturday......................... 😎
 
Eneo la mbagala kuu
Wilaya ya temeke
0762987034
Tatizo la kukatika umeme mara kwa maravkwa siku mara 10
Wengi sanna ntumba zaid ya 200
Hii ni miezi sita tatizo hili limeanza
Je umewahi kutoa taarifa ofisi zetu za mbagala kama ndio tusaidie namba ya taarifa uliyopatiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo: Chini ya Mwatulole Secondary Mpakani na Mwabasabi.

Kata: Buhalahala

Wilaya :Geita Mjini.

Mkoa: Geita

Tatizo: Ukosefu wa miundombinu ya Umeme (Nguzo 15) katika eneo hili.

Taarifa ya Tatizo: Tupo wakazi zaidi ya 100 kwenye eneo hili la chini ya mwatulole secondary hatuna Umeme kwa kipindi kirefu na tumeshindwa kuvuta umeme maana kila tukienda tanesco, idadi ya nguzo ili kuweza kumfikia mwananchi mmoja ni zaidi ya mbili, hivyo tunaambiwa huo ni mradi, na Bajeti yake haipo.
Sasa tunaomba Msaada wa Nguzo 15 ambazo zikisambazwa katika eneo hili zitakuwa zimetoa mwanya kwa sie wanachi kuvuta umeme kwa wepesi zaidi.

Eneo letu lipo mpakani mwa kata mbili yaani Nyankumbu na Buhalahala. Pia ni mpaka wa mtaa wa mwatulole na mwabasabi.

Mtaa wa mwabasabi uliopo kata ya Nyankumbu wao wana mradi wa REA unoendelea chini ya mkandarasi White /New City.

Hali hii inapelekea eneo hili kuonekana kama vile ni kijijini ili hali ni mjini.

Ushauri wangu: Ikiwa bajeti ya upatkanaji wa nguzo tunazoomba haipo ,
Tunaomba basi zile nguzo za HT (High tension ) zenye urefu wa 14M ambazo huwa zinaoza chini , Tufungiwe hizo baada ya kuwa zimekatwa kwa 5M na kubakiwa 9M ili tuanze kutumia kisha tutakuwa tukibadirsha kulingana na zinapopatikana.

Mawasiliano: 0787 537 570.

Kazi njema






Sent using Tecno Sufuria
Ahsante kwa taarifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom