Napoleone
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 10,087
- 16,036
Hahahha.. mtaelewa tuu.. hahah.. mnakomeshwa maana mliishi vzur sana kipind cha nyuma kwa mzee magu..Tuliaminishwa sana na viongozi kuwa mitambo ya Tanesco zilikuwa zikifanya kazi bila marekebisho kwa muda wa miaka mitano. Ndiyo maana umeme unakatika katika.
Tukaaminishwa tena na viongozi wazalendo wa nchii kuwa maji yamepungua kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme na hii imechangiwa na ukame ndiyo maan umeme unakatika katika ovyo ovyo.
Taseco ikatangaza siku 10 kwa ajili ya mate matengenezo ya mitambo ya umeme ili kumaliza kabisa tatizo la kukatika kwa umeme. Na hii ilifanywa kwa weledi mkubwa tukafunga mkanda siku kumi. Umeme unakatwa saa moja asubuhi unarudi kesho yake yaani saa sita usiku. Tumevumilia nchi ikiwa gizani na kuamini sasa lile tatizo la umeme kukatika katika ovyo inakomeshwa kisawa sawa.
Baada ya ukame mashee na mapadre na viongozi wakuu wa serikali na wananchi kwa ujumla wetu tukafunga na kumwomba Mungu atupe Mvua. Hakika Mungu akajibu maombi Yetu tukapata mvua mabwawa ya kufua umeme yamejaa, mpaka Leo mvua bado zinanyesha sehemu nyingi ya Tanzania.
Naomba kuuliza Tanesco tatizo nini sasa kama mitambo yamerekebishwa na mengine kubadilishwa na mabwawa ya kufua umeme yamejaa na maji. Kwann umeme unaendelea kukatika ovyo je bado kuna mgao wa umeme. Toka last week umeme maeno ya Tegeta mpaka wazo madale yote hayana umeme.
Leo toka asubuhi umeme hakuna shughuli zetu zimesisima. Waziri husika na wahusika wote wa Tanesco tatizo ni nini?
Kwanni mnatuonea sana sisi tabaka la chini?
Wengine hatuna pesa ya kununua Majenerata na solar mnatusaidiaje?