Tatizo lilianza nilipofungiwa mita ,alikuja mfanyakazi wenu kuunganisha umeme sasa baada ya kufanya kazi akamwambia wife ampe chochote ili mita isiwe inakula unit,qkadai apewe 70000 ,wife akamgome yule bwana akaomba ngazi akapanda juu ya mita sasa sijui aliichezea vipi akashuka nakuondoka zake akqmwambia wife nnajua utanitafuta tu akadai kuwa si ameona 70000 ni nyingi ataona,ndugu zangu tokea siku hiyo utafikiri ninakiwanda humu ndani ,wakati ni tv,taa zipo 9 na frigde lakini umeme wa elfu 50 haumalizi siku kumi yaani,baada ya kufuatilia saana ikaonekana yule jamaa alitapeli sehem nyingine na kashafukuzwa kazi ila sasa nikaelekezwa kuandika barua mpaka wa leo ni maumivu kabisa,ninakaa madale tunahudumiwa na wilaya ya ubungo,mtaa wetu unaitwa kwa mzungu.