Tanzania yaongoza Afrika kwa kuwa na asilimia chache ya raia wake ambao ni diaspora

Apewe passport ili iweje kwamba watoto wote wanasafiri?
Tumia akili
Passport ni chanzo cha kipato. Kwa Serikali bunifu, ilipaswa kuwahamaisha raia wake kuwa na passport.

Kuwa na passport tayari tayari ni kuwa tayari kuidaka fursa itakayojitokeza.

Bahati zipo, lakini huwa zinatua mikononi mwa waliojiandaa!

Kuwa na passport mkononi ni kuandaa mazingira ya kukutana na fursa inayotembea.
 
Ukizaliwa Tanganyika HAKUNA KUTOKA.

Hili ni gereza lililochangamka.
Kwa afya ya Kisaikolojia, anayeishi Mjini asikose kutembelea maeneo ya vijijini, na wa vijijini nao waende mijini.

Anayetoka nchi maskini asikose kwenda kushuhudia maajabu ya nchi zilizoendelea, na wa nchi zilizoendelea wasiache kwenda kutalii kwenye nchi maskini.

Ni muhimu sana kusafiri, iwe ni kikazi, kibiashara, au hata kutembea.

Kuvuka mipaka ya nchi kutasaidia kuboresha fikra za wahusika.
 
Almanusura niseme "maskini...", lakini kwa sababu sikufahamu, acha nikae kimya.
 
Watanzania wengi waoga,wanaogopa Changamoto za Maisha ya nje ya Tanzania.
Kwa sababu ndivyo walivyojengwa na Viongozi wa kijamaa ili iwe rahisi kuwatawala. Hata baba wa Taifa, hayati Nyerere, aliwahi kukiri kuwa utawala wake ulichangia Watanzania wengi kuwa watu wa "ndiyo mzee"
 
Muongo. Wacha kupotosha wenzako.
 
Ningependekeza kila anayemaliza form six (21) aende nje hata kwa miezi sita, mwaka mmoja kwa kudhaminiwa na serikali / vyuo.

Ingesaidia sana kuongeza exposure. Miaka 16 kila Mtanzania apewe passport, NIDA, kitambulisho cha kupiga kura.
Hii ni hoja ya msingi sana. Exposure ni muhimu na ndiyo mwanzo wa kutawala mazingira ya ulimwengu kama kusudio la Mungu kwa wanadamu.
Hata hivyo, fikra potofu za kisiasa, ubinafsi unatokana na ujinga wa watunga sera, zinasabisha urasimu usio wa lazima katika taratibu za kutoka na pia diaspora kurudi nchini.
Umasikini kwa ujumla (wa mali na fikra) kuanzia kwa wananchi, watendaji serikalini na hata viongozi ni changamoto.
 
Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele kwa takwimu hizo. Hii inaonesha kuwa nchi yetu ni nzuri ndiyo maana kila mtu wnatamani kubakia hapa hapa nchini.

Diaspora kuwa wengi Ina maana nchi haikaliki, haivutii, haina potential kwa watu wake.
Uingereza walijenga nchi Yao kwa kutoka na kwenda kuvuta utajiri wa nchi zingine
Wahindi wametoka na kwenda kuvuna utajri nchi zingine same kwa wachina Wakenya we unaongea masuala ya kifua mbele wakati kupata passport unahisi ni mwenye bahati kupata viza unaona kabisa umewin maisha maana usumbufu wake ni WA hali ya juu sana.
 
Na nchi zinazoongoza ni zile zenye machafuko......
Middle east na ukanda wa Red sea, ndio zinaongoza hapo.
Unataka watanzania waondoke wanakimbia nini?
Nchi nyingi zenye machafuko ni kwa sababu mataifa makubwa wanataka kuvuna human capital ya nchi husika pamoja na rasilimali as unakuta watu wa nchi husika ni brain na nchi Yao pia rasilimali
Tz unaweza kuvuna rasilimali na kuondoka nazo bila shida ukisaidiwa na wao wenyewe Sasa uweke mgogoro wa Nini!?lakini human capital sio productive uitake ya Nini!?
 
Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele kwa takwimu hizo. Hii inaonesha kuwa nchi yetu ni nzuri ndiyo maana kila mtu wnatamani kubakia hapa hapa nchini.

Diaspora kuwa wengi Ina maana nchi haikaliki, haivutii, haina potential kwa watu wake.
Sahihi, sio fahari watoto kushinda kwa jirani wanadoea chakula na kuzurura wakati nyumbani kwao pamefungwa muda wote.
 
Wangekuwa brain wangepiganishwa na wao wakakubali kupigana?
 
Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele kwa takwimu hizo. Hii inaonesha kuwa nchi yetu ni nzuri ndiyo maana kila mtu wnatamani kubakia hapa hapa nchini.

Diaspora kuwa wengi Ina maana nchi haikaliki, haivutii, haina potential kwa watu wake.
Mimi nina mpango wa kutembelea nchi tu lakini sio kukaa
 
Usiumize kichwa chako.

South Africa apartheid. Nigeria, West Africa, kila mwaka mapinduzi ya kijeshi. Kenya vita vya maumau mungiki na sasa ukabila. Uganda wahindi walifukuzwa na idi amin wengine wakauliwa.

Sisi tuna amani, tuanze kuuana ili tupate ratio kubwa?

Indeed, ukiwauliza Rwanda huko waliko ni wapi utakuta kumbe ni Tanzania. Sasa tafuteni ratio ya DIASPORA INWARDS yaani waliokimbilia hapa.
 
Watanzania tunapaswa kutembea kifua mbele kwa takwimu hizo. Hii inaonesha kuwa nchi yetu ni nzuri ndiyo maana kila mtu wnatamani kubakia hapa hapa nchini.

Diaspora kuwa wengi Ina maana nchi haikaliki, haivutii, haina potential kwa watu wake.
Ni umasikini na ushamba wetu ndiyo unaotusumbua
 
Mkuu hujakosea. Kwanza kwa umri huo (21) huo unajifunza mengi jinsi vijana wengine wa umri kama wako wametoa nyumbani wanajitegemea.

Wanajua wanataka nini kwenye maisha na tayari wako serious na Wana mipango yao ya maisha. Wanapambana na maisha sababu hakuna alternative.

Wakirudi nyumbani watataka mazingira na mifumo iwe wezeshi kama huko walipotembelea, elimu iwe practical, haki zao kuzingatiwa.
 
tutapambana hapa hapa mtongani mamaq niende Namibia nikafanye nini ? nianze kupambana na lugha kuzoea sehemu afu niende sehemu sijuani na mtu eti ili mradi niko nje hapana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…