Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Ndugulile sijui ndungulile alipotoa wazo la kuweka gharama kwenye WhatsApp call nilijua kinachofuata huyo jamaa ni mjima kinyama kwa zama hizi hatakiwi kuwa na matamko ya aina hiyo...
Kama ni kiongozi hafaiiiiiii kabisa. Ni mtesi na asiye watakia watanzania mema !!!!
 
Tanzania ni nchi ambayo bado data sio ghali sana,ndo maana wengi wenye smartphone wanaweza kuzurura mtandaoni..sogeeni hapo Kenya muone balaa la safaricom,watu instagram wanaingia kwa machale.
Hii kitu ni kweli, kwa Tanzania bei ya vifurushi ipo chini ya gharama halisi. Serikali ndio ilitaka vifurushi viuzwe kwa bei halisi ili ikusanye pesa nyingi ila makampuni ya simu yamekuwa yakifanya under pricing ili kumaitain ile customer base.
Ila najiuliza waliposema mkongo wa taifa utaisaidia kushusha bei za data ndio zinaongezeka kila siku?

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
IMG_1852.png
 
Katika maisha yangu sitokaa nimsahau jiwe
Amewaharibia watanzania wengi sana utaratibu wao wa maisha ya kila siku kwa sababu zake tu binafsi, na hulka yake ya kuwa mtu mwenye roho mbaya ya chuki na ubinfsi ulio pitiliza!

Kiukweli walistahili kabisa kufanya sherehe mara baada tu ya kifo chake.
 
Kauli yako ya Kifedhuli na Kidharau kama hii ndiyo ilisababisha hata kule nchini Ufaransa mwaka 1789 kukawa na French Revolution ( Mapinduzi ya Ufaransa ) baada ya Mke wa Mfalme Louis XVI aitwae Malkia Marie Antoinette kusimama katika Balcony na Kuwaambia Waandamanaji waliokuwa wakilakamika Bei ya Mkate kuwa juu na Yeye akawaambia Wanunue Keki wale.

Hivi Bei ya Mkate na Keki ni sawa? Na Wewe unavyowakejeli hapa wanaonunua Bando za Buku Buku na kuwataka Wanunue za Tsh 30,000/= hii siyo Dharau iliyovuka Kiwango?

Usisahau huyo huyo aliyekupa Wewe huo Utajiri ndiyo huyo huyo pia amewapa wengine Umasikini. Sikutegemea Member kama Wewe kuwa na Kejeli hivi kama alizokuwa nazo Malkia Marie Antoinette wa Ufaransa.

Mpaka nimesema hivi jua umekera sana.
Tumsamehe labda hajakua,akikua atayaona!
 
Nijibu swali, yeye kama waziri alitumwa na Mkuu wake wa kazi, Je unamjua aliyemtuma???.
Acha uboya sasa umengangania kutumwa kutumwa kwani kila anachofanya waziri katumwa we vp
 
Hii sera nadhani ilipangwa kutukomoa wapenda HAKI ili kwa kujua uchumi umebanwa hivyo wakosoaji watapungua.

Naamini Mama ataliangalia pia maana huku kwenye mitandao anapita na kusikiliza mengi mno na maoni mengi anayafanyia kazi.

Tuombe hivo kuna vijana wako mtaani wanategemea internet kutafuta kazi pamoja na kutuma maombi yao
 
nchi inaenda Kua ngumu sana zaidi hata ya kipindi cha Magufuli subiri muone
Hii ni kwa ya mwendazake na sio kwa ajili ya Mama, kwani wakati panapandishwa huu ujinga nani alikuwa juu ga Sheria/Msemaji wa mwisho?

Ingekuwa ni kwa ajili ya kumfurahisha basi siku hiyohiyo angemtumbua huyo waziri.
 
Wakti Rwanda ikihangaika kurusha satellite ili wanafunzi wao wa vijijini wapate intaneti ,sisi tunahangaika kupandisha.
 
Hii ni kwa ya mwendazake na sio kwa ajili ya Mama, kwani wakati panapandishwa huu ujinga nani alikuwa juu ga Sheria/Msemaji wa mwisho?

Ingekuwa ni kwa ajili ya kumfurahisha basi siku hiyohiyo angemtumbua huyo waziri.
kwahiyo tutegemee nini? kushushwa kwa vifurushi? au moto ni ule ule?
 
Amewaharibia watanzania wengi sana utaratibu wao wa maisha ya kila siku kwa sababu zake tu binafsi, na hulka yake ya kuwa mtu mwenye roho mbaya ya chuki na ubinfsi ulio pitiliza!

Kiukweli walistahili kabisa kufanya sherehe mara baada tu ya kifo chake.
Aisee we wacha ndugu yangu mifumo yoote ya maisha imekuwa paralysed.

Sijui huyu mama atawezaje kuirudisha kwenye hali yake ya kawaida.
 
Mkuu! Freebasics ni huduma ya mtandao ya bure hautumii MB's!.
Kuna Facebook, BBC news and Swahili, Jamii Forums na nyingine nyingi sana!.
Inapatikana kwenye OperaMini!
Haijanipa chochote kaka au unarekebisha setting au ipoje
 
Hii kitu ni kweli, kwa Tanzania bei ya vifurushi ipo chini ya gharama halisi. Serikali ndio ilitaka vifurushi viuzwe kwa bei halisi ili ikusanye pesa nyingi ila makampuni ya simu yamekuwa yakifanya under pricing ili kumaitain ile customer base.
Ila najiuliza waliposema mkongo wa taifa utaisaidia kushusha bei za data ndio zinaongezeka kila siku?

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Yes,serikali inataka ikusanye kodi zaidi..

Ni kama kwenye mafuta(petrol,diesel) tu..bei ya mafuta ikiwachini serikali haifaidi..ndo maana kuna petrol station zilishusha bei zikazinguliwa.

Wanaolaumu makampuni haya wanafanya kuwaonea tu.
 
Back
Top Bottom