Ngoja kwanza, ngoja ngoja ngoja.... kuna miaka hapa tunarushiwa ya uongo.
Tanzania Elimu Supply sijui ilikuwepo toka lini lakini hii picha haiwezi kuwa ya mwaka 1947 kwa sababu magazeti ya Uhuru na Mzalendo yanayotangazwa kwenye kituo cha basi hapo hayakuwepo mwaka 1947! Uhuru limezinduliwa desemba 9, 1961, liki replace Sauti ya TANU, Mzalendo limeanza Aprili 30, 1972, sasa iweje picha ya mwaka 1947 ika advertise gazeti la 1972 na 1961?
Kwa hiyo, miaka mingine mingi hapa, labda yote, inawezekana tunadanganywa. I mean, this is one of the most powerful threads on record at JF lakini kuna kamba nyingi sana humu zimechanganywa.