kwa maslai ya taifa
Senior Member
- May 2, 2025
- 175
- 178
Mama wa kilemba atak kuona neno HAKI kwenye maombi..
Maombi ndiyo yataleta majibu kutoka kwa Mungu kuhusu kifanyike nini.Kupitia waraka huu wa kanisa katoliki ni dhahir shahir kuwa, kanisa linatambua kuwepo kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2025.
Je hii ina itamaanisha nini kwenye kampeni ya " No Reform No Election" ?
NRNE Movement itaathiriwa kwa kiwango gani na waraka huu wa kanisa katoliki?
=============
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa taarifa ya wito wa kufanyika kwa Sala na mfungo wa kuombea Haki na Amani nchini Agosti 23, 2025 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025
Taarifa ya leo Juni 20, 2025 iliyotolewa na Baraza hilo imesema kuwa kila Jimbo, Parokia, Jumuiya za Kitawa na Taasisi wataweka utaratibu utakaowawezesha kusali na kutubu kwa masaa 12 au 24 kulingana na uwezo wa Mazingira.
View attachment 3376972
Mnaomba kila siku, majibu tutarajie lini mkuu?Katoliki ndio wanaanza leo aisee sisi kila siku huwa tunaomba sala kama ilivyoagizwa na Mtume Paulo kwa Timotheo kwenye Biblia kama jambo la kwanza kwenye sala
1 Timotheo 2: 1-2 inasema
"Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli."
Kwa hiyo hao katoliki kuomba hiyo sala hadi watenge siku maalumu na kupiga tarumbeta kuwa kutakuwa na hiyo sala
Aiseeee .Biblia wanasoma au hawasomi? Eti sala maalumu.Hiyo inatakiwa kuwa sala ya kwanza.Sisi wengine kila siku tunaomba na kabla ya sala yeyote huomba hiyo
Mtume Paulo wanamuelewa au hawamuelewi? Aibu kuitisha kuwa itakuwa sala maalumu
Udini, sawa na bangi au kileo, husababisha uraibu. Ukituliza kichwa utakumbuka waraka uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki wakati wa utawala wa Magufuli, ambao Kadinali Pengo alijitenga naoAkikaa pale juu muislamu, chokochoko haziishi. Wakati yupo jiwe hamkufanya maombi wala kuroga, kwakuwa mwenzenu, mnataka kusema enzi za jiwe haki ilikuwa yakumwaga sio, acheni ulofa, kuleni spana mbavu zenu
Yaani baba afanye muhadhara na mtoto wake Tena wa kambo, mi naona sio kwamba hawataki bali hawataki kushusha hadhiMimi huwa najiuliza kwani hawependi kufanya midhara ya kidini wakati wajaa wasomi wengi wa dini mfano wafanye mhadhara wakatoriki na waislamu
Sala za Kila siku zipo saa 12 kabla watu hawajaenda makazini wanapitia kanisani kusali daily,Ruksa siwapangii nawakumbusha hiyo sala ya amani inatakiwa kuwa ya kwanza kila siku au kabla ya sala yeyote kama mtume Paulo alivyoagiza sio ooh unasema leo ndio nitafanya ni upofu wa Biblia wawe wanasoma Biblia kabla kutoa hizo nyaraka zao
Wewe binafsi huna amani? Kama unayo ndio majibu ya maombi yetuMnaomba kila siku, majibu tutarajie lini mkuu?
Kwa hiyo mnarudia kitu kile kile mnachoomba kila siku?Sala za Kila siku zipo saa 12 kabla watu hawajaenda makazini wanapitia kanisani kusali daily,
Sala maalum ni kwa ajili ya jambo maalum, acha kujichetua dogo
Elewa neno maombi maalumu, afu elewa HAKI na AMANI kuekekea uchaguzi mkuu,Kwa hiyo mnarudia kitu kile kile mnachoomba kila siku?
Halafu kila misa huwa mnaomba tutakiane amani .kila mtu akimtakia amani mwingine.Hizo sala huwa za kazi gani?