Tanzania kuna familia ambazo zinaishi kifalme bila Watanzania kuzifahamu au wamepiga kimya tu

Thanks
Huu utaratibu haufutwi kwa jitihada za mtu bali kwa mfumo usiotegemea watu. Unaona sasa unaongelea mtu aliyekufa?
Mfumo kweli lakini kubadilisha huo mfumo lazima kuna mwanzilishi wa hilo Wazo la mabadiliko!
 
Nakubaliana na mawazo ya Askofu Bagonza. Mabadiliko ninayumhusisha nayo mwendazake ni mabadiliko kwanza ndani ya ccm kutokuwa tegemezi wa wafanyabiashara kwa kuwa na vyanzo vyake vya mapato!! Kufanya hivyo kunaisadia serikali kutokuwekwa mifuko hivyo kupunguza rushwa kwenye chama na serikali!! Bila kukithibiti chama ni vigumu kubadilisha mifumo ya serikali kwa utaratibu uliopo!!

Kuwa mwendazake alikuwa mpinga mabadiliko #1 sina hakika; Mimi nadhani it was just a question of timing when to strike the iron! Ingawaje sikukubaliana na jinsi ya mambo mengine alivyokuwa anaexecute!
 

Tambua mabadiliko ya msingi ni katika nchi.

Nchi ni vyote. Tanzania ina watu 60m+ si sahihi kwa awaye yote kufungamanisha CCM au Chadema na Tanzania mpya.

Kwamba mwendazake hakuwa kikwazo kwa Tanzania mpya? Labda wewe kama ni mgeni duniani.

Kumbuka Tanzania mpya = Mustakabala mpya = Katiba mpya

Hiyo ndiyo habari yenyewe.
 
Sina pingamizi na mawazo yako. Mimi siamini kuwa mwendazake alikuwa anapinga kupatikana kwa katiba mpya bali alikuwa anataka kuwa strategic kutokana na upinzani ndani ya chama chake! Ingawa matamshi yake yalikuwa hivyo!
Kwa jinsi nchi yetu na watu wake tulivyo kuwa unlike nchi nyingine, utashi wa vyama vikuu vya siasa ni muhimu ili katiba ya wananchi kupatikana kwa Amani!
 

Mwendazake ndiye aliyekuwa muasisi wa genge la wasiojulikana. Lengo na madhumuni?





 
 
Huu UZI unaingia hapa, kwenye huu UZI mwingine wa Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana, ngoja kesho nikipata muda mzuri tutajadali kwa kina namna au jinsi huu MFUMO unavyofanya kazi.
 
Wamezaliwa kuwa viongozi, wewe kalime korosho mtimbwilimbwi
 
Maji hufuata mkondo, hata kwa wafanyabiashara matajiri au wasomi watoto wao wana good chance ya kuwa matajiri, pambaneni mfungue njia kwa generations zenu zijazo ndio maisha yalivyo, na ukiwa maskini chance kubwa kwa wanao ni umaskini tuu
 
Mpaka akili zikae sawa ndio tutaelewana, mkiambiwa inatakiwa katiba mpya itakayo yatia hatiani haya majizi ya CCM hamuelewi. Wote tukianza kuimba wimbo mmoja tutafika nchi ya asali na maziwa
 
Mwisho wa kufikiri kwako
 
2. Sio kweli
4. Mke ni mbunge
5. Udas ni sawa na katibu tarafa
6. Mtoto wake ni mbunge zanzabar
 
Wewe ndiyo mwisho wakufikri kwako! Tuwe na aibu hata kidogo! Hivi kuna mzazi anayependa mtoto wake apate shida na wakati ana nafasi zakuweza kumsaidia?? Na bado mtoto ana Elimu yakuweza kushika hiyo nafasi??
Wewe mwenyewe una elimu. Mbona usipewe NW?
Nchi ina utawala wa kimwinyi kwa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…