Tanzania tuachane mfumo wa kupandishia watu mishahara bila kuwa na vigezo vya utendaji (performance)

Hayo yafungulie uzi wa mada yake.. Hapa mada ni namna ya kuongeza mishahara na vyeo.

Hakuna aliyelaumiwa hapa. Kusema watu wana underperform siyo kulaumu bali vigezo vyao vikiainishwa halafu hujawapa vitendea kazi watakuwa na haki ya kuachana na hiyo kazi, kwanini ufanye kazi sehemu ambayo haikupi vitendea kazi? utakuwa juha au haufahamu "fundamentals" za kazi yako.

Mfano wewe fundi mekanika uambiwe tengeneza magari bila spana? Ukikubali si wewe ndiye juha au mzembe, hakuna zaidi.
 
Mawazo mazuri mkuu...ila nani atafanya hio appraisal kwa mwenzake?? kila mtu ana interests zake akiwa kazini, the whole system iko corrupted
 
Kwa hapa kwetu usishangae huyo inspector atapewa mlungura anaishia zake siku imeingia🤣
 
Bado sana,Kazi zenyewe hizi za Mjomba na Shangazi.
 
Kwa hapa kwetu usishangae huyo inspector atapewa mlungura anaishia zake siku imeingia🤣
Hapo kutakuwa kuna uzembe kwa mtoa na mpokea hilo hongo.

Nyerere aliwahi kuongelea rushwa ya kwetu huku na ya nchi zilizoemdelea. Ilikuwa kama hivi (simnukuu neno kwa neno bali nilivyoelewa mimi) Kule alisema anapewa mkandarasi kazi kwa kuwa ana mtu wake hapo alipopewa hiyo kazi lakini kazi inafanyika. Hapa kwetu anapewa mtu hiyo kazi kwa kuwa kuna mtu wake na kazi haifanyiki.

Utajaza mwenyewe.
 

Nakumbuka alitolea mfano wa ujenzi wa barabara kama sijakosea sana alikuwa ameulizwa swali na mwandishi wa habari, anyway ndiyo sisi hao
 
Hapo ni kama kusema CAG anapokea hongo?
Mkuu, kuna uzi humu unawalalamikia hao watendaji wa CAG kuwa wamekula sana rushwa huko walikopita kufanya kazi, bahati mbaya sikumbuki title yake
 
Bado sana,Kazi zenyewe hizi za Mjomba na Shangazi.
Ndio hivyo, hayajaanza leo, wakati wa Nyerere tulikuwa tunaziita "undugu-naizeshen".

Tena ni bora sasa kwa Mama hatulioni hilo. Ingekuwa linaonekana tungeona Waunguja wamejaa kila sehemu. Umesahau juzi tu, wakati wa bwana yule?
 
Nakumbuka alitolea mfano wa ujenzi wa barabara kama sijakosea sana alikuwa ameulizwa swali na mwandishi wa habari, anyway ndiyo sisi hao
Yes.Sawa kabisa.
 
Ndio hivyo, hayajaanza leo, wakati wa Nyerere tulikuwa tunaziita "undugu-naizeshen".

Tena ni bora sasa kwa Mama hatulioni hilo. Ingekuwa linaonekana tungeona Waunguja wamejaa kila sehemu. Umesahau juzi tu, wakati wa bwana yule?


Nice to see you tonight, 👍🤣

Nilikufungulia uzi humu sikuoni rafiki, furaha yangu kukuona.

Sikujua kama nachangia uzi wako kiongozi
 
Mixer wakikutana na hawa so called wanasiasa alooh hii nchi bado sana
 
Kwani hoja ya msingi ni kupanda kwa mshahara? Ambapo wewe unadai eti mpaka mtu afanyie appraisal? Hii haipo kikatiba maana ibara ya 23 inaweka wazi kuwa mtumishi ana haki ya kupata mshahara stahiki kukidh mahitaji yake.

Hapa Tanzania unachodai kuwa hakifanyiki kinafanyika sana. Ndio maana kila mwaka watumishi wanajaza Opras kusimamiwa na wakuu wao wa kazi. Wewe hujui kitu umekurupuka
 
Nianze kwa kukupongeza Mkuu Dada yetu FaizaFoxy kwa mada hii. Hizi ndio mada za kwa maslahi ya taifa. Naunga mkono hoja

Mimi nilianzia kazi serikalini early 1990s. Mwaka 1998 mradi wa PSRP ilikuja na kuleta Sheria mpya ya utumishi wa umma, sheria No. 8 ya Mwaka 2002 ili introduce performance appraisal system ya OPRAS, kila mwanzo wa mwaka unajiwekea smart objectives na bosi wako, katikati ya mwaka mnafanya MTR, na mwisho wa mwaka mnafanya review based on performance ya zile SMART objectives.

Haya yote yalifanyika kupitia PSRP Project, sasa sijui hali ikoje.
P
 
Mzee Paskali mimi sio mtumishi ila nina mwenzangu ni mtumishi wa umma. Opras huwa zinajazwa kila mwaka. Na ndik tahmini pekee ya kujua utendaji kazi wa mtumishi .

Afisa utumishi ndio huwa anafanya appraisal na kuzituma mahala husika.

Ibara ya 23 ya katiba ya JMT inatoa haki ya mtumishi yoyote yule kupata mashahara unaokidhi mahitaji. Hii haimanishi kuwa lazima afanyiwe tathimini maana haki ya kukidhi mahitaji ni haki ya kikatiba.
 
Mkuu Idugunde , appraisal haifanywi na ofisa utumishi, inafanywa na your line manager, kazi ya ofisa utumishi ni usimamizi na kuzituma.

Sijaingia kwenye hicho kifungu cha katiba kuhusu mishahara, ila kwenye hili la mishahara, niliwahi kutofautiana na Blaza wangu,Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote
kufunga macho kufungua!, aliweza!. Aliwezaje?!, sijui!.
P
 
Bi Faiza nakuunga mkono kwa asilimia zote

Tena mimi huwa natamani hata mchakato wa kuajiri waalimu ziingizwe interviews, haiwezekani graduates wengi mtaani lakini kigezo bado ni degree!!

Mwisho wa siku waalimu wanaochaguliwa wengine ni tia maji tia maji na wakishaingia hawafanyiwi review yoyote hata wakifelisha consistently.
 
Wazo zuri....ila subirini tustaafu

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Sasa wewe unaandika halafu unajipinga mwenyewe. Unaelewa ulichokiandika? Au ndio meamka nazo "kangala"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…