Tanga ilitakiwa uwe mkoa wa pili kwa uchumi baada ya Dar Es Salaam

Kiografia yake ndio tatizo kubwa sana .Mbeya na Mwanza ni majiji huru tena kikanda zao ila angalia Tanga sasa bandari inanyonywa na Dar huku fursa za shughuli za kiserkali zinapelekwa Arusha ...
Tatizo tanga mjini nayo imejificha ndani ndani sana, Bandari ya Tanga sasa hivi inafanya vizuri, bomba la mafuta ya uganda linapitia hapo, viwanda vya mikonge vimeanza kufanya kazi, reli inafanya kazi, tanga itanyanyuka
 
Tatizo tanga mjini nayo imejificha ndani ndani sana, Bandari ya Tanga sasa hivi inafanya vizuri, bomba la mafuta ya uganda linapitia hapo, viwanda vya mikonge vimeanza kufanya kazi, reli inafanya kazi, tanga itanyanyuka
Umeona eeh!! Tanga mjini niliongea na jamaa yangu ni baharia anasema imejificha sana 😅,ukiangalia kwa ukanda ule inaonekana sana Mombasa zaidi na Lamu, kipind fulani walisema bandari iko sehemu mbaya ifanye kuhamishiwa kule ''Ndumi'' au beach kwa bibi.
.

Kiufupi inahitaji promo ya hali ya juu ; mfano watalii wengi wanashukia Dar Dar,Mafia na kilwa ila pale sio rahisi kusikia watalii wameshuka.​
 

Msijitoe ufaham mpepewa trillion 3.1 na mama hizo si ni hela?
 
Vijana wa huko wavivu, wanajua kuoa tu na kushinda vijiweni ! Kijana akimiliki kakibanda ka kuingiza nyimbo kwenye simu anaongeza mke wa pili,,,, hayo maendeleo watayapata saa ngapi ? Wamejifelisha wenyewe
 
Uko sahihi,watanzania hudhani ili uonekane mchapakazi lazima ufie shambani.
Matajiri wakubwa wa dunia wanajihusisha na technology kuliko kilimo.
Dunia imebadilika
 
Mkoa umebarikiwa kila kitu
Sijui wagosi wanafeli wapi
uvivu, uchawi, uzinzi, ulawiti, n.k, mtu wa tanga akinunua baiskeli huwa anaona ameshafanikiwa, kumkuta baba mtu mzima na wake wawili ila ana mgahawa mdogo sana anaouza tu chapati na vitafunwa asubuhi na jioni, mchana kutwa kalala au anacheza bao, ni kawaida. Pia, hata serikali haijaona fursa, tanga kuna bandari/eneo la bandari inayoweza kulisha sio tu dsm bali kenya, uganda na rwanda na mikoa ya huko. reli toka dsm hadi tanga ipo ya mjerumani, ni kufukua tu na kutandaza mpya ya sgr ili watu wanywe chai tanga na lunch DSM lakini wapi serikali inasubiri mzungu atoe msaada. connecting sgr from dsm to Tanga manake umekonect na MOmbasa pia na kilimanjaro na arusha. Uvuvi, hivyo viboti vimenunuliwa na samia juzi, wanatakiwa kununua boti nyingi na kubwa na kuwapa hao wavuvi kwenye vikundi wavue samaki nyingi wauze wapate pesa mzunguko wa pesa uwepo, kwa wasiojua, bei ya pweza kilo moja hapa bongo ni sawa tu na bei ya pweza kwenye nchi nyingi tu za ulaya na asia, kwa sababu kumvua ni ngumu hadi uzamie, pia samaki tunakula tu dagaa hapa, ukienda pale feri unawaona wanaouza visamaki vichache ambavyo amekesha usiku mzima unawaonea huruma. serikali imewatupa.
 
Nyie mnaoisakama Tanga vijijini kwenu wanalalia ngozi za mbuzi kwa vile mumejua kutumia smartphone basi mnaandika upumbavu tu
 
Nyie mnaoisakama Tanga vijijini kwenu wanalalia ngozi za mbuzi kwa vile mumejua kutumia smartphone basi mnaandika upumbavu tu
sasa watu kama wewe, wanaoridhika wakati wapo kwenye hali duni ndio mnaimaliza tanga. hiyo mentality hadi ukoo wenu mzima utakuta mpo hivyo.
 
Naona bado hujafika kwenye level ya kuelewa watu wa Pwani. Watu wa Pwani wanajua kuwa maisha haya ni ya kupita, na yanapaswa kufurahiwa.

Hawa ni watu ambao wanafurahia kile kidogo walicho nacho badala ya kuishi kwa hofu ya kutokupata kingine. Hawakushikwa na ugonjwa wa ubepari unaowafanya wengine muishi maisha ya wivu, mashindano, na stress zisizo na kichwa wala miguu. Kama Wamasai wanavyopenda ng’ombe wao na kuona utajiri wao kwenye mifugo, watu wa Pwani wanapima mafanikio kwa amani ya moyo, furaha, na mahusiano na watu wanaowapenda.


Na jambo moja la ajabu ni kwamba, watu wa Pwani si wachoyo. Hawana hofu ya kuona mgeni anafanikiwa. Mgeni akija, akafanya biashara, akawa tajiri, watu wa Pwani hawana shida. Hawaishi maisha ya wivu na roho mbaya kama jamii nyingine zinazokaa macho usiku zikiwaza mwenzangu ana nini ambacho mimi sina. Wao wanaishi na msimamo wa mali si kitu, cha muhimu ni maisha yenyewe.

Kwa hiyo, kama huelewi mtazamo huu, utaendelea kufikiria kwamba watu wa Pwani ni wavivu, kumbe ukweli ni kwamba wao wana maisha mazuri kuliko wewe. Hawaishi kwa stress, hawaishi kwa mashindano, wana furaha, na wanajua kuwa mwisho wa yote, maisha haya ni mafupi sana kupoteza muda kwenye presha zisizo na maana.
 
Mkuu umetema madini adimu sana. Hapa watabisha watumwa wa mzungu tu maana wako radhi wauze bia feki ili waonekane nao ni watu kwa mawazo yao
 
Mkuu umetema madini adimu sana. Hapa watabisha watumwa wa mzungu tu maana wako radhi wauze bia feki ili waonekane nao ni watu kwa mawazo yao
hii mentality yenu mbaya sana. sasa ukimiliki baiskeli ukaridhika, una wake wanne na watoto rundo, utasomeshea nini? si ndio maana tunasema kuna cycle ya umasikini kwa sababu ninyi na familia zenu zote na ukoo mzima mna mentality kama hii, what do you expect Tanga iwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…