Tazama hapa makato ya kutuma na kutoa pesa kwa Vodacom (M-Pesa) kuanzia Julai 15, 2021

Tazama hapa makato ya kutuma na kutoa pesa kwa Vodacom (M-Pesa) kuanzia Julai 15, 2021

Huwa najiuliza zile raslimali ambazo tunaambiwa tunazo mpaka wazungu wanaitamani nchi yetu, yako wapi ili yatupunguzie hizi double taxation? Au hizo raslimali ni hizi line zetu za simu?
Mkuu sasa hivi tunapumua baada ya dikteta wako kufariki.

Isitoshe mama anafungua nchi na kurudisha hela mtaani ili tuwe tunaziokota [emoji23][emoji23][emoji23]

Nashauri hii kodi iongezwe mara 100 ili kuwakomoa mataga, sikuma gang na marehemu!
 
Pamoja na Waziri wa Fedha kuipigia debe kodi ya UZALENDO kiuhalisia bila kumumg'unya maneno INAUMIZA Itafika sehemu watu WAUKANE UZALENDO HUU ni wa KUUMIZANA.

Tumuombe MAMA SAMIA alitupie macho hili! IWEJE MUAMALA Mmoja ulipiwe kodi MARA MBILI? Nikituma hela nakatwa kodi, KUITOA hela hiyo hiyo Inakatwa tena, Haa UZALENDO GANI HUU! Tuwaombe wabunge na wao waanze KUKATWA asilimia 5% ya marupurupu yote wanayopokea nje ya MISHAHARA yao ili wachangie MAENDELEO yao.

Kila siku wanajificha kwenye kichaka cha MISHAHARA haitoshi lakini hawaweki wazi kiasi cha MARUPURUPU wanayopata nje ya MSHAHARA ambayo hayakatwi KODI. Sasa MWIGULU peleka HARAKA mswada Bungeni ili marupurupu yote ya wabunge ambayo hayakatwi kodi yaanze pia kukatwa kodi.

Naamini kama ulifanyia kazi USHAURI wa mbunge ZUNGU aliyeanzisha hoja hii MFU ya kodi ya UZALENDO bila shaka na hii utaifanyia kazi, UKIPUUZA basi TUKUTANE KWENYE SANDUKU 2025.
IMG-20210714-WA0140.jpg
IMG-20210714-WA0139.jpg
 
Shida kubwa ni kwamba tuna viongozi ambao IQ zao ni ndogo sana. Uwezo wao unaishia kukariri. Akikariri akapata A au B+ anaamini kuwa ana akili sana.

Waziri ambaye hajui kuwa ongezeko la kodi na tozo kwenye huduma wezeshi, indirectly kunasababisha kupungua mapato na kuzifanya sekta mbalimbali zisinyae, kweli huyo ana akili?
Mama anafungua nchi!

Kaaa kimya!
 
VAT na PAYE vinaenda kupunguzwa next year Ili ku stimulate uchumi...
Daaah, mkuu, unastahili pongezi kwa kumeza maji ya bendera, si ajabu ni Mwigulu flani hivi unayedai unalipwa mshahara ila hukati PAYE, unapewa mafuta kwa bei ya tsh 2,500 kwa lita tangu enzi na enzi, usiyejua gharama za usafiri, unayepewa airtime ya 800,000 kwa mwezi, unayelipiwa umeme na serikali, maji bure na lazima yawepo kwako.

Unajitokeza hadharani kuzungumzia watu wawe wazalendo kwa kukatwa kodi? Unajua wabunge 320 X 11,000,000 × 0.3 = 1,056,000,000

Sasa kwanini wasikatwe kodi tukapata hiyo 1.05bn kwa mwezi toka kwenye kipato cha wabunge, bilioni moja inajenga hizo zahani ngapi mara mwaka? Au ni mshahara wa walimu wangapi wapya kwaajili ya wanafunzi wetu?

Uzalendo ni nini kwanza?
 
Vyanzo vya mapato vingetoka mishahara ya wabunge kusingekuwa na yowe
Sasa kila siku kodi zinaongezwa huku tu kwao ni ganda la ndizi yaan senkeke tu na kitonga
Wenzako wanataka waongezewe mshahara wewe unataka wakatwe kodi. 😂😂
 
Pamoja na Waziri wa Fedha kuipigia debe kodi ya UZALENDO kiuhalisia bila kumumg'unya maneno INAUMIZA Itafika sehemu watu WAUKANE UZALENDO HUU ni wa KUUMIZANA...
Miaka 6 iliyopita yote umelalamika na hii ya Samia unalalamika tena?

Mpaka lini sasa?
 
Ni mambo machache sana yanayofanywa viongozi wetu yananiumiza, na hili ni moja ya jambo linaloniumiza mno nafsi yangu! Viongozi wetu wamezidi kutuumiza, huku hatujamaliza kuwaza rasilimali zetu hazitunufaishi ipasavyo tayari wametuletea huu upuuzi... Inaumiza sana
 
Daaah, mkuu, unastahili pongezi kwa kumeza maji ya bendera, si ajabu ni Mwigulu flani hivi unayedai unalipwa mshahara ila hukati PAYE, unapewa mafuta kwa bei ya tsh 2,500 kwa lita tangu enzi na enzi, usiyejua gharama za usafiri, unayepewa airtime ya 800,000 kwa mwezi, unayelipiwa umeme na serikali, maji bure na lazima yawepo kwako...
Dawa sio kupinga kodi bali kudai wasiokatwa kodi nao wakatwe kama hao wabunge nk

Pili lazima muelewe kwamba covid 19 imeharibu uchumi hususani biashara ya utalii ambayo ilikuwa inaongoza kuchangia mapato hasa fedha za kigeni,pamoja na biashara zingine.

Hivyo basi lazima pengo lizibwe Ili maendeleo yasisimame ndio maana tozo hizo lazima ziwekwe.Unataka nani akuletee maendeleo? Kuna watu walikufa ndio upo huru sasa wewe vikodi vya bando ndio unalia Lia kama mtoto yatima?

Kwa taarifa yako nimekwambia sina undugu na maccm wala Mwigulu ila naunga mkono hizi tozo kwa sababu tuu zimeelekezwa kwenye sekta mahsusi kwa hiyo nasubiria utekelezaji.

Wewe unaishi mjini sie wa Vijijini tunajua ugumu ulioko,kwamba wake zetu wafie njiani Kisa hakuna barabara na vituo vya afya?
 
Nipo Arusha jamaa yangu Extrovert yupo Moshi ananidai laki tano. Nikimtumia nakatwa karibu 8000/- nae akienda kutoa anakatwa zaidi ya 10,000/-. Jumla ya Transaction costs ni zaidi ya 20,000/-

Bora nitume hiyo hela kwa njia ya bus nikiwapa hata khaki (5,000) inafika. Au niende Moshi kabisa nauli kwenda na kurudi 7000.

Hapo tunabakia na change tunaweza kunywa hata beer mbili tatu.
 
Back
Top Bottom