Eneo: Chini ya Mwatulole Secondary Mpakani na Mwabasabi.
Kata: Buhalahala
Wilaya :Geita Mjini.
Mkoa: Geita
Tatizo: Ukosefu wa miundombinu ya Umeme (Nguzo 15) katika eneo hili.
Taarifa ya Tatizo: Tupo wakazi zaidi ya 100 kwenye eneo hili la chini ya mwatulole secondary hatuna Umeme kwa kipindi kirefu na tumeshindwa kuvuta umeme maana kila tukienda tanesco, idadi ya nguzo ili kuweza kumfikia mwananchi mmoja ni zaidi ya mbili, hivyo tunaambiwa huo ni mradi, na Bajeti yake haipo.
Sasa tunaomba Msaada wa Nguzo 15 ambazo zikisambazwa katika eneo hili zitakuwa zimetoa mwanya kwa sie wanachi kuvuta umeme kwa wepesi zaidi.
Eneo letu lipo mpakani mwa kata mbili yaani Nyankumbu na Buhalahala. Pia ni mpaka wa mtaa wa mwatulole na mwabasabi.
Mtaa wa mwabasabi uliopo kata ya Nyankumbu wao wana mradi wa REA unoendelea chini ya mkandarasi White /New City.
Hali hii inapelekea eneo hili kuonekana kama vile ni kijijini ili hali ni mjini.
Ushauri wangu: Ikiwa bajeti ya upatkanaji wa nguzo tunazoomba haipo ,
Tunaomba basi zile nguzo za HT (High tension ) zenye urefu wa 14M ambazo huwa zinaoza chini , Tufungiwe hizo baada ya kuwa zimekatwa kwa 5M na kubakiwa 9M ili tuanze kutumia kisha tutakuwa tukibadirsha kulingana na zinapopatikana.
Mawasiliano: 0787 537 570.
Kazi njema
Sent using
Tecno Sufuria