TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tafadhali onesha umelipia kwa jina gani, namba ya simu , wilaya kwa hatua zaidi
Wapuuzi nyie TANESCO kila siku niwapeni taarifa zangu na sioni msaada wowote ,kutoa taarifa lini mtanifungia umeme hamtoi,nishawafuta PM mnanipigia simu mnaniletea ngonjera tu.
 
Najua mna uwezo wa kutupa taarifa ya ratiba yenu ya matengenezo au marekebisho tukajipaga kuliko katakata ya kila siku huku Dar
 
hatuna waziri wa niahati huyo makamba hana lolote hana chochote tangu magu afariki Dunia hakuna chochote kilichofanyika nchi imerudi nyuma kabisa kila siku safari za nje ya inchi kutafuta wawekezaji lakini hana nishati itawezwkana kweli!!
 
TANESCO hivi wale waliolipia umeme tokea mwaka Jana mwezi 10,11 kabla ya tarehe 05/01/2022 na mkawatumia ujumbe wa simu kua wateja wetu wote mliolipia umeme kabla ya Tangazo la mh Rais tutawawekea umeme kabla ya tarehe 30/03/2022 na hizo meseji zilitumwa January hivi hilo tangazo lenu bado lipo valid kweli? Maana kesho ndo mwisho wa mwezi March na umeme bado shida nini?

Watu wanasubiri umeme kwa zaidi ya miezi 4 kweli? Ni Tanzania tu ambapo unalipia huduma kwa control no alafu unasubiri miezi zaidi ya minne..
 
Nimekuja huku Pugu Umeme unazimwa yaani ndani dakika 20 wamekata zaidi ya mara 7.

Mpaka naonda sio chini ya mara kumi na 12 sasa sijui usalama wa vitu vya watu vinavyoungua inakuwaje.

Jitahidini katika hili kwani ni aibu Chama changu ccm
 
Ndio kwa kasi kubwa kabisa, je weww umelipia lini? Namba ya simu tafadhali
Ndugu zangu wa TANESCO, hivi ni kwa nini namba zenu za huduma za dharura huwa hazipatikani kwa wakati!? Namba ambazo zipo katika mitandao ama zilikuwa hazipokelewi na nyingine kujibiwa kuwa hazipo tena.

Mathalani, siku ya Jumatatu nilipata changamoto katika mita yangu ya LUKU, umeme ulikuwa ukisomeka katika mita, lakini nilikuwa sipati huduma ya umeme katika nyumba yangu na ilikuwa hivyo hata kwa baadhi ya majirani zangu. Hivi tatizo liko wapi kwa namba ambazo mmezitambulisha kwa umma nyinyi wenyewe, lakini hazina msaada wowote ule pale zinapitafutwa.

Je! Hili nalo ni jukumu la moja kwa moja kwa waziri mwenye dhamana!?
 
Tafadhari, fundi mkuu Wilaya ya Serengeti, mbadilisheni/ mmhamishe, amefikia hatua ya kubadilisha Taratibu za quotation kama anavyotaka yeye!

Chonde! Chonde! Kwa ufanisi wa TANESCO Wilaya ya Serengeti, mmamlaka husika chunguzeni mtabaini utendaji wake
 
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi tafadhali
Ila tanesco jaman, yaan nimechoka na hili jibu hamjui tu.. imagine hamjali wateja wenu, yaan unareport kila leo lakini hata kupiga simu kuuliza kwa undani hakuna.. aisee.
 
Tafadhari, fundi mkuu Wilaya ya Serengeti, mbadilisheni/ mmhamishe, amefikia hatua ya kubadilisha Taratibu za quotation kama anavyotaka yeye!
Chonde! Chonde! Kwa ufanisi wa TANESCO Wilaya ya Serengeti, mmamlaka husika chunguzeni mtabaini utendaji wake
Amsmamishwe kabisa maana akihamishwa anapeleka tatzo Kwa wengine inakua n kama kupga upepo rangi
 
Amsmamishwe kabisa maana akihamishwa anapeleka tatzo Kwa wengine inakua n kama kupga upepo rangi
Anajiamini kuliko kawaida, gharama za serikali zinaeleweka, Sera ya serikali juu ya kuweka umeme ni umbali wa mita 0 hadi mita 120, na idadi ya nguzo zisizidi 3!

True anataratibu na kanuni nje ya hizi, wanyonge wanapigwa, amejiwekea genge la kupiga hela
 
TANESCO hivi wale waliolipia umeme tokea mwaka Jana mwezi 10,11 kabla ya tarehe 05/01/2022 na mkawatumia ujumbe wa simu kua wateja wetu wote mliolipia umeme kabla ya Tangazo la mh Rais tutawawekea umeme kabla ya tarehe 30/03/2022 na hizo meseji zilitumwa January hivi hilo tangazo lenu bado lipo valid kweli? Maana kesho ndo mwisho wa mwezi March na umeme bado shida nini? Watu wanasubiri umeme kwa zaidi ya miezi 4 kweli? Ni Tanzania tu ambapo unalipia huduma kwa control no alafu unasubiri miezi zaidi ya minne..
nakazia
 
Hii thread ni ya TANESCO kweli? Mimi nina wasiwasi tusije tukawa tunajibiwa na mchunga ng'ombe wa Rukwa porini huko anakula maembe juu ya mti wa mwembe.

Haiwezekani kila siku malalamiko yanatolewa halafu hayashughulikiwi kazi yao kuomba namba TANESCO namba zetu mbona mnachukua halafu hamshughulikii matatizo kwa nini? Kila siku mtu akitoa lalamiko replies zenu ni tunaomba namba
 
TANESCO leo si ndo deadline ya kuwaunganishia umeme wateja waliolipia 27k .....na.mpaka dakika hii hapa kwangu sijaona Yanesco kuja kuniwekea Umeme sijui hawa Tanesco Kibaha wana deadline yao wamejiwekea ?
 
TANESCO leo si ndo deadline ya kuwaunganishia umeme wateja waliolipia 27k .....na.mpaka dakika hii hapa kwangu sijaona Yanesco kuja kuniwekea Umeme sijui hawa Tanesco Kibaha wana deadline yao wamejiwekea ?
Danganya toto hiyo mkuu,hata Mimi kwangu hamna kitu
 
Anajiamini kuliko kawaida, gharama za serikali zinaeleweka, Sera ya serikali juu ya kuweka umeme ni umbali wa mita 0 hadi mita 120, na idadi ya nguzo zisizidi 3! True anataratibu na kanuni nje ya hizi, wanyonge wanapigwa, amejiwekea genge la kupiga hela
Umbali wa 120 si n nguzo mbili??
 
Back
Top Bottom