Yaani Dubai waje kuendeleza bandari Tanzania??

Huu ni ulemavu wa aina Gani lakini??

Hawa wasomi wanaomaliza vyuo kila siku wanafanya nini na elimu zao??

Mbona huko ulaya hawatuiti tukaendeleze za kwao??

- Kufanya wenyewe sio Nia na sio Sera ya CCM tangu awamu ya kwanza ilipoisha.

- Kufanyiwa ndio Nia halisi na Sera mama ya CCM. Yanayoendelea ni matokeo ya hili.

Bahati mbaya sana sijaona/kusikia chama cha siasa chenye Nia na Sera ya Kumuinua na kumuamini huyu Mtaganyika, kuwa na yeye ni Bin-Adam, na anaweza kufanya ambavyo Bin-adam wengine wanajifanyia.
 
Tatizo ni usimamizi na mfumo mbovu wa ajira. Ilitakiwa kuwe na usimamizi madhubuti pamoja na wepesi wa kuwatimua wazembe na wasio na tija katika ofisi za serikali bila mlolongo mrefu wa taratibu.
katika hilo tunazembea sana ...Kwa vile ni taasisi za serikali mtu anajua hawezi kufukuzwa kazi kabisa.
 
Upuuzi kama huu mnatoa mifano nje... Mkiambiwa huko nje bei ya mafuta, vocha na vyakula mnasema tuacheni na Tanzania yetu
 
Kama kila mahali pakishindwa kuendeshwa wanapewa wageni tutafanyika watumwa katika nchi yetu. Wajerumani na Waingereza wanaendesha bandari zao wenyewe.
Si Kweli Bandari nyingi anaendesha DP world kwenye Hizo Nchi.


England anaendesha London port, Southampton na london park, ireland Galway port Jumla 4 kwa Uingereza.

Ujerumani pia wanazo 3 ikiwemo Stutgart.

Wapo pia US, Canada hadi bandari yako pendwa Odesa ni wao wanasimamia.

Na DP world kazi yao ni kufanya hizo logistics, sehemu kama Dubai imekua kwa Ajili ya Bandari.

Pitia huu Uzi.

Achana na Bandari ya Mombasa na Dar, Angalia hao Djibouti,

Djibout ni nchi mbovu, ilikua na Vita, ni Jangwa, hakulimiki, kifupi ni ka Nchi kalikua ovyo ovyo sana na ka kimasikini. Wame improve Bandari tu na imewatoa kiuchumi, na vitu wanavyotoa bandarini si vyao ni vya nchi jirani kama Ethiopia. Sasa hivi Djibout uchumi wa mtu mmoja mmoja ni zaidi ya Dola elfu 3 aka mara 3 ya Tanzania. Uchumi wa bandari yao ni zaidi ya nusu ya pato la taifa lao.

Kwa Location yetu Tanzania kama Efficiency inaongezeka hapo Bandarini huyo Djibout tunamuacha mbali tu, Congo tu Hapo wana mimali kibao wanaleta na kutuma, Tuna Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda etc.

Assume kama wanaweza kweli kuongeza Pato toka Trilioni 7 mpaka 23, Huoni ni kiwango kikubwa sana? Trilioni 23+Tra tayari Nchi inajitegemea na haihitaji msaada wa Mtu.
 
Samia anauza nchi wajinga wanafurahia,

Samia anarudisha usultan Tanganyika kwa nguvu zote.

Samia ni wakuogopwa kama ukoma.

Tiss fanyeni jambo,damu za watanzia ziko juu yenu.

Vizazi vijavyo vitapiga bakora makaburi yenu kwa kutokuwajibika.
 
CHADEMA ACHENI UPOTOSHAJI, HUU NDIO UKWELI JUU YA MKATABA WA DP WORLD NA TANZANIA.

✅UFIPA kama kawaida yao, wazee wa kuongea urongo kwa maslahi yao ya kisiasa, kujaza watu hofu na taharuki pasi na msingi, tumewashawazoea na hakuna cha ajabu wanachoweza kufanya tena. Hii ni ishara tosha kwamba hawana hoja walichobakisha ni vioja tu, wapuuzwe.

✅Mkataba huu kati ya DP World na TPA kwa niaba ya Serikali ya JMT chini ya Rais Samia Suluhu una faida gani kwetu, kwanini mkataba huu ni muhimu sana wakati huu kuliko wakati wowote ule?

✅Kwanza, achana kabisa na propaganda za UFIPA juu ya kwamba tumetoa bandari yetu 100% iendeshwe na DP World, huu ni uwongo na wala huitaji degree wala elimu ya darasa la 7 kujua kuwa huu ni uwongo.

✅Hadi muda huu tunachojua ni kwamba, makubaliano ya awali yamesainiwa Dubai wakati Rais Samia Suluhu alipokwenda kwenye maonesho ya Dubai Expo 2020, na kama makubaliano ya mwisho yatasainiwa, basi mkataba huu utakuwa na thamani ya USD 500 milioni.

Nini Mtanzania unapaswa kujua kuhusu mkataba huu?

Kwanza, unatakiwa kujua kwamba DP World itapewa
kushughulikia gati ya 5 hadi 7.

DP World mbinu yake ni kuondoa vizuizi vya biashara na kuunda mfumo ikolojia wa biashara ili kupanua mtiririko wa biashara ya kikanda na kimataifa.

▶️Kama mkataba huu utasainiwa, ndani ya miaka 10 ijayo, ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam utaongezeka kwa asilimia 233.7%

▶️Mapato ya Bandari ya Dar es Salaam kuongezeka kutoka Trilioni 7.79 kwa mwaka hadi Trilioni 26, ndani ya miaka 10 ijayo.

▶️Ufanisi wa Bandari utaongezeka, mizogo itatoa haraka, ajira zitazalishwa kwa wingi na pia pato la taifa kuimarika maradufu.

▶️Mapato yakiongezeka kwenye kupitia Bandari ya Dar, serikali itapunguza mzigo wa kodi kwa Watanzania hivyo kuboresha hali ya maisha ya watu.

▶️DP World hawatowekeza bandari ya Dat tu, bali na bandari nyingine nchini na pia, wataalamu wetu watakwenda kupewa mafunzo na kuongezewa ubunifu kwenye utendaji wao.

🚨Angalizo, Kuna uzushi na uwongo mwingi sana unaendelea kutoka kwa watu ambao kimsingi hawana nia njema ya taifa letu na maendeleo yetu. Kikubwa, watanzania tusome tuache kupotoshwa.
6:52 PM · Jun 6, 2023
from Dar es Salaam, Tanzania·
 

Attachments

  • 20230606_185651.jpg
    100.7 KB · Views: 3
Wacha waje waendeshe wenye hakili timamu

Siyo wake washenzi una nunua gari ya mil 100 af eti ushuru mil 150

Huu SI uchizi huu Bora ibinafsishwe
Ikibinafsiswah kwani ushuru ndo utapimgua hujui kuww kodi ni swala la TRA
 
Acha kupamba,hakuna taifa litafaidika,hapo mbeleni ni makashifa tu,hii nchi kila kitu haiwezi


Hasara za kubinafsisha maeneo nyeti siku mwekezaji akileta nyodo tumekwisha
Kiko wapi kwenye mitandao ya simu,wanatupandishia bando wanavyojisikia na hakuna mtetezi.

Wewe endelea kutumika tu
 
Hao wanajulikana ni kikundi fulani cha kudandia matukio na kuyafanya ajenda mbaya baada ya muda ccm huleta mpya!
 
Unaweza kuhisi hii nchi imelaaniwa,kumbe tatizo ni kukosekana kwa watu wanaofikiri sawasawa.

Hivi kweli hayo yote uliyoeleza hapo sisi kama taifa pamoja na mamlaka ya bandari tumeshindwa kuyatekeleza? Na unaeleza kabisa kana kwamba ni sifa na unaona ni ufahari.

Kwa sababu ya uzembe na uongozi wa kupeana peana huu wa mpe huyu ni mtoto wa yule, kuna siku hii nchi watakodishwa watu kutoka nje waje watutawale.

Tunajitukana, tumekuwa kama wendawazimu!
 
Safari ya kwenda Uingereza na Marekani uliyoipigia debe humu JF kwamba tukimchagua GWAJIMA tutaenda imefikia wapi??maana ulikuwa na mihemko humu lakini mwaka wa Tatu huu kimyaaaa!!!hakika akili zako Bwana JUMA JUMA zipo makalioni
 
Nimesoma lkn sjaona umejibu hoja za hao unaowaita waongo,, mda wa mkataba,, pia tutanufaikaje,, umetaja tu matrilion sasa sisi tunanufaikaje vp kama hayo matrilion yote wanachukua DP World
 
Yani kwa hiki ulichoandika ndio wapewe kwa 100yrs?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…