TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Meneja wa Tanesco Monduli awajibike kwa athari zozote zitakazotokea. Watu wameripoti kuhusu miti iliyoko karibu Na Nyumba zao inagusa waya Na kutoa moto Mara kwa mara wakiomba ushirikiano wa kuikata hakuna kinachofanyika wengine report ni mwaka sasa
Tafadhali onyesha eneo na namba ta simu kwa hatua zaidi
 
Tatizo lilianza nilipofungiwa mita ,alikuja mfanyakazi wenu kuunganisha umeme sasa baada ya kufanya kazi akamwambia wife ampe chochote ili mita isiwe inakula unit,qkadai apewe 70000 ,wife akamgome yule bwana akaomba ngazi akapanda juu ya mita sasa sijui aliichezea vipi akashuka nakuondoka zake akqmwambia wife nnajua utanitafuta tu akadai kuwa si ameona 70000 ni nyingi ataona,ndugu zangu tokea siku hiyo utafikiri ninakiwanda humu ndani ,wakati ni tv,taa zipo 9 na frigde lakini umeme wa elfu 50 haumalizi siku kumi yaani,baada ya kufuatilia saana ikaonekana yule jamaa alitapeli sehem nyingine na kashafukuzwa kazi ila sasa nikaelekezwa kuandika barua mpaka wa leo ni maumivu kabisa,ninakaa madale tunahudumiwa na wilaya ya ubungo,mtaa wetu unaitwa kwa mzungu.
Tafadhali onyesha namba ya simu na namba ya mita kwa hatua zaidi
 
Ahsante kwa taarifa tunafanyia kazi
TANESCO kila nikitoa malalamiko yangu unaniambi mnafanyia kazi week sasa imeisha sijapata majibu kutoka kwenu wala kupewa taarifa ya chochote kuhusu malalamiko yangu
 
Nahitaji kufungiwa umeme nipo bukoba mjin bei ya sasa ni hipi?! Kuna taarifa bei imeshuka ni kweli??!;
 
Pugu Mwakanga toka jana tarehe 02/02/2021 saa nne usiku mpaka sasa ninapoandika message hii hakuna umeme, shida ni nini? Nikafikiri labda mtatoa taarifa lakini kimya
 
Pugu Mwakanga toka jana tarehe 02/02/2021 saa nne usiku mpaka sasa ninapoandika message hii hakuna umeme, shida ni nini? Nikafikiri labda mtatoa taarifa lakini kimya
tafadhalo onyesha namba ya simu wilaya na eneo kwa hatua zaidi
 
Nataka kujua kama baada ya mkuu wa sasa hivi kuondoka madarakani mtarudia tena ule uhuni wenu wa zamani wa mgao wa umeme na kuzima umeme makusudi mara kwa mara
 
Nataka kujua kama baada ya mkuu wa sasa hivi kuondoka madarakani mtarudia tena ule uhuni wenu wa zamani wa mgao wa umeme na kuzima umeme makusudi mara kwa mara
Asante endelea kufurahia huduma
 
Nimeungiwa umeme na nahitaji nunua luku lakini naambiwa namba haitambuliki msaada plz
 
Tabata siku hizi umeme umekuwa ukikatika katika hovyo majira ya usiku Yani unakatika baada ya dakika chache unarudi tena unakatika hasahasa kuanzia saa nne usiku kuendelea
 
Halafu Kuna watu wanatumia umeme bure kabisa huu mwaka wa tatu mita yao ilipigwa shot ikaacha kusoma
 
Meter 14386222278 wilaya butiama namba ya simu 0764004600 nimeungiwa tarehe 30/1/2021
 
Nimenunua umeme kupitia NMB lakini kila nikiweka token inakuwa rejected Msaada tafadhali
 
TANESCO Kimara mwisho jana umeme ulikatika mda mfupi,ukarudi.Leo ndio komesha,tangu asubuhi unawaka dk 5,unakatika masaa mawili,mwendo ni huo hadi sasa mchana huu.
Nawashauri kama kuna kitu kifaa kinasumbua line hii msikilazimishe,mnatutesa wananchi,fungeni kifaa kingine ili tatizo la umeme Kimara mwisho maeneo yote ya dawasco,matangini,sokoni,n.k umeme utulie.Wewe nishahidi yangu sasa tuna muda wa miezi mingapi naripoti same issues every week?mwaka sasa!hebu vaa viatu vyetu,how long shall we wait kupata huduma ya uhakika kimara?na umeme unakatwa ubungo line nzima
 
Pugu Mwakanga toka jana tarehe 02/02/2021 saa nne usiku mpaka sasa ninapoandika message hii hakuna umeme, shida ni nini? Nikafikiri labda mtatoa taarifa lakini kimya
Kaka hiyo ni kwanzia pugu, majohe, kigogo, mpaka chanika mwisho ,leo ni siku ya 3 hamna umeme kabisa..

Ukitaka kuchaji simu unaenda gmboto[emoji3][emoji3][emoji3] .

Alafu kuna watu wanasimama vifua mbele kabisa na kusema tatzo la umeme halipo Tanzania..

TANESCO mnatia kinyaaaaaaaa....
 
Back
Top Bottom