TANESCO wapata hitilafu katika mfumo wa kununua umeme wa LUKU
Na Kalemani kakaa tu kimya, umeme tangu juzi haununuliki kwenye simu watu wako gizani hakuna chochote kinachoendelea hela zinaliwa ,mtu kanunua umeme mitandao kama minne hela zinaliwa umeme token haziji Tanesco wanafeli sana
Kwenye kuunda baraza la mawaziri mama Ali copy na ku paste. Sasa kinachotokea avumilie ndio majibu yake
 
Wazitoe wapi nguvu??, Ha ha ah yawezekana tu mmoja kakata waya.
Baadaye utawasikia STIGLERS wakati Stigler haina uhusiano na Luku!

Everyday is Saturday............................... 😎
Sasa inakuwaje?

Maana kila kona kikitokea kitu naona wanasingiziwa sukuma gang

Basi watakuwa wameshika nchi nzima
 
Hivi nikienda ofisi ya tanesco iliyokaribu yangu hawawezi kweli kuniwekea umeme/kunipa token?
Huko kite tumeenda hakuna huduma, naomba kama kuna mtu ana namba ya mh. Waziri mkuu anitumie!
 
Nilipo unakatika kila siku saa sita usiku na kurudi saa moja asubuhi.

Na mmoja yupo juu hapo labda nikuitie umuulize.

IMG20210519134413.jpg
 
Eti uchumi wa Kati.
Umeme Leo siku ya tatu tuko gizani. Biashara zimekwama.
Tanesco wamesema ukitaka umeme uende makao makuu ya wilaya au mkoa. Wilaya nyingine Hadi ufike wilayani Ni safari ya siku nzima au wilaya za Dar zinahudumia wateja lukuki kiasi kwamba Bora kununua ka jenereta kuliko kwenda kukutana na hiyo foleni ya wanunua umeme.
Kama siyo system ya Muhimbili Basi Ni TRA au TPA.
Kuna wanaosema eti na tiketi za Basi tukate kielectroniki, are they serious? TRA tu ambapo Ni sehemu ya kukusanya pesa za kuendesha nchi system zinakua down.
KAMA HAYA MAMBO YA KIELECTRONIK yametushinda Basi turudi kule kule 1961.
Kuna umuhimu wa kuondoa baadhi ya wahuni wanaosimamia hizi taasisi.
 
Habari wadau!

Tanesco nimeamua kuwaita mara tatu kama wapo na wanapita humu JF wasome hizi comment za wananzengo maana naona kama wanaturudisha enzi za zama za mawe.

Umeme siku hizi umekuwa unakatika mara kwa mara pasipo kupewa taarifa rasmi zamani mlikuwa mnapita mpaka na magari mnatutangazia lakini sasa mnakata tu yaani kila ukiamka unakuta washakata.

Ukirudi ukijaribu kununua they are not reachable yaani hauwezi nunua kabisa Luku.

Daah hii sio fare kwa kweli, tukionge tunaonekana waropokaji.
JamiiForums2114352714.jpg
 
yaani nchi nzima haina umeme ila mama anakenua kenu tu ikulu..
fukuza wajinga wote mamluki wa Meko.wanafanya makusudi...yaani humu mama watamzamisha kwenye tope ngoja aendelee kuwachekea tu
Hivi kipindi cha mgao awamu ya nne nani alikuwa anahujumiwa? Au humu JF tumekubaliana kila tatizo tuelekeze kwa hayati?
 
Back
Top Bottom