TBC ni TV ya waislam na wakristo wakatoliki?

Kwa hio wanazidi idadi ya Waislamu na Wakatoliki Nchi nzima? 💩
Idadi si hoja,hoja ni kwa nini malinya umma inatumika kuhubiri Imani Fulani pekee,ni aidha iache au ihubiri Hadi Imani za kihindu ambayo ni sehemu ya jamii ya nchi hii
 
Wanajitahidi kutangaza labda haya mapya ya kilokole na akina Mwamposya na Gwajima, hayo TBC sijasikia wakiyatangaza.
 
Hapo kwenye Uislam sema Suni maana Shia, Ibadi, Ahmadiya, Bohora, Ismailia, n.k hawana chao TBC
 
Idadi si hoja,hoja ni kwa nini malinya umma inatumika kuhubiri Imani Fulani pekee,ni aidha iache au ihubiri Hadi Imani za kihindu ambayo ni sehemu ya jamii ya nchi hii
Ndio ulivyotumwa na Mchungaji wako?
 
Ijumaa ni waislam ,Juma mosi ni wasabato,Juma pili ni Rc sababu ndio mama yao wengine ni watoto
 
Wananchi waliosimika hii siyo akina Gwajima,Mwamposa na makanisa yao ya kihuni huni bali ni watu ambao utawala wa dini zao ulisimikwa na Mungu mwenyewe.

Kama umkristo huna sababu ya kubeza wala kudharau madhehebu mwngine yanayo mtangaza kristo,au mwenzetu una hatamiliki ya kristo ?
 
Dini na Madhehebu yote Nchini yanatakiwa kupewa Airtime bila ubaguzi na National Television ya Taifa hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine.
 
Ni ujinga tu wanajitia kubalance mambo
 
Dini na Madhehebu yote Nchini yanatakiwa kupewa Airtime bila ubaguzi na National Television ya Taifa hakuna mwenye haki zaidi ya mwingine.
Tusome wakiyapa air time madhebu yote Kuanzia walokole mpaka ma budda itachukua muda gani,kutakua na taarifa ya habari kweli na ziara mbalimbali za kiserikali zinazorushwaga mubashara?
 
Shida walokole Wana fujo za kupredent eti wananena kwa lugha. Sasa tbc ni chombo Cha kuangalia watu wastaarabu siyo fujo. Hii tv inaangaliwa mpaka na foreigners Sasa fujo zinawakera. Hizi vurugu mnazofanya halafu mnamsingia mungu eti m mnanena maneno yake ifike mda zikome ili na nyie muwe na access na tbc. Hiki chomba makini siyo Cha kuinvite kelele za ashakabata mara pwapwapwa mara yeyeyeye. Sasa hizi si lugha za Lucifer?
 
Serikali ya Tanzania haina dini ila raia wake wana dini wanaozifuata. Wakristo na Waislamu ndio dini mbili kubwa nchini Tanzania. Televisheni ya TBC ikitaka kupata watazamaji lazima iwarubuni wafuasi wa hizi dini mbili kubwa. Huo ni mwendo wa biashara na kuwa na sauti katika jamii. Watanzania wengi wanamuogopa Mungu na mpaka kizazi hiki misikiti na makanisa makubwa bado yanajengwa, nasikia sehemu nyingine za dunia hasa ulaya - hakuna ujenzi mpya wa makanisa!
 
Hivi huo muda wa kuangalia hayo maudhui kwa masaa 24 kila siku na kugundua hao TBC ni wabaguzi unautoa wapi!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…