Team “Kataa ndoa” wapuuzwe, hawana maadili, ndoa iheshimiwe na watu wote

Hakika ndoa iheshimiwe na watu wote.

Yule anaetaka kuingia kwenye ndoa akumbuke kuwa " Ndoa ni agano la milele baina ya mwanadamu na mwenzie pamoja na M/Mungu likishuhudiwa na ndugu, jamaa na marafiki na sio mkataba".

Hivyo wakati wa kuingia kwenye ndoa inakupaswa ujitafakari ( ukubaliane na yote) kabla ya kutia mguu.
 
Amina mkuu, naona watu makini bado wapo JF
 
Asante DJ kwa kunileta na ngoma ya ""Tunagonga sanaa wake zenu""

Ndugu mleta mada naomba nishike maiki halafu nakujibu kwa paragraph zako za ajaaabu ulizopost ....

1. Nani amekwambia anaogopa familia, Kwani nini maana ya Familia, Hebu rudia "Types of families" kwenye elimu yetu ya Form two.

Mimi binafsi nina familia, ila SINA MKE na wala SIHITAJI MKE.

2. Kuoa hawana uhusiano wowote na uongozi.
Kuna wateuliwa wa raisi kibaoo hawana ndoa.
Kuna matajiri wana miliki ""multiple businesses"" wanaziendesha biashara zao balaa ila hawana ndoa.
Nafikiri uliposema "Sinza" umemaanisha wakataa ndoa ni wanaume wa hovyo, sasa iko hivi, mimi binafsi nina maisha yangu safi tu na naheshimika tu vizurii serikalini ila ndio hivyo "In JF we are ghosts" siwezi reveal ID yangu.

3. Narudia tena, sisi ni wanaume wa heshima tu.
Na ndoa haina uhusiano wowote na kutomb(a)

4. Kwahiyo wewe huoni, mnavyogongewa, mnavyo dhurumiwa, mnavyofokewa na wanawake na menginee kibaoo. MNAFIKIRI HATUYAONI BRAZA MNAYOFANYIWA NA WAKE ZENU??

5. Ushasema Mungu aliagiza "Kuzaa na kuongezeka" ila sio kuoana.

6. Narudia tena kutomb(a) hakuna uhusiano wowote na ndoa.
Kama ni umalaya, waume za watu ni malaya, wake za watu ni malaya.
Kifupi malaya ni malaya tu.

CC.
Katibu dronedrake - Aione kwenye jalada

Nakala kwa:-
Wajumbe wote wa CMT yetu ya chama.

Wenu, Mwenyekiti.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kwani wanawake mnataka kuongozwa siku hizi.
 
Karibu Mr Liverpool ,sasa hiyo one parent family unaiita ni familia?? Mama ya watoto wako yuko wapi au uliwazaa peke yako?

Ni Ego /uhuni tu, lakini kuna wakati ukifika lazima utulie na mke wako.

Kuhusu kugongewa ndiyo uache kuoa? Siyo kila mwanamke ni Malaya mkuu!! Mwanaume anazikabili changamoto head on Siyo kuzikimbia.

Utafurahi kiasi gani mtoto wako wa kike adate na team KATAA NDOA??
 
Wanawake wapo wengi ila Wanawake wa kuoa wapo wachache sana
Tafuta na umshirikishe Mungu, Tatizo wengi humu wanatafuta mke Kitambaa cheupe /wavuvi kempu /warehouse /kidimbwi /mtandaoni halafu yakiwakuta wanalia
 
Biashara nyingi kutofanikiwa inapaswa kuwa sababu ya msingi watu kutofanya Biashara moja kwa moja ? kutofanikiwa biashara inawezekana mtu hakuwa na mtaji wa kutosha , hakusoma vizuri mazingira au nature ya biashara anayotaka kuanzisha , Kutokuwa siriaz na kufuata misingi ya biashara nk .

Ndoa nayo ina misingi yake katika kuchangua mwenza, maisha yake , utatutuzi wa migogoro nk hivyo mtu anapokurupuka kuingia kichwa kichwa lazima ataniona ndoa chungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…