TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi

Kama wewe ni Tanesco kweli, nisaidie hili na unipe majibu hapa.

Nina kibanda changu sehemu furani nimekijenga juzi juzi hivi, lakini sehemu niliyojenga kuna umeme wa REA ulishapita ni mita kama 150 pengine less, naomba kujua , je inawezekana na mimi kuungiwa kwa gharama za REA ambazo ni 27 elfu au utaratibu ni tofauti tena ?
 
Kwanini Umeme mnakata kata muda wote?

Pia mtindo wa kata Umeme dakika moja, rudisha Umeme mnatuunguzia vifaa vyetu vya ndani.

Narudia TANESCO Bukombe mnazingua sana
 
Mh waziri yapata miezi miwili sasa hapa wikayani kyela kumekuwa na kero kubwa ya ukataji wa umeme, yani ni kila siku kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa tatu usiku, kuanzia tar 1 mpaka tar 30, Mwanzoni tulifikiria labda kuna matengenezo au kuna swala liko nje ya uwezo wa Tanesco , lakini katika kufatilia kiundani zaidi imegundulika kwamba wafanyabiashara wanaouza Sola power biashara yao imedoda tangu kuwe na umeme wa uhakika wilayani hapa, hivyo basi ili kuhakikisha sola zinauzika ni kuhakikisha kuwa kuna kua na uhaba wa umeme kwa mfululizo.

Uongozi wa wilaya wamelifumbia macho hili swala kana kwamba hakuna wawakilishi wa serikali wilayani hapa , mh waziri tunaomba utusaidie kwasababu watu wengi ambao shughuli zao zinategemea umeme shughuli zao zimesimama kabisa, tunaomba uliangalie hili swala kwa undani zaidi.

Pia tupieni macho uongozi wa hii wilaya imekua kama ni wilaya ambayo haipo katika jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwani imekua ni kama kisiwa kilichojitenga viongozi wa wilaya kuamua kuwa kimya hata katika maswala ya msingi kama haya.
 
Mh Rais, tunafahamu unavyopambana kuhakikisha mambo yanakaa sawa kila mahali. Lakini uongozi wa wilaya ya kyela wakishirikiana na Tanesco Kyela kwa tamaa zao za pesa za wafanyabiashara wanahujumu juhudi za serikali za kuhakikisha kunakuwa na umeme wa uhakika.

Hii ni kutokana na kudoda kwa biashara ya Sola power wameamua kwa makusudi kukata umeme kila siku kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 3 usiku, wakijua kwamba kwa kufanya hivo wananchi watakimbilia kununu solar, tunaomba mh rais uingilie kati swala hili, maana linaumiza wananchi wengi.
 
Hiyo Hali sio ya huko tu ni maeneo mengi Tanzania hata huku kwetu leo wamekata kuanzia saa moja hadi sasa naamini watarejesha jioni
 
Mh waziri yapata miezi miwili sasa hapa wikayani kyela kumekuwa na kero kubwa ya ukataji wa umeme, yani ni kila siku kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa tatu usiku, kuanzia tar 1 mpaka tar 30...
Tutahakikisha uongozi wote wa Tanesco Kyela unang'olewa , hii kero wanayopata wana kyela sijawahi kuiona popote Tanzania , ukicheka na nyani utavuna mabua
 
Tutahakikisha uongozi wote wa Tanesco Kyela unang'olewa , hii kero wanayopata wana kyela sijawahi kuiona popote Tanzania , ukicheka na nyani utavuna mabua
Tafadhali onyesha namba yako ya simu kwa hatua zaidi
 
Hivi JPM akimaliza muda wake ...mtaturudisha kule kule kwenye mgao tena na kukatika katika kwa umeme mfululizo au tumetoboa tayari?
 
jikite kwenye hoja badala ya kutafuta namba za simu za walalamikaji ili kuwateka na kuwaua , jibu kwanini hiyo kata kata umeme Kyela inafanyika kinyama kiasi hicho , vinginevyo utadharauliwa vibaya sana !
Unapotoa taarifa makao makuu ni wajibu wako kutoa taarifa kamili kwani ufatiliaji wenye weledi unafanyika kupitia taarifa kamili
 
Habar wakuu. Ni mteja wa Tanesco . Nimepata tatizo la kuunguliwa na Mita yangu Nashukuru Tanesco wameshughulikia haraka na nikafungiwa Mita Nyingine wiki iliyoisha. Sasa Ule Umeme Wa mwanzo umeisha, nikaenda Tanesco Leo siku ya tatu kuomba wanisajilie Mita wananiambia hakuna umeme. Ni kweli umeme umekatika hivyo naomba Kama Kuna uwezekano nisajiliwe huko ofisini kwenu
 
Naomba kuuliza ikiwa mteja ana uhitaji na nguzo mbili je kuna gharama yeyote kwa sasa??
 
Habar wakuu. Ni mteja wa Tanesco . Nimepata tatizo la kuunguliwa na Mita yangu Nashukuru Tanesco wameshughulikia haraka na nikafungiwa Mita Nyingine wiki iliyoisha. Sasa Ule Umeme Wa mwanzo umeisha, nikaenda Tanesco Leo siku ya tatu kuomba wanisajilie Mita wananiambia hakuna umeme. Ni kweli umeme umekatika hivyo naomba Kama Kuna uwezekano nisajiliwe huko ofisini kwenu
Nashukuru Tatizo langu limepatiwa Ufumbuzi baada ya Kupiga Simu Huduma kwa wateja huko makao makuu. Asante Sana. Ila ushauri wangu kwenu Kuna haja ya kuwa na Generator la dharura katika ofisi za Tanesco Wilaya ili umeme ukikatika Huduma ziwe zinaendelea kutolewA. Asante Sana.
 
Back
Top Bottom