TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Ngoja TUSUBIRIE... Kuna mteja hapa analamika alilipia 2018 Hadi Leo umeme haujawaka
Tafadhali onyesha jina lake

Namba ya simu

Tarehe aliyolipia

Wilaya

Tuifatilia kupitia mifumo yetu
 
Fahamu hii
IMG_20200914_110855_703.jpg
 
Ngoja nimshawish anipe
Muambie afike hapo ofisini kama ni Kisarawe aulizie Prisca atamsikili hauwajibiki kumshawishi kwa kuwa hauna mfumo wa kuona anachosema
 
NAONA WANATUHUDUMIA FASTA FASTA,MKUU UMEWATWANGIA NINI? INGEKUWA NDO HIVI TANGU ASUBUHI TUSINGEKUWA NA FOLEN AISEEE.
 
NASHUKURU NIMRPEWA CONTROL NAMBA NGOJA NIKALIPIE..
TANESCO NI MDA GANI NIKISHALIPIA LEO..UMEME MTAKUJA KUNIUNGANISHIA?
 
NASHUKURU NIMRPEWA CONTROL NAMBA NGOJA NIKALIPIE..
TANESCO NI MDA GANI NIKISHALIPIA LEO..UMEME MTAKUJA KUNIUNGANISHIA?
Inategemea

Umbali wa mita 30 ndani ya siku 30 za kazi

Umbali wa mita 60 ndani ya siku 60 za kazi

Umbali wa mita 90 ndani ya siku 90 za kazi
 
Naomba niseme kitu Tanesco sijajua tatizo lenu liko wapi......

Hivi inafikiaje hatua watu wako karibu na njia za umeme lakini hawapati? mbaya zaidi eneo lipo 170 meter kutoka kwa Sumai, umeme ulikoishia...... Kwa upande mwingine ni around 60meter kutokea kibaha mjini hapa mto ndio umetenganisha na hawana umeme wanatumia solar,

Naomba mtizame eneo lililopo kiluvya madukani karibu na waziri mkuu sumai..... Eneo linaitwa mpiji, lipo mpakani mwa kibaha mjini na shamba la NSSF linawakazi wengi tu.......

Suala la umeme limeanza kupigiwa kelele since 2013 nikiwa pale, REA ikaja na ikapita

SAD
 
Tafadhali onyesha namba yako ya simu kwa mrejesho zaidi
 
ndugu mteja utapigiwa simu
Hili jibu hata halimalizi kiu ya swali, manake ule mkataba wa huduma kwa wateja mmeeleza muda kila hatua, !! sasa muda umepita halafu eti utapigiwa simu!! piga simu sasa umweleze hayo!!
 
Inategemea

Umbali wa mita 30 ndani ya siku 30 za kazi

Umbali wa mita 60 ndani ya siku 60 za kazi

Umbali wa mita 90 ndani ya siku 90 za kazi
Duuh hiyo kila mita siku moja? hiyo inasababishwa na wingi wa wateja au upungufu wa vifaa?
 
Hapa mkuu kubali mmeteleza hamkutaka kufuata hatua mkataka ujanja.
Naomba msaada enyi TANESCO tafadhali.Mimi ni mkazi nipo mkoa wa songwe.IPO hivi mwezi wa july mwaka huu tulijichangachanga fedha ili tupate huduma ya umeme kwani bado kama nguzo mbili kutufikia.tukachanga zikafika lakinne,.miongoni mwetu tukampa ili azilipe.kabla ya kulipa miongoni mwetu akasema ana namba ya ofisa wa tanesco hivyo ni vema wawasiliane ili atueleze utaratibu wa kulipa.walipowasiliana na yule ofisa yule ofisa akasema,kunanguzo zipo za ziada naweza kuwaletea leteni hizo fedha .ni kweli afisa yule akapewa fedha.
Baada ya wiki moja alileta waya pamoja na nguzo.
KIMBEMBE KILIPOANZIA.
Yule afisa akaleta vibarua wakachimba mashimo nakusimika nguzo na kufunga waya.tulimwita mtumishi mmoja anayehusika kupima aligoma kupima,akadai hizo nguzo hazikuja kihalali mazingira hayo,hivyo ili atupimie ni shart tulipie upya hizo nguzo.
Ilitushtua sana habari hiyo kwani hatukutegemea habari kama hizo.tukajua labda anamambo yake.tukampigia mpimaji mwingine naye kaongea vivyohivyo.
Tukaenda kwa ofisa mmoja pale wilayani tukamwelekeza habari yote akatutishia kutwitia security na takukuru.tumejaribu mala kadhaa kumpigia afisa aliyetuletea hizo nguzo mwanzoni alionesha kuwajia juu wale wapimaji,lkn alipoona wamemkazia naye kaingia mitini na hapokei simu yetu hasa akigundua ni sisi tunampigia
TUNATAKA MSAADA GANI?
Msaada tunaotaka je huyu ofisa tumfanye nini?
Je hili swala ni rushwa?
Je hili swala mwishowe uwe nn?
Tunajiuliza Je tukienda kwa meneja hatatuitiwa security na takukuru?
Kunawakati nilisikia waziri anasema nguzo ni bure mbona wanasema tulipe?
Kama ni bure kwa nn wasitupatie mita ?.tunaomba msaada please
 
Inategemea

Umbali wa mita 30 ndani ya siku 30 za kazi

Umbali wa mita 60 ndani ya siku 60 za kazi

Umbali wa mita 90 ndani ya siku 90 za kazi
WENZAO KENYA NASIKIA WANAFANYA WIRERING HADI KUWASHA UMEME NI SERIKALI UKIWAKA WANAANZA KUKUKATA KODOGO KIDOGO MPAKA GHARAMA ZAO ZINAISHA..TANZANIA MNAFELI WAPI? SIKU 30 MITA 30 KINACHOSABABISHA IWE SIKU 30 ZA KAZI NI NINI? TANESCO
 
Hivi inakuwaje tanesco mnakuta sehemu viwanja vimepimwa na vina namba kabisa halafu nyinyi mnapitisha umeme mkubwa katikati ya kiwanja cha MTU!!!!
 
Back
Top Bottom