Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Asante kwa taarifa

Screenshot_20250308_140744_Samsung Internet.jpg
 
Huwa Simba wanao huu utaratibu wa kufanya mazoezi wakiwa ugenini kabla ya mechi katika uwanja husika!? Au ndio kutafutiana sababu tu😁
Nachokiona hapa kwa wote, ni kuwa na imani za kishirikina badala a kuamini katika mazoezi, mbinu na matayarisho..!
Yanga huwa wanadai wao ni wazee wa kanuni ndio maana waligomea mechi iliyosogezwa mbele masaa mawili,leo wamekumbushwa kufuata kanuni
 
TFF kinabidi kiwe ni chombo huru ambacho kinaweza kusimamia sheria bila kuingiliwa na mamlaka za kiserikali na vilevile kisiwe na mlengo wa kuwa na upande wowote kwenye hizi timu mbili.

Haiwezekani Club iwe na confidence ya kuvunja sheria kwakuona udhaifu wa kanuni kuwa adhabu ya faini ambayo atapata haiendi kumuathiri chochote.

Sasa inapotokea mazingira kama haya kwenye mechi ambayo inaweza kwenda kuamua hatma ya nani kuwa Bingwa.

Huwezi kuishinikiza timu iliyoathirika na uonevu uliofanyika kinyume na sheria kuwa ishiriki mechi kwasababu hao waliovunja sheria watalipishwa faini ambayo kimsingi ndio hiyo laki 5 hadi milioni.
 
Simba wanahangaika tu, wamehairisha kipigo ila kipigo kijacho ni kikubwa zaidi ni Swala la muda tu.

Waliambiwa wafanye usajili wakawa wana fanya mchezo aya ndio matokeo yake.
Usiku wa deni hau kawii kucha.
 
Hii mechi haitakiwi kuahirishwa bali isichezwe kabisa na adhabu kali itolewe kwa waliozuia taratibu za kawaida kabisa za mchezo ili kukomesha huu uhuni.

Siku nyingine timu ikijiona haiko tayari kucheza mechi husika itajiamulia tu kufanya uhuni kama huu ikijua italipa faini na mechi kuahirishwa.
simba anazingua unaendaje kwenye uwanja bila taarifa kwa wahusika
 
Back
Top Bottom