SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MANUNUZI YA LUKU KWA BAADHI YA WATEJA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme wa LUKU siku ya Jumatatu, Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.
Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wanafanya kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa haraka.
Tutaendelea kutoa taarifa kadri huduma itakavyo kuwa ikirejea.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza
Kituo cha miito ya simu makao makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti:
www.tanesco.co.tz
Mitandao ya kijamii
Twitter:
www.twitter.com/tanescoyetu
Facebook
Tanesco Yetu
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Mei 18, 2021.