Teuzi za Rais Samia zina upendeleo?

kama ambavyo kunatakiwa uwe na weledi katika kuitazamia nchi kama inafuata misingi ya demokrasia, ni vema pia haya masuala ya udini, ukabila, jinsia idadi ya wanawake na wanaume katika uongozi yazingatiwe kwa mapana yake.
 
Tatizo mnaishi kwa hao wanaoteuliwa na hamjui madhara ya uteuzi tunaoupigia kelele....Kila kitu unaletewa tu nyumbani kama umeolewa vile hujui mtaani kugumu kiaje.
Wewe unasumbuliwa na udini ndiyo maana kutwa kazi yenu kuwasema viongozi Waislam humu mitandaoni. Enzi za Mwendazake hatukuwahi kusikia hoja za udini kwenye teuzi. Chuki, hasadi na roho mbaya dhidi ya Waislam ndivyo vinavyowatafuna. Mmezoea nyie tu ndiyo mpate akipata Muislam kosa. Hii nchi ni yetu sote kaa kwa kutulia.
 
sikuhizi vilemba vingi, hata ambao waliokuwa hawavai imewabidi tu wapite na huu upepo. mpaka kuna awards
 
Kila akiingia Rais kutoka Unguja na Pwani swala Udini katika teuzi huwa linajitokeza. Sasa limeongezeka jinsia na Uzanzibari. Angalia wabunge wote kutoka mkoa wa Pwani ni mawaziri!
Mama Maridhiano!
 

Ajaze waislamu atakavyo, wakati dhalimu anaharibu mambo mliona yuko sawa. Wakati anachagua wakristo na watu wa kanda ya ziwa mlisema kwani sio watanzania? Sasa mkae kwa kutulia maana kibao kimegeuka.
 
Wewe ulijuaje kama anashauriwa na si utashi wake
 
Thubutu.Hataleta takwimu kamwe.Anaendeshwa na ubaguzi na chuki .Ukiwa na chuki unakuwa na matatizo ya akili hivyo asamehewe.
 

Kati ya vitu ambavyo TANU iliweza ni pamoja na kudevide and kurule.
Hapa namaanisha kuweka chama kimoja chenye nguvu na mabranches yake mengine (upinzani) ili ionekane kuna demokrasia.

Hadi siku moja watu waamke kutoka usingizini na kutengeneza chama kimoja cha upinzani chenye nguvu na kuunganisha watu wote wanaotaka haki na usawa na maendeleo kwa watanzania na sio wachumia juani, hapo mambo yatabadilika.

Otherwise mtalalamika kila siku na Rais huyu atafanya hivi na ajae na mwingine kwasababu sheria inamruhusu na kupitiliza, walioko chini yake wengi hawajali maslahi ya watu bali wao na familia zao na madaraka.

Tunaongea sana uthubutu hamna, hatukosoani kwa hekima na kwa uthubutu, wakosoaji wanatula visogo, nani atatutoa jangwani?
 
Akiteuliwa muislamu mmoja ndani ya teuzi zenye wakiristo watatu, bado kuna baadhi ya Wakiristo wanaona hata hiyo haipaswi kuwa. Wanataka asiteuliwe muislamu hata mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…