Tazama picha ya gari lililotengenezwa na wanafunzi wa UDSM

Tazama picha ya gari lililotengenezwa na wanafunzi wa UDSM

Kabisa mkuu. Hatulazimiki kurudi zama za ujima. Tukitaka kitu tunalazimika kujifunza kulingana na teknolojia ya sasa na kuwekeza ili tuzalishe kitu kinachohitajika sokoni.
Au tubuni mfumo bora zaidi wenye efficiency kubwa zaidi, pamoja na kutatua changamoto za uchafuzi wa mazingira na fuel demand
 
Umeandika vizuri kabisa ila umeharibu kuchanganya r na l. Ni mteRemko, sio mtelemko. Leo fanya mazoezi ya ra re ri ro ru. Kesho la le li lo lu, rudia wiki nzima utabadilika.
Swali muhimu kabisa ni: je wameweza kuunda engine yake from the scratch ??

Nauliza swali hilo kwani gari hasa ni Engine, ukiweza kuunda Engine basi vyote vilivyobakia ni mtelemko tu, kuunda Engine ndio elimu ya ma-engineers.
 
Kila aliyeyejadili hiyo picha ya gari kwa kuisifu au kuiponda bila kuomba apewe specification ya hiyo gari ajihesabu kuwa hana akili au ana akili ndogo mno tena mno hahitqji mtu wa kumwambua huna akili

Yeyote kabla kujadili alitakiwa kuomba apewe Specification ya hiyo gari iliyoko kwenye picha
 
Specifications muhimu design ya nje sio kitu cha maana ni kipengele cha mwisho

Magari ya Umeme ya Tesla yana design nzuri lakini wanunuzi wachache

Hununui design
Una kichaa wewe hebu kafuatilie gari nyingi kununuliwa mwaka Jana Scandinavian countries
 
Kila aliyeyejadili hiyo picha ya gari kwa kuisifu au kuiponda bila kuomba apewe specification ya hiyo gari ajihesabu kuwa hana akili au ana akili ndogo mno tena mno hahitqji mtu wa kumwambua huna akili

Yeyote kabla kujadili alitakiwa kuomba apewe Specification ya hiyo gari iliyoko kwenye picha
Kama hio gari ingekua na specification mwekezaj angetokea mapema na kuweka ela hilo gari ni mfano wa generation ya kwanza ya magari mwaka 1800's
 
Hv muendelezo wa vile viberenge vya kipanya uliishia wapi kweli?, viliingia barabarani kweli au vipo stoo km mabalo ya mtumba?!
 
Samaleko!

Hii ni picha ya gari lililotegenezwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha UDSM. Vipi maoni yako kuhusu huu ubunifu tutawafikia Wachina, Wajapani na German huko mbeleni au tuendelee na huu ubunifu uliojaa utundu.


Mimi kama mdau wa technologia, huwa na penda kutoa mawazo baada ya kujua Sifa na target market
Hivyo napenda kujua yafuatayo
  1. Usalama wake (stability yake ikiwa barabarani) ikoje
  2. Inabeba tani ngani/Abira wangapi na mizigo kiasi gani
  3. Uwezo wake wa kupita barabara za vijijini/Uimara wake
  4. Utumiaji wake wa mafuta (Lita moja Kms Ngapi?)
  5. Inatembea KM ngapi kwa saa (Speed yake ikoje
  6. Target marget/Soko lililo kusudiwa
Nikijibiwa hayo maswali nitajua namna ya kuchangia
Kimsingi magari yapo tayari sokoni hivyo hakuna haja ya kupoteza muda kutengeneza kitu chenye viwango duni kuliko kilichoko sokoni. Sana sana ujifunze kilichopo ili uje na kilicho bora zaidi kwa namna moja au nyingine na ndio sababu nikataka kujibiwa maswali hayo...
"Ungepiga picha ioneshe gari lote na picha moja ya Dashboard" - Natamani nilione vizuri ili nione ubunifu uliotumika
 
Umeandika vizuri kabisa ila umeharibu kuchanganya r na l. Ni mteRemko, sio mtelemko. Leo fanya mazoezi ya ra re ri ro ru. Kesho la le li lo lu, rudia wiki nzima utabadilika.


Kweli unaweza kunifundisha kiswahili katika maneno mengine lakini sio kwa hili neno:- " "mteLemko" eti usahihi ni "mteRemko" !!🤤

Angalia hapo chini👇🏻

Screenshot_20230417-122055.png
 
Kuna mkono na ujuzi wangu hapoooo.
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122], napaswa kujivuniaa.
 
Tatizo ni kulifanya Gari liende hapo ndio muziki munene
Nadhani hapo ndio rahisi zaidi, kwasababu mfumo wa kufanya gari isogee upo tayari hauihitaji wao kubuni, labda iwe tofauti na kutumia mafuta, umeme au gas. Labda iwe gari ya kutumia maji.
 
Back
Top Bottom