Kweli tulikuwa mbali sana! hata Internet cafe zilikuweko siku hizo! ni mwaka gani vile? hapa ni Moshi? naona Mlima Kilimanjaro

Hii ni ya juzi (2004 to 2007) naona Bendera za Celtel katika jengo linalofuata baada ya Posta.etc
 
Asante sana for taking us back thru' the time tunnel
 
CHADEMA ilianza siku nyingi, refer wanafunzi wa kisutu girls
 

Hapo kwenye bold ndio mpango mzima. Miji ya enzi hizo ilikuwa misafi sana, saa hivi mifuko ya plastiki ipo kila kona, masalia ya takeaway junks yapo kila kona. Tulitetereka wapi? Kuanzia lini?
 
Hakika tumetoka mbali najiona kama naota hivi! si unajuwa wengi wetu miaka ya 60 either hatukwepo au tulikuwa watoto wadogo.

Nimeipenda sana hii.
Halafu watu wanasema hakunA maendeleo
 

Heshima kwako mkuu! Asante kwa haya mavituzi ya zamani. Kumbe wanafunzi nao enzi hizo walikuwa wanachana nywele mtindo wa AFRO!
 
View attachment 74223

Hapa Ni Tanzania Elimu Supply(TES) Enzi Hizo 1947
Ngoja kwanza, ngoja ngoja ngoja.... kuna miaka hapa tunarushiwa ya uongo.

Tanzania Elimu Supply sijui ilikuwepo toka lini lakini hii picha haiwezi kuwa ya mwaka 1947 kwa sababu magazeti ya Uhuru na Mzalendo yanayotangazwa kwenye kituo cha basi hapo hayakuwepo mwaka 1947! Uhuru limezinduliwa desemba 9, 1961, liki replace Sauti ya TANU, Mzalendo limeanza Aprili 30, 1972, sasa iweje picha ya mwaka 1947 ika advertise gazeti la 1972 na 1961?

Kwa hiyo, miaka mingine mingi hapa, labda yote, inawezekana tunadanganywa. I mean, this is one of the most powerful threads on record at JF lakini kuna kamba nyingi sana humu zimechanganywa.
 

As a matter of fact 1947 jina la Tanzania lilikuwa halipo . Lilikuja baada ya Muungano wa 1964. Kwa hiyo picha ni ya baada ya 1964.

Mleta mada kapoteza credibility needlessly.

Thread ingekuwa bomba hata kama angeweka picha bila mwaka.

Lakini sasa inanuka uongo.
 

Tunavyosema Miaka 47 Maana yake ni miaka ya kitambo,Hakuna miaka iliyodanganywa hapo
 
Tunavyosema Miaka 47 Maana yake ni miaka ya kitambo,Hakuna miaka iliyodanganywa hapo
Hujasema "miaka 47".... umesema enzi hizo 1947. Tunavyosema? Tunavyosema wewe na nani? Umeandika fixi halafu unataka kuzuga na "tunavyosema miaka 47." Miaka 47 ya nini, ya Muungano?

Na hata uki assume kwamba kweli hukumaanisha 1947. Ina maana unakiri kwamba miaka ya kwenye hizi picha haimaanishwi kama ilivyoandikwa, ni ya kubuni tu, ya kuzuga, sio?

Nilikuwa nimeipanda sana hii thread maana it was a powerful vehicle to a different era, kumbe miaka yenyewe famba...

Hapa Ni Tanzania Elimu Supply(TES) Enzi Hizo 1947
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…