tuko duniani kwa kazi maalum. Muda ukifika wa kuondoka tunaondoka, hakuna cha kujilinda. Ukiwa na mahusiano mazuri na Muumba ukikaribia kuondoka unajua.
Polepole alikuwa mtu wa rohoni ! fuatilia akiwa anaichambua Biblia utajua.
hofu ya kifo huleta utumwa. Ebr 2:14-15
Waebrania 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
¹⁵ awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa."