Lengo ni zuri kwa nini TPA wasijitanue kwa kuwekeza kwenye maeneo ya bandari kavu sababu uwezo huo wanao kuwapa Private sector ni kuongeza wigo mpana wa upigaji na biashara za magendo kwa maslahi ya wachache.
Magendo kivipi?
 
 
 
Wacha waje waendeshe wenye hakili timamu

Siyo wake washenzi una nunua gari ya mil 100 af eti ushuru mil 150

Huu SI uchizi huu Bora ibinafsishwe
 
Kama hili limetushinda, kipi tunaweza?
 
Hao wanaokuja wanaletwa na watanzania, usitegemee hizo hujuma na wizi kuisha. Tulishabinafsisha mashirika mengi Ila ndio yakafa zaidi
 
Wacha waje waendeshe wenye hakili timamu

Siyo wake washenzi una nunua gari ya mil 100 af eti ushuru mil 150

Huu SI uchizi huu Bora ibinafsishwe
Hakili ×
Akili ✓

Muendeshaji mpya wa bandari anahusiana vipi na bei ya magari? Kodi na Ushuru wa gari ni TRA
 
Kama mmeshindwa endesha bora wanaoweza waje.
Mombasa, London, Germany wote waendeshaji si wazawa
Kama kila mahali pakishindwa kuendeshwa wanapewa wageni tutafanyika watumwa katika nchi yetu. Wajerumani na Waingereza wanaendesha bandari zao wenyewe.
 
Profesa Makame Mbarawa Kwenu ni Zanzibar Kwanini hukuanza kubinafsisha bandari ya Zanzibar?
 
Uzalendo au ushamba,tena binafsi naombea sana baada ya bandari wageukie kwenye mwendokasi,wabongo wana kazi ya kuiba tu,magari wamepewa,ya kwao peke yao lkn wanalalamika hasara kila siku,mwendokasi akipewa mtu wa kueleweka kama bandari,bus zote zitakya full kiyoyozi,abiria awatolundikwa kama ilivyo sasa na bus zitafika vituoni kwa wakati,yan unajua kabisa saa 4:00 bus la kivukoni litakuwepo shekilango,sasa vurugu,wabongo hatuwezi kujisimamia na bado tunaendesha maisha ya karne ya 19 while tuko karne ya 21,ngoja watu waje kutufunza ili vizazi vyetu vijavyo vipate kujifunza
 
Naomba niende nje ya mada ya bandari nitoe maoni yangu kwenye kuchapa kazi. Kwa uzoefu wangu nakubaliana na wewe kuwa watanzania hasa wafanyakazi wa serikali kwa asilimia kubwa hawajitumi, hawaendi na muda hata kidogo, wezi balaaa, wachache wanaojituma wanapigwa majungu aisee, mabosi wanapenda kunyenyekewa sana, rushwa na kujuana kwingi. Wiki iliyopita nimeenda ofisi ya serikali kupatiwa huduma yaani bosi mkubwa tu lakini anaongea na simu mambo ya michepuko na michango ya harusi alafu nje foleni ya wataka huduma ni ndefu kinoma nikajituka nashangaa tu. Kuna sehemu serikali imeleta mradi wenye fedha nyingi sana lakini nasikia watu wanaongea habari ya kupiga hizo hela. Nchi hii asilimia kubwa ni wezi tena majizi wa muda, fedha, vifaa vya ofisi, watu wa majungu, kelele na story za wikiend kwenye ofisi za serikali ni jambo la kawaida kwao. Ofisi niliyopo serikali imeleta laptops mpya na machines zingine mpya, sasa laptops za zamani na vifaa vingine vya zamani vimewekwa ofisini kwangu stoo, ndugu ofisi inawindwa balaaa watu wanataka kusepa na vifaa vya zamani.
 
Tatizo ni usimamizi na mfumo mbovu wa ajira. Ilitakiwa kuwe na usimamizi madhubuti pamoja na wepesi wa kuwatimua wazembe na wasio na tija katika ofisi za serikali bila mlolongo mrefu wa taratibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…