Mkurugenzi Mkuu TANESCO.
-Ninauliza kama kuna changamoto na mfumo wa Ni-connect,kwa maana mzee wangu alilipia huduma ya (tarehe 29/09/2022 ) kuunganishiwa umeme,eneo la Mwanalugali, Kibaha, Mkoa wa Pwani lakini mpaka leo,ninapoandika ujumbe huu,hakuna mrejesho na huduma haijatolewa .
-Licha ya kitengo cha huduma kwa wateja Makao Makuu, kusema kuwa shirika litachukua hatua za haraka tarehe 04/10/2022.
Maoni
1). Inavyoonekana kuna wateja wengi waliomba huduma kwa mfumo wa Ni-connect, bado hawajapata huduma au labda ni mzee wangu.
2). Inavyoonekana kuna hujuma za watendaji wako wa chini,dhidi yako,au Waziri mwenye dhamana na umeme au wanamuhujumu Rais wetu.
3).Kama mfumo wa Ni-connect una changamoto ,ni vema wateja wakajulishwa,shirika kimetumia fedha nyingi kulipa wachekeshaji kutoa tangazo, au propaganda badala ya kununua vifaa vya kutoa huduma.
4). Mfumo wa Ni-connect uwe unatoa mrejesho (feedback) pindi mteja anapocheleweshewa kupata huduma ndani ya mudae uliowekwa.
Ushauri.
1). Mamlaka husika sijitafakari na watoe huduma kwa weledi,kama nyenzo zipo.
2). Kama kuna uzembe au wafanyakazi wanataka kuhujuma shirika, wajitafakari.
3). Kama shirika limekuwa kubwa,kiasi kwamba inashindikana kuliongoza,ni vema likagawanywa na kuwa na kampuni tanzu tatu (Generation, transmission na distribution)
Sent from my TECNO KC8 using
JamiiForums mobile app