TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Hayo maeneo umeyataja hata maji ya bomba hayana!!!na yako karibu na ziwa hazizid km20!!

Mwanza bana natamani viongozi (wabunge wa pale) wangelikua na akili, wange kuwa na mpango wa upanuzi wa bara bara kutoka nata mpaka kisesa kuwa njia nne, bara bara ya kutoka igoma via kishiri to buhongwa kuwa njia nne, bara bara ya igombe via kayenze to kisesa kuwa njia nne na bara bara ya igogo mpaka usagara kuwa njia sita!!

Mji unge funguka mpaka raha!!
 
Ni jambo la kushangaza sana! Ni kweli kabisa hayo maeneno yamejengeka lakini hakuna umeme. Unaenda vijijini, sehemu nyingine nyaya zinaenda hata umbali wa mita 400 bila kuwepo nyumba, lakini umeme upo. Mwanza nyumba kwenye hayo maeneno, zipo karibu karibu sana lakini umeme hakuna.

Watu walio mbali na Mwanza, wengi wanaamini marehemu aliipendelea Mwanza, lakini ukweli ni kwamba hakuna cha pekee. Barabara za lami ni za kuhesabu. Barabara ya njia moja ni moja tu ya kilometa 4, mitaani barabara nyingi mashimo matupu, umeme maeneo mengi ya pemebezoni mwa jiji, haujapelekwa.
Umeme na maji ya bomba mwanza mjini inazidiwa parefu na wilaya ya kongwa tena huko ndani ndani kabisa. Geita, shinyanga mjini napo hovyo taabani hakuna maji ya bomba maeneo mengi mpaka leo pamoja na pato kubwa wanalochangia kupitia madini, samaki
 
Ka
Ni jambo la kushangaza sana! Ni kweli kabisa hayo maeneno yamejengeka lakini hakuna umeme. Unaenda vijijini, sehemu nyingine nyaya zinaenda hata umbali wa mita 400 bila kuwepo nyumba, lakini umeme upo. Mwanza nyumba kwenye hayo maeneno, zipo karibu karibu sana lakini umeme hakuna.

Watu walio mbali na Mwanza, wengi wanaamini marehemu aliipendelea Mwanza, lakini ukweli ni kwamba hakuna cha pekee. Barabara za lami ni za kuhesabu. Barabara ya njia moja ni moja tu ya kilometa 4, mitaani barabara nyingi mashimo matupu, umeme maeneo mengi ya pemebezoni mwa jiji, haujapelekwa.
Kabxa mkuu,yaan unashangaa hata barabara za kuingià katkat ya jiji c 4ways, zipo tu kama highway za kawaida, hili wajaribu kuliangalia, mfano kuna barbara ya pamba hapo kuelekea sahara kwa kupitia Aghakan, ni kama uchochoro tu na ukizngatia kuna mabanda ya wafanyabiashara, usalama wao kwel upo chini
 
Kwani wabunge wenu wanasemaje akina Mabula wa Nyamagana na yule wa Ilemela ?
Ingawa wetu wengi wamejitahidi kujenga majumba mazuri tatizo umeme wa tanesco hauwafikii

Maeneo kama Sawa, Nyashishi, Nyamongoro, Bukaga, Kangae, Ilalila, Kakebe, Kishiri, fumagila kwa kutaja baadhi maeneo hayo wetu wamejenga majumba ya kifahari changamoto ni umeme haupelekwi waziri tunakuomba uishtueshutue tanesco ya mwanza jiji
 
Hii Maada ni Muhimu sana Umeme tumekuwa tukilalamika katika jiji hili la Mwanza lakin wahusika wako kimya lakini nikienda bariad kwetu umeme umefika hadi vijiji vyavingi havina hata nyimba, kwetu nyumbani kuna umeme wakati tuko ndani vijijini lakini hapa Mwanza mpaka unashanga kuna sehemu nyumba nzuri hakuna ata Nguzo
 
Ingawa wetu wengi wamejitahidi kujenga majumba mazuri tatizo umeme wa tanesco hauwafikii

Maeneo kama Sawa, Nyashishi, Nyamongoro, Bukaga, Kangae, Ilalila, Kakebe, Kishiri, fumagila kwa kutaja baadhi maeneo hayo wetu wamejenga majumba ya kifahari changamoto ni umeme haupelekwi waziri tunakuomba uishtueshutue tanesco ya mwanza jiji
Tunashukuru kwa taarifa tumepokea kwa hatua zaidi.Tafadhali tambua usambazaji wa umeme maeneo mbalimbali nchini unaenda kwa awamu mbalimbali hivyo kila eneo litafikiwa kwa awamu zijazo
 
Watu wanafanya maendeleo ila mnakua kikwazo
 
Ingawa wetu wengi wamejitahidi kujenga majumba mazuri tatizo umeme wa tanesco hauwafikii

Maeneo kama Sawa, Nyashishi, Nyamongoro, Bukaga, Kangae, Ilalila, Kakebe, Kishiri, fumagila kwa kutaja baadhi maeneo hayo wetu wamejenga majumba ya kifahari changamoto ni umeme haupelekwi waziri tunakuomba uishtueshutue tanesco ya mwanza jiji
Mwendazake aliahidi kwamba jiji la mwanza litakua kama jiji la Geneva uswizi, ila paka amafariki jiji la mwanza nikama fishing village in Gonoa Italy, mambo hubadilika haraka......
 
Ingawa wetu wengi wamejitahidi kujenga majumba mazuri tatizo umeme wa tanesco hauwafikii

Maeneo kama Sawa, Nyashishi, Nyamongoro, Bukaga, Kangae, Ilalila, Kakebe, Kishiri, fumagila kwa kutaja baadhi maeneo hayo wetu wamejenga majumba ya kifahari changamoto ni umeme haupelekwi waziri tunakuomba uishtueshutue tanesco ya mwanza jiji
Mwanza ni shida tupu, umeme kama ulivyotaja maeneo hayo ni tatizo, shida ya maji ndo usiseme, maeneo ya Kanyerere upatikanaji wa maji ni tatizo kubwa.

Barabara ya kutoka Mkuyuni kupitia Mahina- Kanyerere- Nyangulugulu hadi Machinjioni imejaa mahandaki na maeneo hayo ni ndani ya Jiji.

Mbunge wa Nyamagana yule Mgambo Mabula hana lolote la maana la kuwasaidia Wapiga kura wake kwa matatizo yote hayo
 
Tunashukuru kwa taarifa tumepokea kwa hatua zaidi.Tafadhali tambua usambazaji wa umeme maeneo mbalimbali nchini unaenda kwa awamu mbalimbali hivyo kila eneo litafikiwa kwa awamu zijazo
Atleast umeonesha uwepo wenu hongera kwa hili, ila msiishie kutoa comment hapa, nendeni maeneo husika mkaonane na wadau wenu wenye hizo shida muongee nao.
 
Tunashukuru kwa ushauri taarifa yeyote inayotolewa kuhusu TANESCO inafatiliwa na kufanyiwa kazi kuanzia Makao Makuu hadi eneo husika.Hivyo ondoa shaka
 
Mwanza ni shida tupu, umeme kama ulivyotaja maeneo hayo ni tatizo, shida ya maji ndo usiseme, maeneo ya Kanyerere upatikanaji wa maji ni tatizo kubwa. Barabara ya kutoka Mkuyuni kupitia Mahina- Kanyerere- Nyangulugulu hadi Machinjioni imejaa mahandaki na maeneo hayo ni ndani ya Jiji. Mbunge wa Nyamagana yule Mgambo Mabula hana lolote la maana la kuwasaidia Wapiga kura wake kwa matatizo yote hayo
Nyamagana inahitaji jicho la tatu
 
TANESCO nimefika ofisini kwenu nikihitaji huduma ya kuunganishiwa umeme...mmesema hamjui gharama ya nguzo na bado halijatolewa waraka..hivi waziri pale aliposema elfu 27 alimaanisha nini?

Nguzo zetu wateja? Sisi tuna nguzo?
 
TANESCO nimefika ofisini kwenu nikihitaji huduma ya kuunganishiwa umeme...mmesema hamjui gharama ya nguzo na bado halijatolewa waraka..hivi waziri pale aliposema elfu 27 alimaanisha nini? Nguzo zetu wateja? Sisi tuna nguzo?
Je umefika ofisi ya wapi? Namba ya simu tafadhali
 
Back
Top Bottom