TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kukatika ovyo kwa umeme nini tatizo?
Huku kwetu Mtoni Kijichi na Mgeninani,umeme unawaka na kukatika kama kuna mtoto anachezea, toka March,2020 ili tatizo lilianza hadi leo 26 May,2020 hakuna utatuzi,mfano leo unawaka kuanzia dakika 2 hadi 10 na kuzima pia saa 8:00 hadi saa 8:02 umezima hadi sasa ninapo post thread hii hakuna umeme ila nguzo na nyaya zake zipo, leo kazi imekuwa hiyo tu.Idd el fitri na Idd pili umeme umekuwa ukizima na kuwaka.Kwani mnakwama wapi kama mna professional engineer na technicians?Hii haionyeshi uwaredi wenu kabisa.
 
Wilaya ya chemba mkoani Dodoma tanesco wanasema wanasubiri bajeti ya mwaka ujao. Hawana nguzo ila za kununua zipo. Si wananchi hatujui nguzo za kununua au za REA na viongozi wanasema gharama za miundo mbinu ni za tanesco na sio mteja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo: Sakina kwa Iddi

Wilaya: Arumeru

Simu: 0621 28 21 03

Tatizo: Kukatika umeme mara kwa mara (rejea ref7795 posted on 20th May) ninavyo ongea hatuna umeme sasa kwanini hamtatui hili tatizo? Nitapost daily utakapo katika labda hii itakuwa kama kumbukumbu ni mara ngapi tunakuwa na adha hii
 
Naomaba kujua hivi ni kweli Tanesko mnauza nguzo moja 370,000?
Unataka kununua nguzo kwaajili gani?
1. Kujengea nyumba
2. Kujengea Banda
3. Kutengeneza uzio
4. Kuni?

Ninavyoelewa TANESCO wanahudumia kuhusu umeme. Hawauzi nguzo. Nguzo ni material tu kama yalivyo material mengine pale umbali unapokuwa hadi mita 80.
Kwakifupi umbali ndio unasababisha waweke nguzo au wasiweke.

Ukiuziwa nguzo, Dai risiti ya nguzo.
 
Refer to Jamii forum references number 7795 n 7855 there is no power as usual. It's only 16 hours ago I have reported this thanks it was fixed in the midnight but it is not a long last solution a few minutes ago power went off again and we don't know how long it will take. Why don't you guys fix this problem that has been bothering us for more than 17 years? Au hamjui mnacho kifanya ni mnabahatisha tu
 
AHSANTE KWA TAARIFA TUNAIFANYIA KAZI

Sent using Jamii Forums mobile app
Napenda nitoe Shukrani kwa utendaji kazi wenu, tatizo langu kwenye post no 7738
Lilitatuliwa tarehe 20 may. Asanteni sana.

Wahusika pia waliomba samahani kwa kuchelewa kujenga mfumo huo, kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

MUNGU awatie nguvu mzidi kusonga mbele.

Asante



Sent using Tecno Sufuria
 
Napenda nitoe Shukrani kwa utendaji kazi wenu, tatizo langu kwenye post no 7738
Lilitatuliwa tarehe 20 may. Asanteni sana.

Wahusika pia waliomba samahani kwa kuchelewa kujenga mfumo huo, kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.

MUNGU awatie nguvu mzidi kusonga mbele.

Asante



Sent using Tecno Sufuria
Karibu sana mpendwa mteja wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO Control Number inachukua muda gani kutoka? baada ya suvery kuja kusuvery inakaribia wiki control number sijapata.
 
Eneo: Chini ya Mwatulole Secondary Mpakani na Mwabasabi.

Kata: Buhalahala

Wilaya :Geita Mjini.

Mkoa: Geita

Tatizo: Ukosefu wa miundombinu ya Umeme (Nguzo 15) katika eneo hili.

Taarifa ya Tatizo: Tupo wakazi zaidi ya 100 kwenye eneo hili la chini ya mwatulole secondary hatuna Umeme kwa kipindi kirefu na tumeshindwa kuvuta umeme maana kila tukienda tanesco, idadi ya nguzo ili kuweza kumfikia mwananchi mmoja ni zaidi ya mbili, hivyo tunaambiwa huo ni mradi, na Bajeti yake haipo.
Sasa tunaomba Msaada wa Nguzo 15 ambazo zikisambazwa katika eneo hili zitakuwa zimetoa mwanya kwa sie wanachi kuvuta umeme kwa wepesi zaidi.

Eneo letu lipo mpakani mwa kata mbili yaani Nyankumbu na Buhalahala. Pia ni mpaka wa mtaa wa mwatulole na mwabasabi.

Mtaa wa mwabasabi uliopo kata ya Nyankumbu wao wana mradi wa REA unoendelea chini ya mkandarasi White /New City.

Hali hii inapelekea eneo hili kuonekana kama vile ni kijijini ili hali ni mjini.

Ushauri wangu: Ikiwa bajeti ya upatkanaji wa nguzo tunazoomba haipo ,
Tunaomba basi zile nguzo za HT (High tension ) zenye urefu wa 14M ambazo huwa zinaoza chini , Tufungiwe hizo baada ya kuwa zimekatwa kwa 5M na kubakiwa 9M ili tuanze kutumia kisha tutakuwa tukibadirsha kulingana na zinapopatikana.

Mawasiliano: 0787 537 570.

Kazi njema






Sent using Tecno Sufuria
 
Kwakweli inasikitisha zima washa ya tanesco inadumaza maendeleo ya wananchi kwa ukanda huu, kwa siku wanaweza kuzima na kuwasha zaidi ya mara 10, vyombo husika tafadhali mufatilie na kuchunguza sababu haya ya kuwasha zima zaidi ya mara kumi na kuunguza vitu vya umeme, ni miezi sita sasa tangu hiki tatizo lijitokeze.

Je, ni kweli miezi 6 hawajapata ufumbuzi aa tagizo hili
 
Me nipo hapa maeneo ya Kizuiani leo washakata zaidi ya mara 10
 
Mbagala kuu tamesco wawajibishwe
Kiukweli nasikitikq sana kuleta malalamiko yangu hapa kwani kwa siku huku mbagala kuu umeme unazimwa mara 10 kwa siku tumepiga simu tanesco wamesema watarekebisha ilq kiukwwli wanatukwaza sana mana ni miezi sita sasa watafanyia huu upuuzi hasa usiku
 
Halafu bado mnasema mtu aendelee kuongoza miaka kumi mingine huu ni uwendawazimu
 
Back
Top Bottom