Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

View attachment 1740133
Royal bando

View attachment 1740134
Mega bando kwa wiki

View attachment 1740136
Internet kwa wiki


Kwa mabadiliko haya ya vifurushi kwa nini Waziri Ndugulile asijiudhuru kwa kuudanganya Umma wa Watanzania. Tuliaminishwa kwamba vifurushi vitapatikana kwa gharama nafuu, imekuwa kinyume chake.

Kwa heri Halotel, niliwapenda lkn ndo basi tena. Na jana nimetoka kuwapigia chapuo kuwa mko vizuri, kumbe sikujua masaa machache yajayo ingekuwaje.

Baada ya kutoa yangu moyoni, tujuzane wapi pa kukimbilia kwa sasa.
Hakuna maana kote mambo ndiyo hayo hayo.Cha kufanya ni kuachana na mitandao na hizo MB wakae Nazo stoo kama ni dili sana.Tuone watakusanya nini kwa kuongeza gharama?
 
Mkuu wataachia Tu boss tulishawahi nunua mb 70 Kwa jero ,
 
katika hili la kupandishwa kwa gharama za vifurushi wa kilaumiwa sio mama samia, ni mwendazake.

Mwendazake alikuwa hapendi kukosolewa, alionyesha chuki ya wazi kabisa kwa watu waliokuwa wanamkosoa kupitia mitandao ya kijamii. Akafikia hatua ya kutamani malaika washuke wazime mitandao yote.

washauri wake kwa kutambua chuki ya wazi ya boss wao kwenye mitandao, wakaona bora wamfurahishe, wakaja na idea za kutumia vpn kwa upande wa twitter (japo haijasaidia) na kuongeza gharama za vifurushi.

Matokeo ya idea hizo ndio hii bei mpya ya kikatili ya vifurushi. ndungulile na team yake walisukumwa zaidi na utashi wa kisiasa kuliko utu ili wamfurahishe boss wao ambaye kwa sasa ni marehemu.

sina shaka na Mama Samia, najua atafikishiwa malalamiko kuhusu vifurushi hivi vya sasa ambavyo sio rafiki kwa mwananchi mwenye kipato cha chini na haraka sana atatoa amri ya kuvisitisha.
 
Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wanachezewa akili na viongozi wao kadri wanavyotaka!

SUALA la gharama za mitandao kuwa juu lilipigiwa sana kelele Bungeni. Tukaahidiwa litafanyiwa kazi, tukakaa tukasubiri tukiamini kilio cha Watanzania kitapatiwa utatuzi kweli tukatangaziwa kwa MBWEMBWE nyingi kwamba kuanzia APRILI bei ya VIFURUSHI itapungua, ajabu badala ya kupungua vimepanda! Hongera sana WAWAKILISHI wetu.View attachment 1740967
Airtel 1000 unapata 1gb!! 2000 unapata 2gb.. hii ndio inaniweka mjini kwa sasa.
 
Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wanachezewa akili na viongozi wao kadri wanavyotaka!

SUALA la gharama za mitandao kuwa juu lilipigiwa sana kelele Bungeni. Tukaahidiwa litafanyiwa kazi, tukakaa tukasubiri tukiamini kilio cha Watanzania kitapatiwa utatuzi kweli tukatangaziwa kwa MBWEMBWE nyingi kwamba kuanzia APRILI bei ya VIFURUSHI itapungua, ajabu badala ya kupungua vimepanda! Hongera sana WAWAKILISHI wetu.View attachment 1740967
Hawa ni wafanya biashara ambao wamekubaiana kubeep uongozi mpya kuona nini kitatokea
 
Unaongelea Mambo ya kuattack nmekwambia neno moja tu wewe ni stupid maana naonaga maneno yako humu si unaona unavoendelea kumuattack mtu usiyemjua
Now you are talking Mkuu..

Kumbe una personal grudges!

Sasa nimeelewa, ni zaidi ya nilichokoment hapa.

Thanks kwa kuwa wa kwanza kujiweka wazi.!

Mind you, I love you.

Good day Mkuu wangu!
 
Hii mitandao bwana Kama vile walikaa meza moja wakaambizana kutukomoa

Alianza Tigo, Akafuatia airtel , akafuatia halotel, then voda.

Ndugu zanguni niwashauri, kila mmoja afungue WI~FI nyumbani kwake, au kama zinapatikana za kutembeanazo kila mahala itakua poa.


Kitu kingine pia huenda imesababisha kwa hawa wananzrngo kupunguza/kuongeza gharama za mitandao na kuona wanapata hasara, itakuwa sababu kuu kodi kuwa juu, ikapelekea kufanya maamuzi hayo,, nahisi itakuwa ndio sababu hiyo.


Tunamuomba mama samia ashushe kodi, kodi iko juu mno na masharti juu.
 
Si alisema watu wanapiga sinu wasapu kwa kutumia internet na kuukosesha serikali mapato. So wamepandisha bei ya internet ili wajiongezee kipato.
 
Back
Top Bottom