PreGE2025 Tazama Luhaga Mpina akiondoka Uwanjani, Meatu baada ya mkutano wa Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ni mwendo wa Ndiyoooo tu,hata kama mambo hayaendi sawa..Wale tuliowaamini na kuwaita wazee katika hii nchi wanatukosea sana .
 
Mbona kufanya reference kwenye mambo yaliyopita?

Tunaenda mbele au tunarudi nyuma?

Kwa hiyo JPM ndiye rubber stamp kwamba kila alilofanya, lazima na wengine pia wafanye hivyo?

Kwa msingi huo, wanaotuzodoa kwamba hatuna malengo bora ya miaka ijayo, hivi hawako sahihi kweli?!
 
Mnaomhukumu na kumshambulia Rais mnajaribu kutuaminisha kwamba nyie na wengine ni malaika.
 
Mpina ametumia akili kubwa, kuagana na wananchi wake. katua zigo kwa Rais, kwa kusema wananchi wanamdai.

santuri ya mpina haitopotea kirahisi masikioni mwa wanakisesa maana hata wakiletewa mbunge mwingine wao, tayari wataamini deni lao liko kwa Rais na sio mpina.
yamkini ni kauli ya kibabe, mbele ya kiongozi mkuu wa nchi, lakini inamletea huruma na simanzi yeye mpina kutoka, kwa wananchi wake.
 
Ila tuende mbele turudi nyuma anachokitetea Mpina ni sahihi kabisa na watanzania wengi tunam-term kama mwanaharakati lakini unajiuliza kipindi cha Magu wakati yeye ni waziri mbona hatukuwahi kumsikia akipinga ukatili wa Magu hususani kunyanyasa wapinzani mfano wizi wa kura pamoja na kupigwa risasi akina Tundu Lissu...


Binafsi simpendi mama Samia, hizi harakati za kina mpina na Askofu Gwajina naziunga mkono huku nikiziangalia kwa jicho flani la mashaka... Najiuliza hivi mpina angeendelea na uwaziri hizi movement tungeziona kweli! Itoshe tu kusema binadamu siku zote maslahi binafsi kitu cha kwanza..
 
Sina hakika ila nafahamu magari huwa yanapaki pembeni kidogo ya eneo la mkutano ili kuruhusu wananchi ambae ndio walengwa wa mkutano washuhudie vyema waliyoketewa, sababu magari huwa mengi mkiruhusu yote yaingie eneo la mkutano itakuwa kipengele, hivyo huenda ilikuwa pembeni tu kidogo ya eneo hilo
 
Aseme alikopeleka T 17 sio kutuletea minyambo
 
Bashe ndio aliharibu zaidi pale alipotetea mnunuzi mmoja kwa zao la Pamba, alijisahaulisha kwamba wanunuzi wengine wanapita vijijini na kudai kwamba wao wana uwezo wa kulipa zaidi ya kile kilichopangwa papo kwa papo na sio kwa mkopo, mateso ya mtoa Huduma mmoja kama TANESCO ndio hayo wananzengo hawayataki,

Tunapoongelea Pamba maana yake Ni Musoma, Mwanza, SIMIYU, Shinyanga, Tabora na kidogo Singida,
Pia ndivyo barabara iliyotajwa ya ndanindani kupitia Meatu Singida mpaka Mbulu Ni kweli inahudumia watu walewale wa zao la Pamba

Ukiisha angalia hayo sasa jiulize Nani atakuwa man of the match
 
unaseema mpina anachuki na samia, chuki gani , ipi, na kwa sababu gani? Embu anika hapa
 
Huenda machoni pake anaona ni Sukuma gang vs Sa100!
Usimchezee Mfalme kwa sababu ndiye ameshika Upanga mkononi.
Hata akiamuru Mpina akamatwe na kuwekwa kizuizini anaweza.
Ujinga mtupu

Kwa style hii ndio maana wanakanyaga katiba wanavyotaka, je kuna sehemu Mpina alimtukana?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…