Tazama ushahidi huu wa kimahesabu wa Michango ya Lissu Unaothibitisha CHADEMA haifikishi wanachama hata million Moja

Tazama ushahidi huu wa kimahesabu wa Michango ya Lissu Unaothibitisha CHADEMA haifikishi wanachama hata million Moja

Maana imeonyesha wazi kuwa CHADEMA ni wapika data na hawana wanachama hata million moja tu.fikiria tu kuwa hata ikiwa wanachadema laki moja wangeamua kutoa elfu moja moja tu maana yake ni kuwa CHADEMA mpaka sasa wangekuwa wamepata millioni mia moja. Lakini bado wanatoka jasho utafikiri wameanikwa juani
Hapo wa kulaumiwa ni nani?Maana yake wananchi hawana hela.Kwa nini hwana hela?Uchumi mbovu.Nani kasababisha uchumi mbovu?Serikali na chama chakavu.Andika insha ya maneno laki tatu kutetea hoja.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Michago ya kumchangia Lissu Fedha za kununulia Gari imewaumbua sana CHADEMA, imewapa aibu,fedheha ,imewavua nguo hadharani na imeonyesha na kuthibitisha kauli yangu nayosemaga humu jukwaani kuwa CHADEMA imepuuzwa na inaendelea kupuuzwa na mamilioni ya watanzania kila uchwao.

Michago inayoendelea kuchangwa imeonyesha CHADEMA haina wanachama hai hata million moja tu.imeonyesha CHADEMA huwa wanapika takwimu ili kuwapofua macho na akili wafuasi wake kiduchu na wafadhili wao. Sasa kwa sasa tangia michango imeanza kuchangwa kwa ajili ya Lissu, CHADEMA na wana CHADEMA mpaka muda huu wameshindwa kufikisha millioni 30.

Sasa tizama mahesabu haya kutoka kwangu Mwashambwa Lucas kada kindaki Ndaki wa CCM.

Kama CHADEMA ingekuwa na walau wafuasi na wanachama hai hata laki tano Tuuuu yaani 500,000 na kila mwanachama akachanga walau elfu moja tu maana yake mpaka sasa ingekuwa imepatikana Million mia tano keshi. Yaani

500,000×1000= 500,000,000/=

je pesa hizi zisingetosha kununua gari analolitaka Lissu na chenji kubaki??

Kama CHADEMA ingekuwa na wafuasi Million moja na kila mtu akachanga walau shilingi mia tano maana yake ni kuwa bado Lissu angepata millioni mia tano keshi.

Sasa hao mamilioni ya wanachama ambao CHADEMA huwa inasema inao wengi kuliko wana CCM wapo wapi? Wamejificha wapi? Hawajaona na kusikia kuwa Lissu anahitaji na kuomba walau hata miatano tu? Ikumbukwe kuwa CHADEMA huwa wanasema wana wanachama zaidi ya millioni kumi.

Sasa kama kati ya wanachama zaidi ya milioni kumi wanashindikana kupatikana hata wanachama laki tano tu wa kuchangia elfu moja tu ili kupata million mia tano.je hamuoni kuwa chama hiki kinapika takwimu mara nyingi?

Hata zile kura alizopata Hayati Lowassa mwaka 2015,zilitokana na mgawanyiko uliotoka ndani ya CCM katika upatikanaji wa mgombea Urais. Hata katika ngazi ya ubunge mahali popote pale wanapopata ubunge CHADEMA huwa ni kura za wana CCM wenzetu wanaokuwa wamegawanyika nakupiga kura za hasira kwa upinzani kama sehemu ya kutoridhishwa wakati mwingine na jina linalokuwa limerejeshwa na vikao vya juu.

Lakini kama sisi sote Wana CCM Pamoja na mashabiki wetu na wakereketwa na wanachama kindaki ndanki tukiamua kupigia kura wagombea wetu,nawahakikishia CHADEMA na upinzani wote kuwa hakuna kiti kinachoweza kwenda upinzani kuanzia mwenyekiti wa kitongoji hadi ngazi ya Urais. Upinzani hauwezi kuambulia chochote kile.

Na kwa sasa wale Wana CCM wachache waliokuwa wanapiga kura za hasira kwa upinzani hasa CHADEMA wamejifunza na kujutia makosa yao kwa machozi na maumivu makali sana.wametambua kuwa walikuwa wanajikomesha wenyewe na siyo chama.maana wameona upinzani kazi yao ni kupinga kila kitu na kila jambo pasipo kumpigania mwananchi kwa lolote lile. Kwa hiyo huu mserereko na mteremko waliokuwa wakipata CHADEMA kwa sasa wasahau kabisa kuupata.maana kila mwana CCM amejilia kiapo cha kuipa kura ya ndio CCM Katika kila ngazi ya uchaguzi.

Naweka kalamu yangu chini na kuishia hapa. CHADEMA njooni Nataka tubishane kwa hoja na siyo makelele na matusi. Weka hesabu nami niweke hesabu. Weka takwimu nami nishushe nondo za uhakika. Raha ya CCM Ni kubishana kwa hoja na siyo matusi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hv huko kwenu CCM, hakuna cha maana cha kuongelea? CCM mpo tangu 1960+, sasa hv idadi ya watz ni 60+ milioni,Ila wanachama wenu hawavuki milioni 10!
Sio kila m Tanzania ni mwanachama wachama cha siasa! Fafanueni wizi huu kwanza, acha makelele
 
Attachments

Mkuu hoja yako sio sahihi kwa sababu hizi tatu:

1. Wazo na mchakato wa kununua gari hilo sio la chama.

2. Wazo na ombi hilo hapo juu halijatoka kwa Lisu mwenyewe,

3. Unatumia influence ya mwanachama mmoja ndani ya chama chake, kuhitimisha jumla jumla kuwa huo ndio ukubwa wa chama cha siasa.

Mkuu hoja zako zote toka hili jambo la hiyari na upendo limeanza mpaka sasa zimejikita on wrong premises.

Kwa ufinyu wako wa kupima na kuchanganua jambo badala ya kuona kuwa huo ni ushawishi wa mwanachama mmoja ndani ya chama chake, wewe unachukilia ndio kipimo cha ukubwa wa chama!

Kama kweli wewe ni sehemu ya wachambuzi wa mambo wa chama chako basi kuna shida, wamepigwa!

Mkuu kisaidie chama chako kwa kusimamia ukweli na sio sifa. Penye kuhitaji sifa stahiki sifia kwa haki, penye shida kosoa kwa haki.

Kwamba hujamsikia Lissu akiomba michango mpaka kutoa akaunti ya benki pamoja na namba za simu? Kwamba hujamsikia Lissu akisisitiza anaomba sana kuchangiwa ili apate gari kuweza kuendelea na harakati za kukijenga chama? Kwamba hujaona magroup mbalimbali ya CHADEMA yakihamasishana kuchanga?

Je kwa kauli yako unataka kusema kuwa kwa kuwa wazo la kumchangia gari Lissu halijatokea kwa Mbowe kwa hiyo mmesusa kumchangia Lissu?

Unaweza kuniambia kwenye Join the chain ilipatikana shilingi ngapi? Maana hiyo si ilitangazwa na chama?

Kwenye maporomoko ya Hanang mlipata shilingi ngapi? Maana nako si mliweka namba ya simu na picha ya Mbowe?
 
Hapo wa kulaumiwa ni nani?Maana yake wananchi hawana hela.Kwa nini hwana hela?Uchumi mbovu.Nani kasababisha uchumi mbovu?Serikali na chama chakavu.Andika insha ya maneno laki tatu kutetea hoja.
Nani kasema hawana hela? Umekwenda ukawauliza wakakwambia hawana hela? Au umeamua kuja kupiga porojo zako za ki CHADEMA za kudanganya data?
 
Hv huko kwenu CCM, hakuna cha maana cha kuongelea? CCM mpo tangu 1960+, sasa hv idadi ya watz ni 60+ milioni,Ila wanachama wenu hawavuki milioni 10!
Sio kila m Tanzania ni mwanachama wachama cha siasa! Fafanueni wizi huu kwanza, acha makelele
Acha kurukaruka kama maharage kwenye chungu. Jibu hoja je CHADEMA mna wanachama hai wangapi?
 
Nani kasema hawana hela? Umekwenda ukawauliza wakakwambia hawana hela? Au umeamua kuja kupiga porojo zako za ki CHADEMA za kudanganya data?
Wewe uliwauliza saa ngapi kwamba wana hela?Umeziona?Au unaanzisha nyuzi za..."Ndugu zangu blah blah & blahs CHADEMA fyeee"...?
 
Narudia tena, kura hutolewa bila kutoa hata Senti Moja, hivyo wingi wa wafuasi kipimo chake sio michango ya hiyari. Sasa unaposema umesema kweli sijui unamaanisha nini? Kuna watu kibao ninao wajua hawajamchangia Lisu, lakini ukifika uchaguzi watampa kura.
Embu nijibu jibu fupi hapa je CHADEMA ina wanachama hai wangapi?
 
Nani kasema hawana hela? Umekwenda ukawauliza wakakwambia hawana hela? Au umeamua kuja kupiga porojo zako za ki CHADEMA za kudanganya data?
Alitaka kujua kuwa lingekuwa Tanko la chama ndani YA siku2 tayari lengo lingefikiwa

Kumbukizi, kulipa fine za mahakama, kipindi cha JPM michango total TZS milion 300 zilopatikana ndani YA siku moja Na hili ilikuwa Na Tanko la chama la kuwalipia viongozi Wa CDM
 
Ndiyo hitimisho lako kujua uchumi na kumiliki fedha kwa kila mwananchi?Inawezekana upo darasa la watoto wenye mahitaji maalumu.Si bure.😂😂😂
Uchumi wa Taifa letu unakua vyema kabisa kwa kipimo cha aina yoyote ile cha kiuchumi. Iwe ni katika kipato na nguvu ya uchumi wa mtu mmoja mmoja mpaka Uchumi wa nchi. Ripoti mbalimbali zimethibitisha jambo hilo. Ongezeko la mapato ni ishara pia kuwa shughuli za. Kiuchumi zinaendelea kuongezeka na kufanya vizuri mitaaani. Angalia hata takwimu za TIC yaani kituo cha uwekezaji Tanzania pamoja na usajili wa biashara mpya unavyoongezeka.
 
Umeandika matakataka.Kidunia Tanzania ni ya ngapi kwa umasikini?
 
Mambo ya chadema waachie wenyewe! Ukiona chadema ni nzuri na unahitaji mabadiliko ktk hiko chama basi chukua kadi kuwa mwanachama

Tulia na chama chako jenga chama chako, kosoa chama chako, kijenge chama chako!

Usingoje makonda aje akosoe ndio nawe utokeshimoni...!

Usingoje mwenyekiti wako aseme ndio nawe useme! Wakati huo akiwa kimya unamsifia ata kama amekosea!

Jenga chama chako, jenga taifa lako!

Chama chako kipo madarakani miaka nenda rejea, kina mapungufu kibao! Paza sauti kujenga nchi na chama

Kemea watendaji wazembe!

******
Wewe atakuwa mtendaji wanyumba kumi hakuna utafanya, ata ile kazi ya Anuani za makazi sijui kama ulifanya kwa ufanisi kwa namna unavyoishi katika hii platform!
Asiposikia na hili basi kweli huyu atakua masaaburi
 
Back
Top Bottom