Siku chache zilizopita nilikua napitia mtandao mmoja wa kijamii nikaona post jamaa mmoja anauza simu , sasa ameandika bei yake pale kaweka na taarifa za ile simu.
Nilicheka sana , maana kwa uhalisia maelezo ya ile simu muda wake wa matumizi na bei havikua sawa na bei halisi ya simu ile naifahamu hivyo bei yake kuwa ndogo ilikuwa ni red flag ya kwanza kwangu ikabidi niwe mdadisi nipitie reviews za watu.
Kwanza katika zile reviews watu zaidi ya 10 waliingia katika website ya ile kampuni na kuingiza IMEI za simu ile ambayo jamaa aliweka na wakatuma screenshot kuonyesha kampuni haina simu ya aina ile katika database zake hivyo ni fake 100% , wa kutukana na kucheka walikuwepo pia hadi hapo jamaa alikua amewekwa kwenye kona.
Nikatafakari na kukumbuka miaka 10+ nyuma jinsi watanzania walivyokuwa wanatapeliwa kwa kutoajua vitu vingi tu japo ni vidogo basi wangekuwa wametapeliwa wengi siku hiyo kwa kununua simu feki kwa bei ya kutisha.
Kwanini nimeleta hii habari niliyoona huko, jibu ni kuwa watanzania wa sasa sio wajinga wanajitambua na wanajua wapi wapate taarifa sahihi na wapi waache kubeba taarifa za kupikwa.
Watanzania wa sasa sio wale wa kusubiri kusikiliza RTD jioni kujua kimejiri nini siku hiyo.
Watanzania wanamjua adui yao, adu8 wa watanzania sio TEC , sio BAKWATA, sio Buddha, sio wapagani .
Watanzania wanajua sababu zilizowapeleka barabarani 100% .
Watanzania wanajua anayeteka , anayeua , aliye nyuma ya kesi za kubumba kuonea watu.
Watanzania wanajua mahali walipozikwa ndugu zao katika makaburi ya halaiki baada ya kuuawawa kinyama na polisi.
Watanzania kwa sasa wanajua deni la taifa ni nini, watanzania wa sasa wanajua mafisadi na majizi wote hata nchi walipoficha pesa.
Watanzania wanajua lile genge la wastaafu lilioitwa tume ya uchubguzi liko kama picha tu na ndio maana walijua na wanajua wapi wanatakiwa kupeleka ushahidi kupata haki za ndugu zao.
Mtandao huu ni wanne mmewafungia watanzania kuanzia X, Clubhouse, Tiktok na sasa JF , kwa kisingizio haina maadili ila bado waliofungia na vidampa wao hamkauki humu ila yote hayo watanzania wanawangalia tu na wanaujua ukweli maana sio wajinga tena kama zamani.
Watanzania wanajua kwanini wanashangilia misiba ya wabunge, mawaziri , polisi na watumishi wengine wa vyombo va dola.
Watanzania wanatekwa mnakuja mnasema wamejiteka .
Watanzania mnawatishia maisha wanatafuta asylum mnasema wamelipwa na wanalelewa na wazungu.
Watanzania wanajua nini cha kufanya baada ya kujisahihisha waliposhindwa October 29.
Shupazeni shingo kuna siku inakuja tena watanzania watawaambia TUNAJUA tunachokitaka.
Idadi ya wajinga wakati katika hii mbovu inapitishwa 1977 ilikua kubwa ndio maana haikuonekana hatari yoyote wala ubaya wake kwa wakati huo ila kwa sasa idadi imeshapungua na kuelekea ukingoni basi kuna siku mtaelewa nini watanzania wanakitaka kulingana na mahitaji ya wakati uliopo.
Watanzania sio wajinga kama mnavyodhani.