Mh waziri yapata miezi miwili sasa hapa wikayani kyela kumekuwa na kero kubwa ya ukataji wa umeme, yani ni kila siku kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa tatu usiku, kuanzia tar 1 mpaka tar 30, Mwanzoni tulifikiria labda kuna matengenezo au kuna swala liko nje ya uwezo wa Tanesco , lakini katika kufatilia kiundani zaidi imegundulika kwamba wafanyabiashara wanaouza Sola power biashara yao imedoda tangu kuwe na umeme wa uhakika wilayani hapa, hivyo basi ili kuhakikisha sola zinauzika ni kuhakikisha kuwa kuna kua na uhaba wa umeme kwa mfululizo.
Uongozi wa wilaya wamelifumbia macho hili swala kana kwamba hakuna wawakilishi wa serikali wilayani hapa , mh waziri tunaomba utusaidie kwasababu watu wengi ambao shughuli zao zinategemea umeme shughuli zao zimesimama kabisa, tunaomba uliangalie hili swala kwa undani zaidi.
Pia tupieni macho uongozi wa hii wilaya imekua kama ni wilaya ambayo haipo katika jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwani imekua ni kama kisiwa kilichojitenga viongozi wa wilaya kuamua kuwa kimya hata katika maswala ya msingi kama haya.