Tangu Rais Dkt. Magufuli afariki, hakuna Habari za vifo vya Corona


kwahiyo watu hawafi wanasubiri mama alekee kwenye sayansi[emoji16][emoji16][emoji16].

nyie watu hata nguruwe wanawazidi utashi.
 
Kwa bandiko lako hili unamtuhumu mwendazake zake kuwa ana mkono na vifo vilivyokuwa vinatokea wakati wa uhai wake. Shauri yako, hizi ni tuhuma nzito sana
usinilishe maneno mkuu

nimemtuhumu wapi?
thibitisha
 
mkuu kuna watu wanapiga propaganda tu
Tanzania tunaishi salama zaidi tunatishwa tu
 
Wewe acha tu,Magufuli wamemuua kabisa,ila Mungu ni mwema
 
Siku nilipoona Kikwete kavaa Barakoa na wale mapadri,Magu mwenyewe alitepeta sana,Mungu ailinde familia ya Magu
 
Hatuna haja ya kupiga kelele,Raisi aliyepo anakubali Covid ipo,na watu wachukue hatua,hakuna ushenzi ule wa kuwalazimisha watu wavue Barakoa,Wala hakuna dhihaka dhidi yao,na Raisi ameahidi kuunda tume kucheki madhara ya Covid,hatuna haja ya kupiga kelele Tena.
Sasa hv tupo huru kusema mgonjwa kafa kwa corona.
Jiwe hakutaka tuseme kitu,ukisema kuna covid,unaambiwa mchochezi.
 
Hakuna jambo jipya humu duniani yote unayoyaona sasa yalikwisha tokea huko zamani, Kama sayansi biblia inabainisha. Kusudi la tukio likisha pita linalofuata kusudi jingine jipya lililo pangwa. Utaelewa kidogo kidogo baadaye
 
Siku nilipoona Kikwete kavaa Barakoa na wale mapadri,Magu mwenyewe alitepeta sana,Mungu ailinde familia ya Magu
Ule mwezi wa pili huenda ulimpa Magufuli stress sana maana alishuhudia watu wakikataa style yake ya uongozi wa nchi waziwazi. Wakatoliki walimgomea waziwazi, nahisi pale ndipo alipojua kuwa uraisi wake una mipaka
 
A third wave is coming Next Year,miezi ya January kuelekea March.
Its gonna strike again.
 
Tanzia zimepotea sana saizi humu jukwaani.......nadhani vifo viliisha baada ya jeipiemu kuondoka......anywei nchi hii ngumu sana

Sababu kubwa ni wale ambao hawakujikinga kipindi cha mwendazake walianza kujikinga aliopoondoka. Wengi waliamini korona ipo lakini wasingeweza kujikinga kwa sababu walipenda kuonekana hawampingi mwendazake.

Vifo bado vipo sana na mama yangu ni mmoja waliokufa hata baada ya mwendazake kuiacha dunia hii. Korona ipo, tujilinde!!
 
Mleta mada, umeshasikia kiongozi yeyote akisema “Tanzania hakuna korona” toka JPM aiache dunia hii?? Umesikia tena habari za nyungu japo wapigadebe wa nyungu bado wangali na sisi katika uongozi??

Sababu ni hii - watanzania wengi wamekubali korona ipo na wanajaribu kukabiliana nayo. Waliopiga kelele kipindi cha mwendazake walitaka tukiri ipo na hata SSH na Mwinyi wameshakiri ipo na twende pamoja na dunia!!

Kilichokuwa kikitafutwa kimeshapatikana - kukiri tuna tatizo. Tusubiri Taskforce ya SSH ituleteee ushauri wa kitaalamu.
 
Hata misururu ya malori tukiambiwa yamebeba maiti kwenda kuzika na kupigwa picha yamejipanga eti yote hayo yamebeba miili kuelekea mikoa fulani kwa changamoto ya upumuaji hakuna, Tz tunataka kucopy siasa mbaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…