Tanzania imefeli vibaya kwenye vituo vya reli ya kisasa(SGR)

Tanzania imefeli vibaya kwenye vituo vya reli ya kisasa(SGR)

Haaaa eti kibarua muulize Masanja kadogosa, au Mr. Mgezi au MR Katalaya watakuambia mimi ni nani
Ndugu jitahidi tu kuwa mvumilivu maana wanalumumba hawawezi kukubaliana nawe kwani unakosowa mradi wa malaika mkuu
 
Hilo nakubaliana na wewe 100%.

Angalia tu station za mabasi za hivi karibuni zinavyojengwa ni upuuzi mtupu.
Jamaa nimemuelewa, mi ni mpenzi wa documentaries na fani yangu ni logistics & transportation , vituo vya usafiri vinaplay role kwenye kuvutia abiria, eg Dubai airport ni nzuri sana wale si wajinga kuinvest vile, angalieni tu pale ferry terminal ya Azam pako vizuri, abiria anaanza kutathmini mode of transport toka anapokelewa na mkata ticket hadi kwenye onboard products ,huko duniani vituo vya reli na mabasi ni vizuri utafikiri uko airport. Kuna kiazi mmoja anasema sie shida yetu ni train tu stations zikiwa hovyo poa tu, hebu tuwe tunakubali constructive I dia .Nchi nzima bus terminal nzuri Msamvu tu shame on us.
 
Nyinyi ndio watumishi ambao hamjui maadilli ya kazi(Work Ethics),unajiitaje Engineer katika mradi halafu unalalamika kuhusu poor designing,wewe kama Engineer Mtanzania mzalendo si ndio ilibidi ukosoe kwenye vikao vyenu vya ndani ili hilo tatizo litatuliwe,sasa kama wewe ambae ni Engineer ambaye ndio unafanya nao kazi na upo ndani umeshindwa kutatua tatizo,unadhani hawa Jf wataweza?ni mda muafaka wataalamu wetu wa kitanzania muache unafiki na siasa kwenye mambo ya kitaalamu mtangulize uzalendo na mfanye kazi,kwa maslai ya sisi wanachi ambao ndio walipa kodi wakubwa.
Kasome tena, amesema walitaka fukuzwa kuleta huku maana yake anataka wenye mradi wenu(wananchi- sio bwana yule)mpige kelele
 
Huko kazini kwako hakuna vikao? Kwanini usilizungumze kwenye vikao vyenu? Ukituambia sisi tuna nguvu gani ya kubadili mambo yaliyopo kwenye ngazi ya utekelezaji? Ni nani amekutuma kuja kulalamika kwetu? Kama ninyi kwa ninyi mmekosa kuongea lugha moja huko ndani, je sisi wa nje tutaielewa lugha iliyowashinda ninyi wa ndani?
Wewe utakuwa umesoma comments za watu ila uzi hukusoma.
 
Wakuu pole na mihangaiko ya kila siku. Nchi yetu inajenga reli ya kisasa Kwa mabilioni ya dola($3.2b) kutoka Dar kwenda maktupora.

Nashukuru mimi ninausika na ujenzi huu nkiwa kama mhandisi wa Yapi Merkez wanaojenga hio reli.

Reli hii Kwa kweli itakuwa moto wa kuotea mbali, kuanzia speed yake, aina ya treni itakayo tumika, na uwezo wa kubeba mzigo, yaani hapa SGR itakuwa vizuri sana.

Kituko kinakuja kwenye station za reli, yaani aliyefanya design aliambiwa adi-sign kulingana na vitu vya Tanzania yaani station zi-reflect Tanzania. Basi station moja itafanana na umbo la Madini ya Tanzanite, nyingine itakuwa na umbo la kiremba cha mwanamke, nyingine sjui vinini yaani ujinga tu, kibaya zaidi station ni ndogo saaaana, tena sana.

Kwa hili TZ tumepigwa gape na wa Kenya wana station za kisasa na kubwa sio kama zetu.

N. B. Tulipojitahidi kuzikosoa wakatishia kutufukuza kazi,
Watanzania station za SGR ni upupu mtupu.

Engineer,
Rukuku boy
Sasa wewe unataka SOGA ,Ngerenger wajenge station kubwa? kama VOI au Mariakani kama Kenya? Kenya reli inapita kwenye Miji.Sisi ukitoka Dar mji mkubwa ni Morogoro.Ndio maana Dar na Moro ni kubwa.Hata reli ya Tazara Stesheni kubwa ni Dar na Mbeya.Ukiangalia za mlimba,ifakara,Makambako ni stesheni ndogo kama hizo za Pugu,Soga,na Ngerengere.Sioni kama kuna ubaya.Umuhimu ni kufika mapema zikianza kufanya kazi.
 
Mnapinga ila ukweli ndo huo Yapi Merkez kwenye station hayupo vizuri angalia alichowafanyia ethiopia hadi humuhumu watu waliziponda station za Ethiopia ila wewe uliyesoma political science unajifanya unajua
Empty set
Mbona ya Kombolcha huko Ethiopia ni kubwa.
 
Mnapinga ila ukweli ndo huo Yapi Merkez kwenye station hayupo vizuri angalia alichowafanyia ethiopia hadi humuhumu watu waliziponda station za Ethiopia ila wewe uliyesoma political science unajifanya unajua
Empty set
Kiongozi ungetuwekea picha basi tuone maana wewe si upo jikoni huko haa haa,ili tulinganishe na za jirani
 
Haaaaaaaaaaaaa unaumwa wewe mungu ananiona me sio dereva, na ukimsingizia huyo jamaa wakamfukuza kazi hakika utakuwa umechuma zambi ya bure me sio dereva na haitatokea
We engineer huna gari? Eti haitotokea. Kuwa dereva sio lazima uajiliwe hyo kazi, hata waheshimiwa wanaendeshwa lakini na wao wanajua.
 
mbona station ya dar ni kubwa tu. tena itakuwa na shopping malls, station ni sehemu ya kushuka na kupanda abiria kama hamna movement kubwa ya watu huna haja ya kuremba unajiingiza hasara, pili mahitaji yakiongezeka zitajengwa na kupanuliwa, nenda uingereza station kubwa utazikuta london, birmingham, manchester na miji mingine mikubwa ila station za njiani za kawaida sana
Hzo station ulizotaja unajua zimejengwa miaka gani? hadi leo bado nzuri ,wasije wakatujengea kama magorofa ya NIC na Tanesco kule posta (just kidding)
 
Hzo station ulizotaja unajua zimejengwa miaka gani? hadi leo bado nzuri ,wasije wakatujengea kama magorofa ya NIC na Tanesco kule posta (just kidding)
Angalia watu walivyoponda vituo baada ya Ben mwanantala kuweka video ulnionesha hivyo vituo
Screenshot_20181201-101236.jpeg
Screenshot_20181201-101215.jpeg
 
Mtoa post unazingua " sasa hapo kilichokukera nini " hao ma engineer ku design vituo vyenye muonekano wa maliasili zetu na tamaduni ya mavazi ya kiafrica au ni nini !!? Wewe ulitaka wa _design katika muonekano wa nchi za kimagharibi sindio ".... Mimi nimependa hiyo idea yao " maana hayo majengo yatakuwa yana tukumbusha umuhimu wa kuthamini vya kwetu na kutuasa tuache kutukuza tamaduni za watu "..... wape kongole viongozi wote walio pendekeza hilo "..... !!
Cheki watu wameviona kwenye video ya reli TV watu wamevikosoa
Screenshot_20181201-101236.jpeg
Screenshot_20181201-101215.jpeg
 
Back
Top Bottom