Tanzania: Kanisa Katoliki kufanya ‘sala maalum’ kuombea uwepo wa Haki na Amani katika nchini

Enzi za Magufuli kulikua na Haki na amani sana hawakuona hata umuhimu wa kuombea taifa
 
Kupitia waraka huu wa kanisa katoliki ni dhahir shahir kuwa, kanisa linatambua kuwepo kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2025.

Je hii ina itamaanisha nini kwenye kampeni ya " No Reform No Election" ?

NRNE Movement itaathiriwa kwa kiwango gani na waraka huu wa kanisa katoliki?
=============
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa taarifa ya wito wa kufanyika kwa Sala na mfungo wa kuombea Haki na Amani nchini Agosti 23, 2025 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025

Taarifa ya leo Juni 20, 2025 iliyotolewa na Baraza hilo imesema kuwa kila Jimbo, Parokia, Jumuiya za Kitawa na Taasisi wataweka utaratibu utakaowawezesha kusali na kutubu kwa masaa 12 au 24 kulingana na uwezo wa Mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…