TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Yani huku chang'ombe ndo hatuna umeme toka asubuh mpaka hii saa 5 usiku

Wanatuonea sana Tanesco huku, Kama weekend ya juzi walikata umeme kuanzia Jumamosi saa11 jioni wakaurudisha Jumapili saa2 usiku,,, yaani zaidi ya masaa 24 hakuna umeme
 
TANESCO Mimi nimelipia mwezi wa 12 tarehe 8 Hadi Leo sijafungiwa umeme na niliambiwa umeme utafungwa ndani ya siku 30 hii hipo vipi ??
 
TANESCO Mimi nimelipia mwezi wa 12 tarehe 8 Hadi Leo sijafungiwa umeme na niliambiwa umeme utafungwa ndani ya siku 30 hii hipo vipi ??
Tutakufungia umeme kabla ya tarehe 30 Machi 2022 tafadhali, Tupo kwenye hatua nzuiri sana.
 
Hivi hapa dumila-kilosa mbona kila siku mnakata umeme

Leo hii mshakata tangu sambili hapo kurud paka usiku shida nini

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Mnakata kata sana umeme dumila yaani ni kero sana
Paka muda huu hakuna umeme mnaleta mnakata yaani kama mchezo

Rudisheni umeme dumila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO ni kweli mmefanya marekebieho ya umeme ila kwa hapa Dumila yaani ni kama hakuna lolote ndani ya siku hizi mbili katakata imezid yaani hapo nyuma tulitulia ila kwa sasa imerudia tena yale yale mfano leo hadi sasa mshakata mara 4 na mkikata mnakaa lisaa mkirudisha ni dk 30 halafu mnakata tena
Yaani hapa dumila siku hizi umeme ni tatizo sana as if tupo mashambani daah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TANESCO hivi nyinyi mnatutafuta nini wakazi wa Kimara?jana usiku mlikata umeme,leo hapa mmekata tangu saa mbili asubuhi mpaka mchana huu.

Usiniambie ni hitilafu maana ntakuuliza wiki nzima mnatukatia umeme mlikuwa mnafanya matengenezo gani? Kimara mwisho line ya Dawasco ina shida gani?!
 
Mkoa: Arusha
Halmashauri: Arusha Jiji
Kata: Sokoni 1
Mtaa: Seinevuno
Karibu na kanisa la ZION TEMPLE
.
Hili eneo tangu usiku wa kuamkia leo hadi sasa, mnakata umeme na kurudisha mara kwa mara,
Na sasa tangu 16:30 Mlipokata mara ya mwisho hadi sasa 21:30 hamrudishi umeme.
Sijui mna maana gani, siku hizi mumekuwa HOVYO SANA.
 
Arusha maeneo ya field force pale msikiti wa vibandani kuna nyaya zenu zinaning'inia karibia zifike chini, kazishughulikieni isijekuwa ni excuses za kutukatia umeme mtaa ule 😒
 
Habari tanesco?naomba kujua muda mnaotumia kuunganishia wateja umeme baada ya kukamilisha taratibu za malipo?nipo Dsm kibesa mpigi wahusika wa eneo hili ni tanesco kibamba
 
TANESCO ebu tuelimishemi juu upatikanaji na kuunganisha umeme huku jijini baada ya huu utata wa REA
 
Habari tanesco?naomba kujua muda mnaotumia kuunganishia wateja umeme baada ya kukamilisha taratibu za malipo?nipo Dsm kibesa mpigi wahusika wa eneo hili ni tanesco kibamba
Je umelipia lini? Wilaya gani na namba ya simu tafadhali
 
Mkoa: Arusha
Halmashauri: Arusha Jiji
Kata: Sokoni 1
Mtaa: Seinevuno
Karibu na kanisa la ZION TEMPLE
.
Hili eneo tangu usiku wa kuamkia leo hadi sasa, mnakata umeme na kurudisha mara kwa mara,
Na sasa tangu 16:30 Mlipokata mara ya mwisho hadi sasa 21:30 hamrudishi umeme.
Sijui mna maana gani, siku hizi mumekuwa HOVYO SANA.
Tafadhali onesha namba ya simu
 
Asubuhi tu ya saa 1 mshakata umeme tena kwa kujikatia na nyie kazi yenu ni kujibu mnafanyia kazi ni kazi ipi hyo mnayofanyia huku hakuna mabadiliko yoyote yale tunayoyaona ? Au mnapenda kulalamikiwa TANESCO
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Tafadhaki tujulishe ni nini haswa unataka kujua?
1. Kuna hili suala la nguzo za umeme kununuliwa na mteja.

2. Kama zinahitajika nguzo 2 unapaswa kulipia kiasi gani?

3. Leo (February 2022) ukiomba kupatiwa umeme unapaswa kulipia kiasi gani huku vijijini ambako REA alipaswa kurudi kwa awamu ya pili?

4. Ikiwa hatua kuanzia survey hadi kurekodiwa kwenye computar zimefanyika nini kinafuatia ili kupatiwa umeme.

Ahsante
 
Back
Top Bottom