Teuzi za Rais Samia zina upendeleo?

Hajasema waislamu lakini, yeye amesema udini.. Umekimbilia kwenye point haraka sana
Ficha ujinga wako.Topic yote kuhusu udini inajulikana anamaanisha nini.Au upo so naive hujui anachomaanisha mleta mada?.Kuna ubudha au uhindu kwenye siasa za Nchi hii kwa walio na tabia za kulalama?
 
Waombaji waliofaulu Usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo Unguja – Zanzibar (Mazizini) katika Jengo la Sheria Ghorofa ya 3
Listi imejaa waislamu, lakini je uombaji wa hizo kazi wewe hudhani kuwa Upande wa Zanziba labda waombaji walikuwa ni wakazi wa huko pekee?.. Je population ya huko unadhani domition ya Muslims ni %ge ngapi. Waliozaliwa kusoma na kuishi huko je?.. Je kuna Christians na dini zingine waliomba na wana vigezo. Kama waliomba na wana vigezo hapo itakuwa ni shida kama lah, sishangai..

Tupe na mkeka wa huku Bara mkuu
 
Bora mzee Mohamed umekuja na real data. Mim kila nikiona nyuz humu jamaa wanalia ilihal hizo data bado hujagusa kwa watumish tu kawaida.wanalijua hilo na hata Mh analijua hilo.pita ukute kwaya zinavoimba maofisin hata muda wa kaz
 
Tuende na takwimu kwa kujiuliza maswali haya.

Ni awamu gani ya Rais ambae Baraza lake la mawaziri halikujaa mawaziri wa dini moja

Idadi sasa ikoje ukilinganisha na marais waliofanya uwino wa baraza la mawaziri.
Wakikujibu ni tag.
 
Acha Udini wewe yani katika majina yote unachoona ni dini tu. Ukimaliza udini utakuja ukanda ukimaliza ukanda utakuja jinsia ukimaliza jinsia utakuja urefu na ufupi then mweupe na mweusi then kabila. Mtu mbaguzi hua hatakosa cha kukosoa. Baraza halina shida yoyote sana sana wananchi tunataka uwajibikaji.

Achana na UDINI kwani unasukumwa na ubaguzi.
 
Wewe ndo mdini namba moja, why uchambue viongozi Kwa dini zao?

CCM mnalipeleka wapi Taifa?

Awamu ya 5 na 6 wote ni CCM,

Utaifa na Uzalendo kwanza.

Maamuzi ya viongozi yaheshimiwe.

Tuangalie uwezo wao, Si dini zao.
 
HII NI KWA UPANDE WA ZANZIBAR , AM SURE .
WALIOPATA TKEA BARA HUWA WANAJIBIWA HUKU BARA NA KUNA SEHEMU WANAKWENDA KURIPOTI
 
Hata sasa hivi teuzi za Samia Wakristo ni wengi kuliko Waislamu, sema hawa watu hata takwimu hawaangalii na mijadala yao ni hasira kuliko facts
 
HAYA FANYA HESABU UTUPE %GE

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO​

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MHE. DKT. HUSSEIN ALI MWINYI​

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA - Jimbo la Ruangwa - Lindi​

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MHE. KAPT GEORGE HURUMA MKUCHIKA - Jimbo la Newala Mtwara​

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum)

MHE. JENISTA J. MHAGAMA - Jimbo la Peramiho Ruvuma​

Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA - Jimbo la Karagwe Kagera​

Waziri wa Ulinzi

MHE. ANGELLAH J. KAIRUKI - Wa kuteuliwa​

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

MHE. SELEMAN S. JAFO - Jimbo la Kisarawe Pwani​

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO - Jimbo la Kasulu Mjini Kigoma​

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)

MHE. GEORGE B. M. SIMBACHAWENE - Jimbo la Kibakwe Dodoma​

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

MHE. PROF. MAKAME M. MBARAWA - Jimbo la Mkoani Pemba Kusini​

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

MHE. UMMY A. MWALIMU - Tanga Mjini Tanga​

Waziri wa Afya

MHE. DKT. MWIGULU N. MADELU - Iramba Magharibi Singida​

Waziri wa Fedha na Mipango

MHE. MHANDISI HAMAD Y. MASAUNI - Jimbo la Kikwajuni Mjini Magharibi​

Waziri wa Mambo ya Ndani

MHE. DKT. STERGOMENA LAWRENCE TAX - Kuteuliwa​

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

MHE. HUSSEIN BASHE - Jimbo la Nzega Mjini Tabora​

Waziri wa Kilimo

Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko -Jimbo la Bukombe Geita​

Minister Of Minerals

MHE. PROF. ADOLF. F. MKENDA - Jimbo la Rombo Kilimanjaro​

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. NAPE M. NNAUYE - Jimbo la Mtama Lindi​

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

MHE. JANUARI Y. MAKAMBA - Jimbo la Bumbuli Tanga​

Waziri wa Nishati

Mhe. Dkt. Angeline Sylvester Lubala Mabula - Jimbo la Ilemela Mwanza​

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

MHE. DKT. DAMS D. NDUMBARO - Jimbo la Songea Mjini Ruvuma​

Waziri wa Sheria na Katiba

MHE. DKT. DOROTHY O. GWAJIMA - Kuteuliwa​

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. DKT. ASHATU K. KIJAJI - Jimbo la Kondoa Dodoma​

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara

MHE. JUMA H. AWESO - Jimbo la Pangani Tanga​

Waziri wa Maji

MHE. DKT. PINDI H. CHANA - Viti maalumu​

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - Jimbo la Rufiji Pwani​

Waziri wa Maliasili na Utalii

JF Member Tui
 
Bara 70% wakristo mkuu
 
Ficha ujinga wako.Topic yote kuhusu udini inajulikana anamaanisha nini.Au upo so naive hujui anachomaanisha mleta mada?.Kuna ubudha au uhindu kwenye siasa za Nchi hii kwa walio na tabia za kulalama?
Sasa mbona Baraza lina wakristo wengi kuliko waislamu.. Huoni wewe umekurupuka bila kujua alimaanisha dini gani.

Umeweka ujuaji mkuu
 
Wakati wa John wala hamkusema chochote japo baraza lilijaa Wakristo utafikiri lilikuwa baraza la maaskofu.
 
Bara 70% wakristo mkuu
So ni kawaida,
Halafu sidhani kama Ajira tuna haja ya kuangalia %ge ya waislamu na wakristo. Serikali haiko hivyo bali sisi na akili zetu tunaona hivyo.
Serikali haifuatilii udini, MOSTLY INAFUATA SANA UKADA
 
Akina John wakijaa kwenye mkeka hakuna shida ila ikitokea kuna akina John 20 na akina Ali 10 tayari kuna udini. Mmezoea kuwa peke yenu akiteuliwa Muislam mmoja tu povu kama lote. Hii nchi si yenu peke yenu.
Kaka hakuna mahali nimesema lazima baraza liwe la dini flani...ila tunachotaka kuwe na balance 50% kwa 50%
 
Kwaiyo na yeye Mama ameamua kufuata upuuzi wa JPM!
Mama hakufuata upuuzi bali anajaribu kubalance. Haiwezekani nchi yenye baraza la mawaziri 30 uteuwe waislam wanne tu kana kwamba wao hawakusoma au nchi nzima wamekosekana waislam hata 10 wa sifa za kiuwaziri. Hii iliwaumiza wengi mno ila hawakuwa na la kufanya katika nchi yao kwa vile katiba inampa mteuwaji ridhaa ya kuchagua yoyote.

Anachokifanya mama ni kubalance ili kutengeneza serikali yenye utaifa. Tofauti na kipindi kile ilikuwa ukienda Tanesco utafikiri uko kanisani, ilikuwa ukienda bandari same story, wizara ya elimu ndo usiseme watoto wanaletewa hadi biblia mashuleni.

So acha mama ayaponye majeraha ili nchi iwe na sura ya kitaifa sio sura ya vatican kama tuko roma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…