TCRA, BASATA zafungia video ya wimbo wa Diamond Platnumz ft Zuchu - "Watasubiri Sana"

Hii ni mpya aiseee, kwahiyo huu ndio ukakasi wanao sema kumbe? vip wakati Masanja kujifanya wanawake kuimba nyimbo za kina Christina Shusho ? Basata kuna tatizo
 
Wangeigiza madrasa ingekuwa poa, kulingana na imani yao, huku kwingine sio sawa,
Kwahiyo Wakristo msikitini au sehemu za kiislamu hawatakiwi kuzionyesha kwenye nyimbo zao hata kama kuna maudhui hayo? mimi nafikiri labda wangefanya jambo baya kwenye hilo kanisa ingekuwa tatizo
 
Nisamehewe!!!

But in short,imani uliyoitaja hapa msingi wake mkuu ni unafiki,nazini lakini nguruwe haramu,naiba ila kunywa pombe haramu,nasali lakini kutukana na kuita majina ya kuudhi asiyefanana na mimi siyo haramu.
sasa unataka kila dhambi afanye ! kila binadamu ajitahidi kwa uwezo wake, kwani ukisikia kiongozi wadini ndio unafikiri hana dhambi? wewe jitahidi kwa uwezo wako kufanya mema na kuacha dhambi
 
Maisha ya milele wewe unaona vigori 72 ni wengi? mbona wachache hao ilitakiwa hata vigori 10000 angalau, wewe kinacho kuuma ni kuwa ukifika huko mbinguni kazi yako ni kuimba tu mpaka koo likukauke, sasa unaona wivu wengine kwenda kuenjoy life, kijana kupanga ni kuchagua
 
Duuh...! Sijui Diamond alikufanya nini wewe mama?. Maana sio kumdis kwa hivyo. Hebu weka wazi hapa kuna nini kati yako na huyu dogo?. Au ndio yale yale?
 
Mkuu lilikuwa wazo langu ndo mana nikatanguliza samahani ila pia nayaheshimu mawazo yako japo hukuweza kuniambia kwanini watu wanatofautisha dhambi.
 
Huyo diamond ndo anatia kinyaa kujifanya muislamu hanywi pombe ila anaimba zinaa
Hata wewe yapo unayafanya mabaya japo unajidai ni mtu wa imani fulani, hata Diamomd binadamu sio Mungu yule, muhimu hajawai kusema kuwa zinaa sio dhambi
 
Aiseee hizi dini ni majanga kabisa alie zileta ametuweza
 
Sikiliza maudhui ya wimbo, Zuchu anapigiwa simu na anatoka kanisani kwenye mazoezi ya kwaya ili kwenda kudinywa/kuzini na Mondi kwani ndani ya wimbo hawaonyeshi kwamba ni wana ndoa!
 
Kwani wimbo umefungiwa ktk mtandao gani!?
Mbn YouTube bado upo!!
 
Yaani sababu hiyo tu?
 
Hii nchi ina viongozi vilaza sana,mi ni mkristo tena RC,nimejaribu kurudia ile sehemu sioni tatizo kabisaaaa halaf hata kama kuna tatizo sawa,mbona video inaonyesha Zuchu alitoka kanisani baada ya kwaya kumalizika
Nakufahamu wewe unaitwa Juma.
 
Habari wakuu!

BASATA kwa kushirikiana na msanii Diamomd wameamua kuja na kiki ili kuhamisha mjadala wa bei za mafuta & mfumuko wa bei wa bidhaa nchini.

Kwa hali ya kawaida wimbo uliyofungiwa umekaa muda gani hadi uje ufungiwe leo?

Acheni kutengeneza kiki za kipumbavu BASATA & Diamond.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…