Tanzania: Kanisa Katoliki kufanya ‘sala maalum’ kuombea uwepo wa Haki na Amani katika nchini

Tanzania: Kanisa Katoliki kufanya ‘sala maalum’ kuombea uwepo wa Haki na Amani katika nchini

AMANI na UTULIVU waombewe viongozi!
Waache kutesa, kuteka, kuuwa, wizi, ufisadi, kuuza maliasili na rasilimali, kuwa wabinafsi!
 
Enzi za Magufuli kulikua na Haki na amani sana hawakuona hata umuhimu wa kuombea taifa
We Kila siku ukiona comment humu inahusu mwenendo wa haki na amani nchini lazima comment yako ianze na "Enzi za Magufuli"
Do you have personal issues with the deceased??au ndo mnashabikia siasa kama vilabu vya mpira!
 
Shetani kishajulikana, Maombi ya nini tena?
Wanahalalisha move ya kijasusi Ili ije ionekane Mungu kajibu maombi!!

Wewe hujajua namna kanisa linavyotumika kuhalalisha operation!!?

Subiri uone baada ya maombi au baada ya hiyo tarehe nini kitajiri!!
 
Katoliki ndio wanaanza leo aisee sisi kila siku huwa tunaomba sala kama ilivyoagizwa na Mtume Paulo kwa Timotheo kwenye Biblia kama jambo la kwanza kwenye sala

1 Timotheo 2: 1-2 inasema

"Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli."

Kwa hiyo hao katoliki kuomba hiyo sala hadi watenge siku maalumu na kupiga tarumbeta kuwa kutakuwa na hiyo sala

Aiseeee .Biblia wanasoma au hawasomi? Eti sala maalumu.Hiyo inatakiwa kuwa sala ya kwanza.Sisi wengine kila siku tunaomba na kabla ya sala yeyote huomba hiyo

Mtume Paulo wanamuelewa au hawamuelewi? Aibu kuitisha kuwa itakuwa sala maalumu
 
Sasa wewe unawapangia kama nani?
 
Sasa wewe unawapangia kama nani?
Ruksa siwapangii nawakumbusha hiyo sala ya amani inatakiwa kuwa ya kwanza kila siku au kabla ya sala yeyote kama mtume Paulo alivyoagiza sio ooh unasema leo ndio nitafanya ni upofu wa Biblia wawe wanasoma Biblia kabla kutoa hizo nyaraka zao
 
Ni kupoteza muda! Watu walishaomba na kuomba na kuomba lakini hakuna matokeo! Hapo ni sawa na kuomba chupa iondoke mezani bila kuchukua hatua ya kwenda kuiondoa kwa mikono yako.
Ukingoja kuwa Malaika watashuka kuleta haki na amani bila kuipigania tutangoja miaka na miongo na miongo!
 
Taarifa ya leo Juni 20, 2025 iliyotolewa na Baraza hilo imesema kuwa kila Jimbo, Parokia, Jumuiya za Kitawa na Taasisi wataweka utaratibu utakaowawezesha kusali na kutubu kwa masaa 12 au 24 kulingana na uwezo wa Mazingira.
Kuna mambo mawili unatakiwa uyazingatie:
1. "NORNE" haikatazi kuwepo uchaguzi wa HAKI.

2. "waralka", unahimiza HAKI na AMANI; hauhimizi "uchaguzi" usiokuwa wa HAKI

Sasa usitafute kupotosha watu humu. kuwa hayo mambo mawili yanazungumzia taarifa tofauti
 
Ni kupoteza muda! Watu walishaomba na kuomba na kuomba lakini hakuna matoleo! Hapo ni sawa na kuomba chupa iondoke mezani bila kuchukua hatua ya kwenda kuiondoa kwa mikono yako.

Ukingoja kuwa Malaika watashuka kuleta haki na amani bila kuipigania tutangoja miaka na miongo na miongo!
Mwishowe nitakuwa najaza majibu kwenye mada hii; kana kwamba nimeianzisha mimi!

Mkuu 'sysafiri', siyo kweli kuhusu hilo unalolizungumzia wewe.
Hiyo sala; pamoja na ushiriki wa watakao ishiriki sala hiyo wao siyo kama maroboti yaliyo wekewa program ya kuyaendesha. Hawa ni binaadam, wanao uwezo wa kuelewa; na wakielewa watatenda kama walivyo eliwa.
Hawa ndio watakao "sogeza" hiyo chupa kwenye meza" unayoizungumzia wewe. Wanao utashi wa kufanya hivyo.

Sasa usitegemee tu, "wasogeze chupa" kama unavyopanga wewe katika akili yako. Kuna njia nyingi sana za "kuisogeza" chupa, na hawa wanaweza kuwa na mchango mkubwa zaidi katika kuhakikisha HAKI na AMANI inakuwepo katika taifa letu; hata kama hao wanaolazimisha vitu hivyo vivurugwe.
 
Back
Top Bottom