Kwanza hao watu bilioni 5 wanatoka wapi. Ninavyo fahamu Mimi watazamaji wa hizo gemu zote almost ni wale wale (mutually inclusive).jambo ambalo Waziri wa Utalii, Ndumbaro na wengine hawakulizingatia wakati wanaruhusu timu ya Simba au Yanga iitangaze Tanzania na Utalii wa Tanzania kwa kwamba kama timu hiyo ikifanya vizuri na utalii unafanya vizuri pia na kama ikifanya vibaya na utalii unafanya vibaya, kama timu ikizomewa na utalii wetu utazomewa na kama ikishangiliwa na utalii utashangiliwa, kama mchezaji atawaonyesha wenzake kidole cha kati hata utalii wetu utaonyeshwa kidole cha kati pia, na kama mchezaji wa hiyo timu akivua bukta akabakia na chupi wakati wa kushangilia hivyohivyo hata utalii wetu utavuliwa bukta na kubaki na chupi. Kuipa timu ubalozi wa kutanga biashara yako sio kitu cha kufanyia mzaha na porojo porojo kama ilivyofanyika,
Kwanza timu nzima, wachezaji, wadhamini na viongozi na hata wale mashabiki kindakindaki wa timu walipaswa TANAPA ikae nao na ikibidi iwatembeze kwenye vivutio vyetu vya utalii ili wote wafahamu kile wanachokitangaza, kisha wapatiwe dos and don'ts zao kama mabalozi wetu wanapokuwa ndani na nje ya uwanja. Ndumbaro hakulifanya hilo, anadai watu 5b wameangalia mechi lakini hajui kuwa, ukiwaudhi watu 5b pia ni hatari sana kwenye utalii. Ndio maana watu wenye akili hawezi kutumia club za nchi yake kwenye ligi ya nyumbani kuandika Visit South Afrika, Visit England, Visit Egypt. Kama ni hivyo Al-Ahly timu kubwa Afrika ingekuwa na maandishi mwili mzima ya Visit Egypt kuwaita watu wakaone mapiramidi ya mafarao kule.
unaweza kuwavutia watu 5b lakini unaweza kuwafukuza watu 5b pia.
Kama mechi ya kwanza iliangaliwa na watu say 5,000,000 , mechi ya Pili nayo 5,000,000 si hasha ni wale wale wa mechi ya mwanzo kama kuna tofauti haiwezi kuzidi hata asilimia 1, na kila mechi inazidi kupunguza au isiwepo kabisa hiyo nyongezj ya watazamaji wapya, pamoja na kwamba unajiona bado umeangaliwa na watu milioni 5.
Hesabu ya 5b ni unrealistic kama lengo ndio hilo la kupata 1% of it.