TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO mlisema mnakata umeme kuanzia alfajiri saa 11 hadi saa 5 asubuhi.Sasa saa hizi saa 6 mmekata Kimara.Tushike lipi?
Mida ya kazi hii mnatutia hasara nyinyi watu,kila siku hamuishu sababu.
Sababu zenu hazihalalishi incompetence yenu kwamba tuna shirika ambalo kila mda linashindwa kutoa huduma endelevu kwa wananchi.
Mimi humu nalumbana na nyinyi tangu 2012 na majibu yenu ni haya kwamba mnaboresha miundombinu.
Tangu 2012 tunasubiri miundombinu iboreke,tunazeeka tukisubiri nyinyi,biashara zetu zikiharibika kabisa,kweli?hii ni hoja ya maana?!
Hapa tumekaa tumezima mashine,tunasubiri Tanesco warudishe umeme na ndio trend miaka nenda rudi!msss!
Morogoro Turiani ndio usisema kbs umeme unakatika Karibu Kila siku, hivi wameuchukua asb mpk saa 1 Usk huu haujarudi ,hakuna taarifa Wala chochote ,

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeweka wazi mipango yake ya kumaliza tatizo la umeme kwa asilimia 100 Mkoani Tanga kufikia Machi 2023, huku kukiwa na mikakati ya kuzalisha umeme kwa njia ya jua kufikia mwishoni mwa mwaka huu (2022).

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa amezungumzia jinsi changamoto ya mabadiliko ya Tabia Nchi yanavyochangia changamoto kwa TANESCO, akisema:

“Dunia sasa ina wimbi na changamoto ya mabadiliko ya Tabia Nchi, mmoja wa wahanga wakubwa ni TANESCO. Tafsiri pekee tuliyonayo ni changamoto ya upatikanaji wa maji ambayo tunaitegemea kama sehemu ya uzalishaji umeme.”

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usafirishaji Umeme wa TANESCO, Abubakari Issa ameeleza kuwa Shirika hilo linafanya maboresho ya laini ya umeme kutoka Ubungo kwenda Chalinze kisha Tanga ikiwa ni juhudi za kuboresha upatikanaji wa umeme maeneo hayo.

Issa amesema “Hii laini ina uwezo wa Megawati 75, tunaenda kuifanyia maboresho ya kuiongezea uwezo kuwa na Megawati 150, ambayo ni mara mbili ya kiwango kilichopo sasa, hii kazi itafanyika katika awamu tatu.

“Awamu ya kwanza ya Chalinze kwenda Mlandizi tumeikamilisha, ahadi yangu ni kuwa hadi kufikia Machi 2023 tatizo la umeme litakuwa limemalizika kwa wakazi wa Tanga.”

Akizungumzia ahadi hiyo, Meya wa Jiji la Tanga, Abrahaman Shiloo amesema hatua zinazofanywa zinaonesha kuna mwanga mzuri wa kuondoka kwenye tatizo la kudumu la upungufu wa umeme Nchini.

Upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Martin Mwambene amesema TANESCO imejidhatiti kuhakikisha wana vyanzo mchanganyiko, akigusia mpango wa kuanza kuzalisha umeme kwa njia ya jua maeneo ya Kishapu Mkoani Shinyanga pindi itakapofika Desemba 2022

Habari, nnapata message iyo napojaribu kununua umeme. Nimepiga simu zaid ya mara 20 haipokelewi
Screenshot_20221028-131446_Messages.jpg
 
Untitled Page
  • Habari, nnapata message iyo napojaribu kununua umeme. Nimepiga simu zaid ya mara 20 haipokelewiView attachment 2400376
    Ndugu mteja tafadhali fanya manunuzi ya umeme muda huu, kabla ujaingiza Token zako za umeme kwanza fanya zoezi hili, Ingiza hizi namba za key change kundi la kwanza (2877 3153 6083 5256 9256 Bonyeza OK) Kundi la pili (4320 1659 8340 5655 9936 Bonyeza OK) Baada ya hapo unaingiza token zako za umeme
    TANESCO Huduma Kwa Wateja
    SIMU:0748 550000^IT

    Untitled Page
    Habari, nnapata message iyo napojaribu kununua umeme. Nimepiga simu zaid ya mara 20 haipokelewiView attachment 2400376
 
Hivi iliwahi kutolewa sababu ya kupunguza jitihada za kutumia gas kuzalisha Nishati na kuongeza jitihada za kuzalisha umeme Kwa kutegemea vyanzo vingine?

Hivi Kuna taarifa gani kuhusu vijana waliokuwa wanaajiriwa Kwa mkataba Tanesco na kusaidia kazi kwasasa wapo wapi? Mmewafukuza? au mmebadili utaratibu ili KAZI kubwa ifanywe na wachache Kwa tija ndogo?

Je,huu Wizi unaoendelea wa VIPURI vya Tanesco havihusiani na kuwafukuza hawa waliokuwa watumishi wa Tanesco?

Je,Shirika letu pendwa linataarifa kwamba sasa Wizi wa umeme,Mita na Transfoma umeongezeka?

Badala ya kukaa na kutafuta ufumbuzi wa matatizo mnapanga kuondoa huduma ya matumizi MADOGO Kwa wateja Maskini!

Haya ni mawazo yangu tu yametokea nilipokatiwa umeme ghafla wakati AMBAPO nilikuwa nauhitaji mkubwa na kukosekana Kwa umeme kumenipa hasara kubwa najuta.
 
Habari, pole kwa changamoto unayoweza kuwa uliiptia, tafadhari tupatie taarifa kamili ya kukatiwa kwako umeme, ili tufatilie na kuweza kuifanyia kazi.
 
Naomba kuuliza, hivi inachukua siku au miezi mingapi kuingiziwa umeme yumbani baada ya kufanya malipo tanesco?

Maana nimelipia laki 320 na mia kadhaa toka 24/10/2022 hadi leo kimya, labda leo watakuja sijui na hakuna taarifa yoyote niliyopewa hadi sasa!
 
Mmmh!! Mwezi WA 10 ilikuwa elfu 21 boss mbna unatupiga na kitu kizito me nililipia mwezi WA 12 nikafungiwa mwezi WA Tatu hiyo 320 ulilipia na nguzo au 3phase ??
 
Mmmh!! Mwezi WA 10 ilikuwa elfu 21 boss mbna unatupiga na kitu kizito me nililipia mwezi WA 12 nikafungiwa mwezi WA Tatu hiyo 320 ulilipia na nguzo au 3phase ??
Niliambiwa ndiyo ghalama ya kawaida! Ni ndani ya mita 30 na wala siyo 3phase. Niko ndani ya manispaa na siyo umeme wa REA
 
Mi nipo Shinyanga, barabara iendayo Magereza, Ushirika Chamaguha. Hivi, inakuwaje, karibia kila siku maeneo yetu kukatwa umeme, lakini maeneo mengine hatuoni tatizo hilo? Leo, toka ukatwe jana jioni, umerudishwa leo saa mbili asubuhi. Muda huu, umekatwa tena, hatujui utarudi muda gani!
Hivi, kama ni mgawo, ni maeneo yetu tu? Naomba kufahamishwa ni tatizo gani linalosababisha hivyo!
 
Asante kwa taarifa tumeipokea kwa hatua zaidi
 
Mnapokata umeme bila kufuata ratiba mnaonaga ufahari sana???. Sawa tumewakubalia kuna mgao sasa kufuata ratiba na ratiba iwe wazi ili tujipange mnaona shida gani?
Sijui mkoje
 
  • Thanks
Reactions: ABJ
Mnakata umeme bila taarifa wakati platform zote za habari mnazo tangazeni instagram ratiba ya mgao, twitterna facebook.
Tena kibaya zaidi wanakata baada ya dk3 unarudi wanakata tena yaani Kama wanafanya kamchezo[emoji30]

Jamani Tanesco mtatuunguzia vitu wooi mnakeraa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom