Tanzania tuachane mfumo wa kupandishia watu mishahara bila kuwa na vigezo vya utendaji (performance)

Wafanyakazi wanauza muda ili wapate pesa.

Afrika hakuna anayezingatia muda kwa ajili ya kufanya malipo.

Tunafanya kwa mazoea na malipo yetu ni masikhara.

Nani analipwa anachostahiri baada ya kufanya kazi stahiki.

Hivyo Thumb rule ndio msingi wetu na kupanda madaraja ni kautamaduni tu.

Ila hiyo system ya pili Ina raha zake na karaha.

Wao serikari wanapunja stahiki zako na wewe iba muda wao.

Ni ngumu kuitekeleza kwa taasisi za umma.
 
Tatizo wanaotegemewa kupandisha mishahara nawenyewe performance yao ni zero kabisa!

Mwenye performance mbovu anampima mmbovu mwenzie ilhali yeye anajilipa vizuri na ubovu wake!

Nchi hii tukubali tu kuwa tumekwama, labda ndipo tutaanza kuyaona matatizo yetu na kuyafanyia kazi
 
Performance appraisal ni mtindo unaotumika hata hapa nchini kwenye mashirika/taasisi binafsi ambazo zinafanya kazi kimataifa kama migodini na kwingineko.

Sehemu yenye mfumo huu mfanyakazi anafurahia kujituma kwa kujua atavuna anachopanda.
 
Ila kumbuka Ukitaka Kuwabana Watu basi wape Pia Stahiki zao muhimu. Usitake kuwabana watu wakati hujawalipa Malimbikizo yao..mishahara haipandi . marupurupu hulipi..overtime hutoi

Ulaya huko watu wanalipwa Stahiki zao kwa Wakati tena Kwa Masaa siyo kama Sisi huku kwa Mwezi
 
The bottom line ni kwamba appraisal inafanyika hapa nchini.

Kwamba iwe kigezo cha kupandisha watu mishahara ni kinyume na katiba.

Kwamba rais hana mamlaka ya kupunguza mishahara ya yoyote? Hili ni suala la kisheria zaidi. Maana hao MaCEO aliowagusa wengi walikuwa wakilipwa mishahara iliyowekwa na mashirika yao kupitia board za mashirika. Sasa labda utujuze rais hana mamlaka ya kuingilia maamuzi ya hizo board?
 
Bongo serikalini si wana kitu kinaitwa OPRAS?
 
Siasa mbovu, poor leadership
 
mmmh bongo tunavyopenda connection, hapo hakuna atakae chapa kazi bali wataanza kutafuta connection tu
 
Kwenye Utumishi wa Umma Kuna wafanyakazi wengi tu wanakula mishahara bure,maana uwezo wao wa kudeliva ni mdogo sana........Kuna uozo mkubwa sana, watumishi wengi hawajui hata majukumu yao.....kazi kubebana bebana tu Kwa kujuana......kuna mtu tangu ateuliwe title fulani na Sa100 mpaka sasa nizaidi ya ndugu 50 wameingizwa serikalini...... wengine wanafanya usaili wengine wanaingia tu dairekti bila jasho.....inaumiza sana
 
Mimi naisi ungesema kupanda madaraja Ila kupanda mishaara ni swala linalousu sana Mambo ya kiuchumi Kwa wakati uwoo Ila madaraja ni kuusu utendaji kazii wako na apoo ndyo nafasi ya kuwaacec wafanyakazii sema Kwa Tanzania hasa serikalini kuna watu wataumizwa sna sababu kama umegombana na boss au hamuelewani ni rahisi sana kukukanyagia ili usipande daraja
 
Huijui bongo ww watu watatumia huo huo mwanya kupiga hela ili mtu asiye na sifa apande bongo kila kitu ni deal ila kiufupi kama gharama za miasha zimepanda na mishahara lazima ipande bila kuangalia performance au kitu kingine chochote kile.
 
Maajabu! Hivi inakuwaje watu wanapinga hata mawazo chanya yanayoweza kuleta mabadiliko.

Definitely, to impliment changes, force must be applied.
 
Rais alisema Tucta wawe wanakuja na tija ya wafanyakazi wao kama msingi wa hoja ya kudai maslahi yao vinginevyo hakuna salary increase.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…