Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

holoholo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2023
Posts
1,859
Reaction score
2,986
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha leo Machi 8, 2025, ilipitia shauri la klabu ya Simba kuzuiliwa kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC (Young Africans SC vs Simba SC) uliopangwa kufanyika kwenye uwanja huo leo kuanzia saa 1:15 usiku.

Soma Pia: Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Katika shauri hilo, klabu ya Simba iliandika barua kwa Bodi ya Ligi kueleza kususu tukio tajwa hapo juu, huku pia ikieleza nia yao ya kuto shiriki mchezo huo kwa sababu wamezuiliwa kutumia haki yao ya kikanuni kama ilivyoai.
Snapinsta.app_483196805_18059686901501660_1758982673497521479_n_1080.jpeg
 
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha leo Machi 8, 2025, ilipitia shauri la klabu ya Simba kuzuiliwa kuingia kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC (Young Africans SC vs Simba SC) uliopangwa kufanyika kwenye uwanja huo leo kuanzia saa 1:15 usiku.

Soma Pia: Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Katika shauri hilo, klabu ya Simba iliandika barua kwa Bodi ya Ligi kueleza kususu tukio tajwa hapo juu, huku pia ikieleza nia yao ya kuto shiriki mchezo huo kwa sababu wamezuiliwa kutumia haki yao ya kikanuni kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni ya 17:45 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Screenshot_20250308-135808.png
 
Hii mechi haitakiwi kuahirishwa bali isichezwe kabisa na adhabu kali itolewe kwa waliozuia taratibu za kawaida kabisa za mchezo ili kukomesha huu uhuni.

Siku nyingine timu ikijiona haiko tayari kucheza mechi husika itajiamulia tu kufanya uhuni kama huu ikijua italipa faini na mechi kuahirishwa.
 
Kwa hio isichezwe arafu iweje? nyie ndio wale wajinga wajinga
 
Nimemaliza kusoma barua nikaishia kucheka sana na kujiuliza maswali fikirishi kua yanga ni nani nchi hii? Viongozi Gani wa kisiasa na kitimu wako nyuma ya hili la kua na uwezo wa kuzuia watu wasitumie uwanja ..tena uwanja wa serikali..yanga ni nani nchi hii...ama kweli leo ndio nimejua maana halisi ya ubaya ubwela. By the way msicheze na Tajiri Mo dewji. Watu wamewekeza pesa zao kwenye timu, Simba timu kubwa inawakilisha nchi halafu muwafanyie UHUNI NA DHARAU kwa kutowaheshimu.
 
Back
Top Bottom