Tetesi: Tetesi za usajili wa dirisha kubwa ligi kuu Tanzania bara 2025/2026

Tetesi: Tetesi za usajili wa dirisha kubwa ligi kuu Tanzania bara 2025/2026

Nenda kamsikilize Zaka za kazi, utajiridhisha.
Hata mimi lile swala la mkataba uliopo baina ya Yanga na Azam kuhusu kuuzwa kwa Feisal nilidhani viongozi wetu (wa yanga) wanatupanga tu.
Ila nilipo msikiliza kwa makini Zaka za kazi ndipo nikaamini maneno ya viongozi wa Yanga.

Amini na kwambia hakuna club ya Tanzania inayoweze kulipa Billion 2 kwa mchezaji mzawa.

Kama Simba munayaweza tuonyesheni.
feisal akiuzwa bongo yanga ipate 1B vipi kama atauzwa kwa 800 million?. usikubali kufanywa kichaa, hakuna terms za kibugusa kama hizo.
 
Hoja sio "nguvu kubwa kwenye assist na magoli"

Hapa hoja ni kweli Aucho aliwahi kkumaliza msimu paspokuwa na assist wala goli? Hapa tunataka kufanya tathmini ya msimu mmoja tu sio mechi 55 ambazo Conte amecheza.
Kwani Yanga waliwahi kukuambia wamemsajili huyo mchezaji ili awasaidie kwenye kufunga magoli na kutoa assist? Mbona unapenda sana ubishi usio na ulazima wowote ule!
 
Biashara za matajiri katu kapuku hawezi jua. Ndio maana Masanzu anasema Sowah katolewa bure. Tumsimlaumu kwa sababu inawezekana matajiri wamelipana juu kwa juu wenyewe kwa wenyewe au kupitia makampuni yao halafu yeye Masanzu anasubiri aone muamala kwenye benki akaunti ya timu ya Singida. Mwambieni anajichosha bure mitandaoni na redioni anakokesha akipiga kelele na kushupaza shingo kuwa Sowah katolewa bure.

Vivyo hivyo kwenye suala la Feitoto lolote linaweza kutokea kwani sasa hivi imebaki mazungumzo kati ya matajiri wawili. Huko sio Zaka Zakazi, Hashim Ibwe au Ahmed Ally wanaoruhisiwa hata kupita karibu wakati mazungumzo yanaendelea. Kwa hiyo hao wasemaji wote wa Simba na Azam wasimalize maneno waweke akiba ya maneno ili likija kutokea la kutokea wasibaki na aibu. Tuwape muda matajiri wazungumze wenyewe watamalizana kwa aidha Fei kwenda Simba au kubaki Azam. Hakuna linaloshindikana chini ya jua ndio maana wiki mbili tu zilizopita mtu angeanzisha uzi hapa kusema Sowah anaenda Simba angetukanwa kila aina ya tusi na watu wote hapa jamvini wa Yanga na hata wa Simba.

Ni mtizamo tu
 
bilioni mbili mbona nyingi mno hizo
Ndio mana nimemuuliza au nauliza alieona mkataba halali wa huyo mchezaji aupige picha aulete hapa ili tusome kipengele Cha bilioni 2 wasiniletee habari za yule media journalist puppet wa yanga...Hans na genge lake ..nikiona tu huo mkataba na kusoma hiko kipengele Cha bilioni 2, ndio niulize Sasa kua kwanini anadhani timu inayomtaka haiwezi kutoa hizo bilioni 2.
 
Naipenda sana Simba lakini ni ukweli mchungu unaousema... kwa mateso tunayopitia kila msimu mpaka nione kombe ndio nitaamini kama tumesajili vizuri. Karibia ni msimu wa tatu sasa Mashabiki wa simba tunafurahia wakati wa usajili lakini mambo yanageuka mwisho wa msimu.
Kwahyo una guarantee Gani usajili wa uto kwa hao wachezaji wote kina ecua, kouma n .k utalipa?
 
Kupitia vyanzo vya Sofascore, FBref, na FootyStats nimejaribu kuangalia stats za Busquets katika mechi 27 yani nusu ya mechi alizocheza Balla Conte. Hapa sijataka kwenda mechi 55 kufanya uwiano sawa.

MechiTareheMashindanoAssist
vs D.C. UnitedMay 18MLS1
vs Atlanta UnitedMay 29MLS1
vs MonterreyApr 11CONCACAF Champions1

Tafiti zinaonesha Busquets hakupata goli lolote kwenye mechi 27 ila alifanikiwa kupata assist 3.

Niliporudi kwa Ngolo Kante naye kwenye mechi 27 alikuwa na goli 4 pamoja na assist 3

Mechi Ambazo Alipata Magoli​

  • vs Al-Riyadh – 1 goli
  • vs Al-Ettifaq – 1 goli
  • vs Al-Qadsiah – 1 goli
  • vs Al-Orobah – 1 goli

Mechi Ambazo Alitoa Assist​

  • vs Al Kholood – 1 assist
  • vs Al-Hilal – 1 assist
  • vs Belgium (UEFA Nations League) – 1 assist
Kwa hiyo bado hujani convince nikashawishika na hoja zako kufafanua kwanini kitendo cha mechi 55 kwa mchezaji wa ndani kutokuwa na goli wala assist isiwe uzembe?
Hao jamaa wanavyotumia nguvu kumtetea jamaa yao....😂
 
Kwa wasiojua biashara ya mpira wanaona eti Fei kuthaminishwa kwa 1B au hata 2B kabisa sio sawa kwa kuwa ni mchezaji mzawa. Hizo ni fikra potofu kabisa kwani kuna wachezaji wa kawaida sana wamewahi kuja kucheza hapa bongo kutoka nje wakiwa na viwango vya hovyo kabisa. Ukija kuhesabu signing fee, mshahara wa msimu mmoja jumlisha kuvunjiwa mkataba unakuta kwa msimu mmoja mchezaji wa nje kibonde kabisa amekunja zaidi ya hiyo 1B.

Kama ningekuwa MO huyo Fei hata kama ni zaidi ya 1B ningetoa kwa kushirikiana na mdhamini wa Simba kits kwa makubaliano maalum. Kwani kitendo cha Fei kusaini Simba ukiwa na timu nzuri ya marketing 20% - 40% ya hiyo pesa inarudi. Watu wengi mpaka leo hawajui kwa nini Hersi alijitolea kumchukua Chama pamoja na uzee wake kwani zaidi ya uchezaji uwanjani kubwa zaidi kwake ni suala la kibiashara.
 
Hata Masanza alikua anakaza Sowah hawezi kununuliwa hapa bongo, mwisho wa siku wamekuja na swaga za kua ameenda simba kwa makubaliano maalumu. Soka letu kivyetu vyetu
Mbona kwenye maelezo ya ile barua inaonesha huyo Sowah amesajiliwa simba kwa mkataba/makubaliano maalum!! Imekaaje hii!!
 
Back
Top Bottom