Tanzania na Equinor / Shell yasaini mradi wa thamani dola bilioni 30

I heard it right, ubepari!
 
Itakuchukua muda gani kudungua kuwa mradi utekeezaji huenda ukaanza 2027 au zaidi ya hapo. Na hata probably 2030??
 
Toka maktaba :

25 January 2022

January Makamba : Mkataba Hodhi (HGA) kati ya Serikali na wawekezaji, Shell na Equinox


Alichokisema JANUARY MAKAMBA kuhusu mkataba wa ushauri | Uchakataji gesi asilia TANZANIA


Arusha.Serikali ya Tanzania imesaini Mkataba wa Huduma ya Ushauri Elekezi utakaosaidia kujihakikishia manufaa ya Taifa katika uwekezaji wa Mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia(LNG), mkoani Lindi.

Mkataba huo umesainiwa leo kati ya Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania(TPDC) na Kampuni ya Baker Botts UK LLP ya Uingereza ikiwa ni miezi mitatu imepita baada ya kuanza tena majadiliano ya Mkataba Hodhi(HGA) kati ya Serikali na wawekezaji, Shell na Equinox.

Hii inamaanisha kwamba, kampuni ya Baker Botts imepewa dhamana ya kuhusu maslahi ya Taifa kupitia mradi huo uliokuwa umepoteza matumaini kwa miaka saba mfululizo kutokana na mwenendo hafifu wa majadiliano ya HGA.

Majadiliano ya HGA ndio yanayoweka msingi wa namna pande mbili zitakavyonufaika kupitia mikataba midogo inayohusisha masuala mengi ikiwamo mgawanyo wa mapato, usuruhishi wa mogogoro, matumizi ya ardhi na usafirishaji. Katika tukio hilo jijini Arusha, Waziri wa nishati January Makamba alisema kama ilivyo utaratibu wa kimataifa katika masuala a majadiliano ya miradi mikubwa ya LNG ushauri wa kitaalam Kutoka makampuni yenye uzoefu ni muhimu .

“Mchakato wa manunuzi ya mshauri mwelekezi ulifanyika kwa mujibu wa Sheria na kampuni ya Baker Botts ilifanikiwa kushindwa zabuni ya kazi hiyo,”amesema. Waziri Makamba aliongeza kuwa kutokana na Nia njema ya Serikali katika kuhakikisha masuala ya majadiliano yanamalizika kwa haraka na kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi iliona umuhimu wa kupata mshauri mwelekezi mwenye uzoefu mkubwa katika miradi ya namna hiyo .

Baker Botts Hired by the Tanzania Petroleum Development Corporation to Advise on $30 Billion LNG Project​

26 January 2022
Release
LONDON, January 26, 2022 - Baker Botts (UK) L.L.P., a leading international energy, technology and life sciences law firm, confirmed press reports that it has been hired by the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC), the national oil company of Tanzania, as the Transaction Adviser to the Government Negotiation Team and TPDC regarding the development of a liquefied natural gas project.

The project involves development and construction of an onshore LNG plant to process and liquify natural gas from significant offshore natural gas discoveries in Tanzania and to export liquified natural gas to international markets.

The project would involve TPDC and the Government of Tanzania together with a number of international energy companies including Equinor, Shell, ExxonMobil, Pavilion Energy and Ophir Energy.
 
Hapa tukubali Jiwe alituchelewesha sana. Hii signing ilipaswa kuwa imefanyika tangu 2015, lakini uzalendo uchwara ukaingizwa kuturudisha nyuma. Right now na hii vita ya Ukraine tungekuwa tunavuna dola.
Kwenye madini tu miaka zaidi ya 50 Sasa, kaangalie tunachukua dola ngapi
Si tuna mradi wa gesi na tunazalisha umeme, umewahi kujiuliza kwa nn tunanunua? Au unafikiri hiyo gesi ya kuzalisha umeme tunachukua bure?
Kwa lugha nyepesi sisi ni wanunuzi kwenye mali yetu sababu kubwa inayotajwa ni hatuna mtaji Wala teknolojia
 
Ni kweli tulijitoa na hata yeye jpm alikua haweki wazi mikataba
Lakini kabla ya jpm kipindi tupo huko open governance mikataba ilikuwa wazi?
 
Nilikua nimekupa like, Ila baada ya kusoma hadi mwisho nikaitoa. Samahani
Kuhusu wataalamu wala hatuna wengi kama unavyosema, na Hilo linasemwa na haohao viongozi wa serikali kila mara. Makamba alisema kuhusu kuwapa tender kampuni ya nje kwenye negotiation sababu ndani hatuna wataalamu
 
Tuambie mapato yanayopatikana kwenye gas Mtwara umefaidika na nini mpaka sasa???
Unaposema mtu amefaidika au kutofaidika na gas ya Mtwara, unamaanisha nini. Nini vigezo vya kufaidika au kutofaidika? Kama unamaanisha kugawiwa pesa mkononi, sijafaidika.

Kama unamaanisha wananchi kupata ajira, nina hakika wapo (japo siyo mimi), kama ni Serikali kupata kodi, nina hakika wanakusanya (japo sijui ni kiasi gani), kama ni wafanyakazi wa umma kulipwa mshahara, najua wanapokea mishahara kwa wakati, tofauti na miaka ya nyuma kabla ya uwekezaji wa makampuni mbalimbali ambapo mfanyakazi alikuwa anaweza kufanya kazi miezi mitatu bila ya kupata mshahara. Kama ni kuwepo kwa baadhi ya huduma za jamii, ingawa bado ni chache na za kiwango duni, lakini kumekuwa na unafuu kuliko hapo zamani.

Kama laiti tungekuwa na kiongpzi mwenye akili timamu wakati wa awamu ya 5, ambaye angewezesha uwekezaji wa dola billion 30 kujenga LNG utimie nchini Tanzania kama ilivyokuwa imepangwa, sasa hivi, na kwa namna kulivyo na uhaba wa gas Duniani, tungekuwa tunachekelea, hata mafuta tungeweza kuilazimisha Setikali itoe ruzuku kubwa zaidi ili bei ya mafuta isipande.
 
Mkuu una miss point hapa
Mikataba haikuwa kuwekwa wazi hata kabla ya jiwe, wanaosema iwekwe wazi sasa nao wanapoteza muda kwa kuwa haiwezi kuwa wazi. Lakini ikiwa unaamini Magufuli alifanya kosa hilo, mama Samia anapaswa kuendelea nalo? Mbona Kuna makosa Magufuli alifanya na Samia kayarekebisha?
 
Nakubaliana na wewe kwenye ya juu hapo Ila kusema jpm aliweka precedence mbovu nakataa kwa kuwa hata kabla yake mikataba haikuwa wazi na pia mama samia ameonyesha kurekebisha makosa yaliyofanywa na jpm kwa nn sasa kwenye hili useme iliwekwa precedence mbovu?(japo sio kweli)
 
The project involves development and construction of an onshore LNG plant to process and liquify natural gas from significant offshore natural gas discoveries in Tanzania and to export liquified natural gas to international markets.
Mkuu bagamoyo, my biggest interest ni LNG plant inajengwa onshore or offshore?. Hapa inaonyesha ni LNG plant itajengwa onshore, ila kama nimesikia sasa ni offshore!.
Soma concern zangu toka ile 2012. Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!
P
 
Pamoja na madhaifu ya Magufuli
Lakini huu wako ni uongo mkubwa sana
 
Nilichopenda na realistic timeline! Miaka 7!
Ila, ingekuwa mtu fudenge ungesikia jukwaani mradi lazima ukamilike 2025! Ili azindue hata kama ni theluthi Tu iliyokamilika!
Huenda hujaelewa chochote, kilichosainiwa ni HGA.
Mradi kuanza bado, huenda ukaanza 2027 au zaidi ya hapo au usiwepo kabisa kutegemeana na sababu mbalimbali ikiwepo upatikanaji wa pesa hizo
 
Mradi wa trillion 2, lakini hadi sasa ni miaka 9 bado haijarudi? Si ndio?
Trillion 70 itachukua miaka mingapi?
 
Umeongea vitu vyepesi sana, sasa kwa Teknolojia ya Leo ulitegemea huduma bado ziwe Kama miaka 10 au 20 iliyopita? Au ulitegemea mishahara ipitie miezi mitatu bila kulipwa?

Kuhusu huu mradi Kuna maswali unapaswa kuyajibu vizuri.
  • gharama za mradi
  • itachukua muda gani mradi kurudisha pesa ili nchi ifaidike
  • kwa Sasa kwenye gesi ya mtwara tunapata kiasi gani.

Ukishindwa kuyajua haya basi ni bora utulie tu
 
Mradi wa trillion 2, lakini hadi sasa ni miaka 9 bado haijarudi? Si ndio?
Trillion 70 itachukua miaka mingapi?
It’s beyond any sane individual kuelewa Barrick kupata 50% ya economic benefit baada ya kuchuma for decades.

Halafu wanasema wana trained negotiators na jamaa kwenye mazingira tunabembelezana nao wakishafanya yao.

Huku kwenye LNG labda wanadhani kuuliza ni chuki, wakati ata kwa layman tu ukiangalia approach na ukimsikiliza kiongozi wa nchi na waziri husika lugha yao ya kulilia mradi uanze unaona ni tatizo.

Mbele giza kuonyesha tu hadharani upo desperate kwenye negotiation yeyote ni disadvantage god knows how these people reason behind the scenes mpaka tulipofikia.
 
Kipindi Cha chairman Mao au Chiang Kai Shek China ilikua na uchumi Gani ndugu yangu, sembuse Japan was a power but China ilikua maskini kuna mpaka wakati watu zaidi ya million 20 walikufa kwa njaa.
Hivi huelewi kwamba hata Marekani enzi za akina Washgton nchi ilikuwa ni maskini?
Hapo Ulaya kuna nchi ngapi zilizokuwa na uchumi mzuri nyakati za akina Mao?

Hili nalo unataka uwe mjadala wa kuhalalisha upepari kuwa ndiyo njia pekee ya kuleta mabadiliko katika maisha ya watu?
"Reverse Engineering", nani hakufanya reverse engineering hata leo hii!
 

#TanzaniaLiquefiedNaturalGas Project (#TLNGP), also known as the Likong’o-Mchinga Liquefied Natural Gas Project (LMLNGP), is a planned liquefied natural gas processing plant to be located on the Indian Ocean, opposite Tanzania’s main offshore gas exploration sites. 11Tth June , 2022 :Tanzania signed a framework agreement on Saturday with Equinor (EQNR.OL) and Shell. This bring closer the start of construction of a $30 billion liquefied natural gas (LNG) export terminal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…