TANZIA: Mwandishi Lutengano Haonga wa TBC afariki dunia

TANZIA: Mwandishi Lutengano Haonga wa TBC afariki dunia

Party gani hiyo
Ipo YouTube mkuu ni uzinduzi wa kipindi kipya cha aridhio washereheshaji walikosa toothpick za kulishana keki wakaanza lishana kwa mikono....afu walirundikana sana kwenye kile chumba afu na mc pilipili alikuwemo kwaio tujiandae....

am better here
 
Too sad ujinga ni mzigo. Unajua nini Kirus haonekani kwa macho hivyo walipuuzia, wanapuuzia. Ngoja wiki mbili zijazo tutatafutana.
Kumbe wabongo hawajajua corona inauaje ? Haiwezekani Marin alikuwa kwenye party anapumua poa kirusi kikamchukua kesho yake kimya kimya lazima angekuwa Nan signs . Corona haiui hivyo
 
Kumbe wabongo hawajajua corona inauaje ? Haiwezekani Marin alikuwa kwenye party anapumua poa kirusi kikamchukua kesho yake kimya kimya lazima angekuwa Nan signs . Corona haiui hivyo
Itakuwa alikuwa na signs za mwanzo. Kushindwa kuhema ni sign ya mwisho. Halafu haikuwa kesho yake ujue. Zilikuwa zimepita siku mbili au tatu.
 
View attachment 1415685

Lutengano amefariki jioni ya leo hospitali ya Mloganzila jijini Dar.

Alikuwa mtu wa watu, rafiki wa watu na mtu muungwana sana.
Requiescat in pace, Ndugu Lutengano. Na salamu nyingi za rambirambi kwa nduguze, marafiki na watu waliokuwa wakifanya kazi naye. Mola awafariji katika msiba huu.

Pamoja na hayo, ningependa kusema kwamba msiba haukutokea kwa sababu ya kutakiwa kufanya kazi. Sababu hasa ya kifo ni jinsi marehemu na wafanyakazi wenzake walivyofanya wakiwa kazini. Walikusanyika kwenye hafla wakawa wakigusana na hata kulishana keki kwa mikono mitupu. Haya ndiyo serikali inasema tusifanye: tusisogeleane; tusisalimiane kwa kushikana mikono; n.k. Lakini kazini tuende. Kwa hiyo mtu asilete porojo ya kwamba marehemu amefariki kwa kutakiwa kutoka nje na kwenda kazini. Tufuate mawaidha tunayoambiwa na Rais, Mkuu wa Mkoa wa Dar, na Serikali kwa ujumla: tuchape kazi lakini tuzingatie maelekezo ya wataalamu wa afya, wakiongozwa na waziri mhusika. Zaidi ya hayo, kama Rais anavyotuasa, tusali na kumwachia Mungu afanye apendavyo wakati sisi tumetimiza wajibu wetu.
 
Back
Top Bottom